Mwigulu Nchemba Ndani Ya Mara jumapili 30/11

Mwigulu Nchemba Ndani Ya Mara jumapili 30/11

acer

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Posts
1,595
Reaction score
142
Hima Hima wanamkoa wa Mara! Yule kijana wenu mtoto wa mfugaji alimaarufu "SOKOINE WA PILI " naibu Waziri wa Fedha na naibu Katibu mkuu Wa chama cha mapinduzi (CCM) Mh Mwigulu Lameck Nchemba. Kesho tarehe 30 atakuwa akinguruma ndani ya viwanja vya mkendo Musoma mjini! Hii sio ya kukosa jitokezeni kwa wingi ili mjue ukweli wa majambazi ya Tegeta Escrow account! ImageUploadedByJamiiForums1417277899.396264.jpgImageUploadedByJamiiForums1417277916.484256.jpg
 
Tunakusubiri kwa hamu sana hapa Mkendo Rais wetu 2015 wa Jamhiri ya muungano wa Tanzania. Tunaimani na Mwigulu Nchemba.
 
Jana hii Mwigulu akichangia Bungeni.
Mwigulu Nchemba: Ukububwa wa jambo
tunaongelea maadili na maslahi ya watanzania,
nitajikita eneo linalogusa wizara ya fedha.
Nazipongeza taasisi zote zilizoshiriki kwenye
ripoti hii(anazitaja). Tangu utaratibu huu uanze,
chimbuko la ripoti hii ni serikali yenyewe.
Kodi, imegawanyika maeneo matatu, VAT
haikukatwa na kukatokea mkanganyiko, TRA
inashughulikia na ni ilikua ni bilioni 26.97 lakini
baada ya kugundua kuna kodi ya wananchi
haijakusanywa ndipo wakakusanya bilioni 4.1
na ukaguzwa ni wa kwenye Escrow na sio IPT.
Niwahakikishie watanzania kuwa kodi hii
italipwa, hatuwezi kuacha kodi kwa tajiri halafu
tukimbizane na mama mjane anaeuza mchicha
barabarani.
Kodi ya pili ni iliyotokana na kukosewa kwa
mahesabu na ni lazima ilipwe, TRA
imeshaandika barua ya Novemba 2014 ya
kufuta cheti(certificate). Brela wameshapewa
notice ya kufuta capital gain certificate
iliyotolewa kipindi kilichopita. Hatua
imechukuliwa na serikali na tuko makini. Kuna
watu wasio waaminifu, kuna mtu badala ya
kuandika $ milioni 6 akaandika Tshs milioni 6
na badala ya kuandika $milioni 20 ameandika
Tshs 20. Naagiza mamlaka ya TRA ifanye
uwajibishaji wa ndani na akafanye kazi nyingi
na hakuna uchunguzi juu ya uchunguzi. Mtu
aliyeiba ukimfukuza kazi ni kumpa likizo
akatumie fedha alizoiba hivyo mamlaka husika
wachukue hatua. Tumeambiwa kuhusu pesa
zilizogawiwa, na wenyewe walipie kodi kabla ya
tarehe 31/12/2014. Baada ya tarehe hio TRA
wafatilieni mmoja mmoja. Kuna taarifa pesa
zilitoka kwenye mafurushi na magunia,
nimefatilia na wamefata sheria. Anatoa agizo
kwa Stanbic na Mkombozi watoe matamko,
wateja wao wana haki ya kujua reputation ya
benki yao. Niwaombe wabunge, kuna kuongea
na kuchukua hatua na watanzania wanasubiri
kuchukua hatua. Tumekua tunawachukulia
hatua wanasiasa lakini wataalamu
waliosomeshwa kwa kodi hawajibiki popote.
(Muda umeisha)
Kafulila: Benki ya stanbic wamemfukuza kazi
aliefungua akauti ya PAP amefukuzwa kazi
asharudi kwao Uganda hivyo hizi ni dalili kuwa
kuna makosa yalifanyika ndo maana hatua
zimechukuliwa.
Mnyaa: Nampongeza Nchemba kwa kusimama
katika ukweli, economic hitman ni kama Mafia,
na washawahi kuziangusha nchi(anazitaji)
 
Lini anaenda Switzerland kufuatilia mabilioni ya Uswiss $529 million kufuatilia taratibu za kuyarudisha hayo mabilioni ya walipa kodi wa Tanzania?
 
Danganya toto hiyo, ameshindwa kufuta misamaha ya kodi kwenye makampuni ynye kukwapua rasilimali zetu, ameshindwa kuwalipa wazee mafao yao, ameshindwa kufuatilia Trillions zilizoko Uswis kama wafanyavyo wakenya anakuja kujifagilia kiumbea umbea huku... Mara watamtoa nduki tu ...
 
Sisi wakazi wa musoma hatuhitaji upumbavuuu wa ccm,ngoja kesho tuwaonyeshe kazi nyie ukoo wa panya,na mkumbe juzi tu hapa mmemtukana mzee wetu jaji warioba
 
Lini anaenda Switzerland kufuatilia mabilioni ya Uswiss $529 million kufuatilia taratibu za kuyarudisha hayo mabilioni ya walipa kodi wa Tanzania?

Njoo kesho kwenye mkutano kisha umuulize hilo swali
 
Sisi wakazi wa musoma hatuhitaji upumbavuuu wa ccm,ngoja kesho tuwaonyeshe kazi nyie ukoo wa panya,na mkumbe juzi tu hapa mmemtukana mzee wetu jaji warioba

Unaikataa Neema? Utakuwa fisadi wewe maana mafisadi wote hawampendi Mwigulu
 
Usijibaraguze jibu swali, nani anataka kuja kwenye mikutano ya Maintarahamwe iliyojaa pumba!?

Njoo kesho kwenye mkutano kisha umuulize hilo swali
 
Back
Top Bottom