Mwigulu Nchemba: CHADEMA itakufa 2015

Mwigulu Nchemba: CHADEMA itakufa 2015

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Posts
4,789
Reaction score
1,732
nchemba.jpg

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba

CHAMA Cha Mapinduzi kimekitabiria kifo Chadema baada ya uchaguzi wa 2015 kikieleza kuwa CCM ikishinda, chama hicho kitakuwa hakina nguvu tena kwa kuwa Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa atakuwa amechoka.


Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba aliliambia gazeti hili jana kuwa chama hicho kinapoteza umaarufu kadri siku zinavyokwenda hasa kutokana na siasa zake za uchochezi na mwaka 2015 ndio itakuwa mwisho wa chama hicho.


Alisema kitakufa na kitasahaulika kabisa, akisema sasa hivi vijana wameshaanza kuwakimbia, na kwamba anaamini pia baada ya 2015 hakuna diwani ambaye atagombea kupitia chama hicho.


Alisema pia ni mwaka ambao Katibu wa Chadema Willibrod Slaa amestaafu kwa kuwa alishatangaza asiposhinda atastaafu na Chadema haiwezi kushinda hivyo mwisho wa Dk Slaa ndio utakuwa umefika kwa kuwa nyota yake haitang'aa tena.


"Nguvu ya Dk Slaa aliyokuwa nayo miaka miwili iliyopita sio aliyonayo sasa na mpaka mwaka 2015 atakuwa ameisha kabisa." alisisitiza.


Pia Mwigulu aliyataka makundi yaliyojichomoza ndani ya CCM ikiwa ni harakati za kuwania urais mwaka 2015 kuheshimu ilani ya chama hicho kwa kuitekeleza na kuisimamia kwa kutoleta vurugu ndani ya chama wala kujenga chuki kwa wale ambao hawawaungi mkono.


|"CCM ina utaratibu wake wa kupata mgombea na hatumzuii mtu kugombea, sisi kama kamati ya utendaji tunatekeleza maagizo aliyotoa mwenyekiti tutayasimamia kwa nguvu zote anayetaka kugombea ahakikishe havurugi chama na asitengeneze chuki kwa ambao hawamuungi mkono."


Wakati huohuo Naibu Katibu huyo wa CCM na Mbunge wa Iramba Mashariki aliwataka wakazi wa Mtwara kuachana na propaganda zinazoenezwa na wapinzani kuhusu rasilimali ya gesi na badala yake wafanye kazi kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.


"Rasilimali iliyopo ni ya taifa na watafaidika, hakuna rasilimali ya wilaya fulani, bomba la gesi ni lazima lijengwe tutawaelimisha wakazi wa Mtwara, kwani hata Ziwa Victoria bomba lilijengwa kwenda Shinyanga badala ya Kwimba, kwa nini basi halikujengwa kwenda Kwimba wakati pale ni karibu zaidi.


"Utajiri unategemea na jitihada, wasitegemee kwa vile tuna rasilimali ya gesi basi wakae wategemee watapata utajiri bila ya kufanya kazi haiwezekani, wasisubiri kupewa vya bure, ni kama mikoa yenye madini halafu wakazi wa pale wategemee Serikali itawapa vocha za kuweka kwenye simu kwa vile madini yao kwao, haiwezekani ni lazima wafanye kazi.

Source: Mwananchi

My take:

- Attention ya CCM ni Dr. Slaa.
 
Kumbe Wanaijua Nyota ya Dr. Slaa ndio maana hawalali kupandikiza Masalai, tunguli nk?

Nawaakikishia, Mwigulu Nchemba atakufa
yeye Akifanya URODA kabla ya CHADEMA. Chadema ni movement ya Watanzania millioni 44. Kwa hiyo ili CHADEMA kife, ni bora awaue watanzania hao wanaoishabikia CHADEMA. Mbona akili zao zinawaza CHADEMA tu na sio mke wao wa Ndoa CUF?
 
Alisema pia ni mwaka ambao Katibu wa Chadema Willibrod Slaa amestaafu kwa kuwa alishatangaza asiposhinda atastaafu na Chadema haiwezi kushinda hivyo mwisho wa Dk Slaa ndio utakuwa umefika kwa kuwa nyota yake haitang’aa tena.
Sasa nimeelewa kwa nini CCM wahahunyahunya na harakati za kumchafua Dr. Slaa; kumbe Bwana huyo ni noma kwao!
Jambo jingine pia nililokuwa silifahamu ni kwamba mtu akiwa m-CCM hata akili kidogo alizojaliwa hupeperushwa na hubaki mweupee kama kijana huyu niliyekuwa namheshimu kama msomi.
Kutapatapa kwa CCM ni daalili tosha kwamba CHADEMA wamewashika CCM pabaya na sasa wame-resort kutapatapa na kauli za ki ramli ramli vile!

