KasomaJr
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 368
- 144
Nimesikitishwa sana na kauli ya Mh. Mwigulu Nchemba, kwamba serikali inapaswa kupunguza viwango vya ufaulu vinavyoweza kuwapa fursa vijana wanaomaliza elimu ya kidato cha nne kujiunga na vyuo vya ualimu kwa gradi A. Huu binafsi naona ni upuuzi na muendelezo wa kudidimiza elimu ya nchi hii, na kwa tafsiri nyingine ni yale yale ya kuendelea kutowarendea haki wapiga kula, kwa maana kwamba kuendelea kuandaa tabaka tawaliwa.
Kudai alama za ufaulu zirudi kuwa point 28 & 29 toka 26 na zaid kama ilivyoamliwa na serikali hivi karibuni maana yake ni kwamba;
Mwigulu umeonyesha usivyo na uchungu na hali halisi ambayo imeendelea kuwa mbaya kwa shule zetu, na kwa msingi huo uzalendo wako ni sifuri bali umedhihirisha ubinafsi ule ule mlionao viongozi wengi. Nilitarajia utumie nafasi yako kuishawishi serikali na zaidi kutumia taaluma yako kuielekeza serikali yako namna bora katika kuinua viwango vya elimu kwa taifa lako.
Personally umenisikitisha sana sana.​
Kudai alama za ufaulu zirudi kuwa point 28 & 29 toka 26 na zaid kama ilivyoamliwa na serikali hivi karibuni maana yake ni kwamba;
- Tuendelee kutumia waalimu ambao wao binafsi hawakufaul lakini ndio hao watufundishie watoto wetu huko shule za kata, na matokeo yake bila shaka wote tunayafahamu.
- Kuifanya serikali isione umuhimu wa kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kujenga miungo mbinu kufanya mazingira bora ya kupata waalimu bora na walio faulu kwa viwango stahiki, na hatimaye kupata vijana walio faulu kidato cha nne kuweza kuendelea na kidato cha sita, vyuo nk.
- Kuendelea kutengeneza tabaka tawala na tawaliwa, kwani watakao endelea kuumia ni wale tu watoto wetu wanaosoma shule za misingi huko vijijini ambako miundo mbinu imeendelea kuwa mibovu kwa miaka mingi sasa.