Kinachopaswa kufanywa na CHADEMA kwa sasa ni kuongeza mbinyo kwa walegevu hawa kabla ya kuwashushia pigo kubwa litakalowaduwaza na kuwamaliza kabisa 2015.
Wamejaribu kila njia na kushindwa vibaya. Wamejaribu kuwanunua viongozi (kina Kaburu, Akwilombe na wengine watakaofuata) wameangukia pua; wameweka mapandikizi ya kina Shibuda na Shonza - wapi! wamejaribu kutumia Polisi 'kuwanyonga' walioonekana kushabikia CHADEMA kama walivyofanya kule Arusha, Songea, Morogoro, Iringa na sehemu kadhaa; wapi. Wametumia Usalama wa Taifa kuwateka, kuwatesa na hata kuwasababishia ulemavu lakini ndiyo kwanza wameimarika zaidi! Na hili la sasa la kuropokaropoka mithili ya mtu aliyefunguliwa toka kwenye kibuyu litashindwa vibaya kama lile la kijinga la ati Dr. Slaa ana kadi yao na wanapokea ada yake! Naona wamefyata baada ya kubanwa na vipengele vya Katiba yao wenyewe. Na sasa wamerukia fani za watu - za unajimu na ramli - watashindwa na kuaibika vibaya pia!
Waacheni waweweseke jamani ukoloni ni mtamu kwa mtawala, si mmeona jinsi ilivyokuwa vigumu kuwaondoa wareno na walowezi kule kusini?
Mwisho nasema tu CHADEMA ni A luta continua!


 
Yaani taabu kwelikweli, CCM wanafikiri CHADEMA ni Dr. Slaa!?? na kauli hizo zinatolewa na mtu mwenye nafasi nyeti kama hiyo kwenye chama!!? afu waandishi wa habari nao wakumbuke sio kila limtokalo mtu kinywani ni habari, njaa zitawadhalilisha sana
 
kwel Mwigulu. CHADEMA itakufa kabla ya hata ya yauchaguz mm nifahamu.

Dr Slaa yupo pale kufukuza wanaompinga mabadiliko acha kife r.i.p CHADEMA
 
Kwa ujumla hapa hapakuwa na kitu cha maana cha kusema kwa sababu yote ni kama marudia. Kufa kwa CHADEMA unakuwa Wimbo wake wa kila siku. Namshauri basi apeleke hoja binafsi Bungeni kuomba Bunge liridhie kufutwa kwa vyama vingi ili ibaki CCM tu maana ndicho kinachoonekana kuwa malengo ya Bw. Nchemba. Inasikitisha kuona kija anakuwa na maono ya aina hii, katika ulimwengi wa siasa za kisasa vyama vingi ni muhimu ili kuendelea kuwajibishana na kusukuma maendeleo ya nchi kwa kasi, haki na usawa.

Kwa maana nyingine kurudi katika mfumo wa chama kimoja anachotaka Nchemba ni sawa na kuua siasa ya Tanzania, tulitarajia ajikite katika kuwaelimisha wananchi namna ya kujiletea maendeleo baadala ya kuwa mtabiri wa vifo ya vyama vya siasa, tunaipeleka wapi nchi yetu. Cha ajabu zaidi wapo watu ambao wanashangilia utumbo ulipo katika kauli kama hizo.

Wewe Rais ameongelea suala la gesi, waziri husika ameongelea wewe nani kuja kusema lazima bomba lijengwe. Tumaieni hoja kuwaelimisha wananchi kwa nini ni muhimu kujengwa kwa njia hiyo ya kusafirisha gesi siyo tu kusema lazima ijengwe, walekeze sababu wakuelewe ili wasije baadaye kusabortage huo mradi.

Halafu ni vyema kuita media pale tu ambapo unahoja ya maana kusema, sasa hapo kwenye taarifa yote hiyo nini kipya, navyo vyombo vyetu vya bahari kwa sababu ya njaa vinadika kila kitu hata ambavyo havina impact yoyote kwa jamii.

Tubadilike, kama umechagua siasa fanya siasa kitaalam ili tuone kweli wewe siyo mwanasiasa njaa na mtabiri wa vifa vya vyama vya siasa na kuastaafu kwa baadhi ya wanasiasa ambao unadhani kwako wewe ni kikwazo cha survival yako.
 
kwel mwigulu.cdm itakufa kabla ya hata ya yauchaguz mm nifah.dr slaa hupo pale kufukuza wanaompinga mabadiliko acha kife kile kizee kihamie adc.r.i.p chadema

Jifunze kuandika wewe!! alaa
 
kwel mwigulu.cdm itakufa kabla ya hata ya yauchaguz mm nifah.dr slaa hupo pale kufukuza wanaompinga mabadiliko acha kife kile kizee kihamie adc.r.i.p chadema

Kati ya wale masalia wewe ni nani? Unaonekana wewe ndiye ulikuwa mjinga kuliko wote.Eti hili ndio kundi lililokuwa limepanga kumpindua Mbowe.Shame!!
 
Sijawahi kuona mtu wa ajabu katika tasnia ya siasa kaa Mwigulu Nchemba. Kila kukicha nikuropoka. Yeye anajua CCM kuna makundi kwa nini asiseme nayo itakufa kutokana na makundi hayo.

Mimi naamini ng'ombe haelemewi na nundu yake, migogoro iliyopo CDM ni kama nundu au viraka barabarani havizui kuendelea na safari.
 
Sasa nimeelewa kwa
nini CCM wahahunyahunya na harakati za kumchafua Dr.
Slaa; kumbe Bwana huyo ni noma kwao!
Jambo jingine pia nililokuwa silifahamu ni kwamba mtu akiwa m-CCM hata
akili kidogo alizojaliwa hupeperushwa na hubaki mweupee kama kijana huyu
niliyekuwa namheshimu kama msomi.
Kutapatapa kwa CCM ni daalili tosha kwamba CHADEMA wamewashika CCM
pabaya na sasa wame-resort kutapatapa na kauli za ki ramli ramli vile!

Kinachopaswa kufanywa na CHADEMA kwa sasa ni kuongeza mbinyo kwa
walegevu hawa kabla ya kuwashushia pigo kubwa litakalowaduwaza na
kuwamaliza kabisa 2015.
Wamejaribu kila njia na kushindwa
vibaya. Wamejaribu kuwanunua viongozi (kina
Kaburu, Akwilombe na wengine watakaofuata) wameangukia pua;
wameweka mapandikizi ya kina Shibuda na Shonza - wapi!
wamejaribu kutumia Polisi 'kuwanyonga' walioonekana kushabikia
CHADEMA kama walivyofanya kule Arusha, Songea, Morogoro, Iringa
na sehemu kadhaa; wapi. Wametumia Usalama wa Taifa kuwateka, kuwatesa na
hata kuwasababishia ulemavu lakini ndiyo kwanza wameimarika zaidi! Na
hili la sasa la kuropokaropoka mithili ya mtu
aliyefunguliwa toka kwenye kibuyu litashindwa vibaya kama lile la
kijinga la ati Dr. Slaa ana kadi yao na wanapokea ada yake! Naona
wamefyata baada ya kubanwa na vipengele vya Katiba yao
wenyewe. Na sasa wamerukia fani za watu - za unajimu na ramli -
watashindwa na kuaibika vibaya pia!

Waacheni waweweseke jamani ukoloni ni mtamu kwa mtawala,
si mmeona jinsi ilivyokuwa vigumu kuwaondoa wareno na walowezi kule
kusini?
Mwisho nasema tu CHADEMA ni A luta
continua!




aka mkosa chama tatizo la Watz tunashabikia tusilolijua kwani hamjua vita iliyopo cdm? kama hamjui hicho chama cha wachaga mtadanganyika mpaka lini fuatilieni mtaona au ni chama cha mzee Mtei
 
Kati ya wale masalia wewe ni nani? Unaonekana wewe ndiye ulikuwa mjinga kuliko wote.Eti hili ndio kundi lililokuwa limepanga kumpindua Mbowe.Shame!!

Mkuu Molemo hapo ndipo niliposhangaa! Kiukweli ukiangalia mabandiko yao masalia na mpangilio wa maneno yao ya utetezi wa kipuuzi unagundua ni watu wenye upeo mdogo sana!! Tena ni wote sio mmoja!
 
Mimi naamini kuwa Mungu amewapiga upofu CCM kiasi kwamba hawamjui wala hawamuoni adui yao wa kweli, wamefocus kwa Dr na CHADEMA. Adui wa CCM kwa sasa sio Dr wala CHADEMA bali ni UMMA wa watanzania na Mungu wa watanzania. Hii ndiyo nguvu ama nyota ya Dr na CHADEMA. Hii ndiyo maana hata CCM walipojaribu kutumia pesa, mapandikizi na Masalia kumchafua Dr, wamejikuta wakitawanywa na wamebaki wakiangaliana na kuulizana "what happened?"
 
Back
Top Bottom