Mwigulu Nchemba atua Machinjio ya Vingunguti usiku huu, akuta kodi

ukwelinauwazi

Member
Nov 24, 2014
71
91
1558428_929149373805554_7019256894256114543_n.jpg
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,Mh.Mwigulu Lameck Nchemba akisikiliza kero za wadau wa machinjio ya Vingunguti usiku huu wa January 1/01/2016.
1682_929149433805548_7776065019326928329_n.jpg
Mwigulu Nchemba akishuhudia Ng'ombe aliyetayari kwa taratibu za kuchinjwa kwaajili ya kitoweo.

10336793_929149423805549_5813147724928826829_n.jpg
Mbuzi wakiwa tayari kwaajili ya kuchinjwa kwenye machinjio hayo ya Vingunguti.Mbuzi hawa asilimia kubwa wanatoka mnada wa pugu ambao Ushuru wake unakusanywa na serikali kuu.
10348287_929149357138889_3144989189231161392_n.jpg
Waziri Mwigulu Nchemba akikagua maeneo ya machinjio hayo usiku huu.

1654063_929149367138888_8865657160090386502_n.jpg
Mwigulu Nchemba akitoa maagizo kwa uongozi wa Machinjio ya Vingunguti kukutana kesho saa 2:00 asubuhi kwa wahusika wote wenye dhamana na Machinjio hayo,Mkutano utafanyika eneo la Machinjio hayo.


Katika hatua ya kushitukiza,Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba amefanya ukaguzi wa Machinjio ya Vingunguti usiku huu.

Mh. Mwigulu Nchemba amefika kwenye Machinjio hayo usiku huu ilikushuhudia Mifugo ikiandaliwa kwaajili ya kitoweo cha wananchi.Uchinjaji wa Ng'ombe na Mbuzi katika machinjio haya hufanyika nyakati za Usiku kuanzia saa 4 hadi 10 alfajiri.

Mbali na kusikiliza kero na maoni ya wananchi kuhusu uendeshwaji wa Machinjio hayo,Mwigulu Nchemba ameshuhudia utafunwaji wa kodi ya serikali inayokusanywa kwenye mnada wa pugu.

Utafunwaji huo unatokana na uandikaji wa kibali cha mifugo michache kuja Machinjioni ili hali mifugo Zaidi huingizwa machinjioni bila kibali.Matharani hii leo Mh.Waziri ameshuhudia Ng'ombe waliotoka mnada wa pugu ambao wameshalipiwa kodi wakiwa 1450 lakini kibali chake kimeandikwa Ng'ombe 300 tu.Inamana kuna ng'ombe 1150 wamelipiwa ushuru lakini machinjioni kimeletwa kibali cha ng'ombe 300 wakati kwa kuwahesabu ng'ombe hao wanazidi 1000.

Kutokana na hali hiyo,Mh.Waziri ameagiza wahusika wote kufika kesho kwenye mkutano wa asubuhi kwaajili ya hatua stahiki kuchukuliwa,Mwigulu amesisitiza kuwa kwa mtu yeyote mwenye dhamana na kusimamia sekta ya kilimo,Mifugo na Uvuvi afanya kwa mujibu wa sharia,vinginevyo hakutakuwa na huruma kwa wanaohujumu.
 
Last edited by a moderator:
Wahujumu UCHUMI hawatapona katika awamu ya 5. Twende kazi Field Marshall Komredi Mwigulu.
 
Kwa kweli nimependa hii

Lazima walifikiri hawataguswa sababu ni usiku.

Hapa kazi tu


Oyeeee Mh.Magufuli

Ukitembelea hizo machinjio kwa jinsi hali ya usafi ilivyo unaweza geuka vegetarian. Ni aibu hadi leo ng'ombe wanachinjwa wakiwa wamelazwa chini badala ya stunning n.a. kisha kuchinjwa usafi ukizingatiwa. Sishangai supermarket kuagiza nyama tokà nje
 
Mi ningetamani Waziri wa Mambo ya Ndani aende UWANJA WA FISI ashuhudie POMBE (iikiwemo GONGO) inauzwa mpaka kwa watoto huku pembezoni kuna vyumba zaid ya 70 vya MAKAHABA wakipiga kazi kama vile wapo TRINIDAD & TOBAGO.
 
Ukitembelea hizo machinjio kwa jinsi hali ya usafi ilivyo unaweza geuka vegetarian. Ni aibu hadi leo ng'ombe wanachinjwa wakiwa wamelazwa chini badala ya stunning n.a. kisha kuchinjwa usafi ukizingatiwa. Sishangai supermarket kuagiza nyama tokà nje

Na mimi nimeona ila siku hizi nikiona kama Ng'ombe au Mbuzi mzima akichinjwa simli naona na mimi naelekea huko nilimaliza kuangalia picha nimebaki na kama bado naona huyo ng'ombe mweusi aliyelala pale chini.

Natumaini Waziri atajali kuhakikisha usafi nao unakuwa unawekwa mbele kwanza.
 
Tatizo Wabongo mnapenda na mnapumbazwa sana kwa mambo madogo yasiyokuwa na tija kwa Taifa. Hivi zile siku saba za kulipa kodi wa zile kontena zimeishia wapi na nini kimefanyika mpaka sasa?
Kama umeshajua tatizo letu Wabongo rudi kwenu Kenya nyang'au we.
 
kwani Ng'ombe moja ushuru kiasi gani. minada na machinjio duni kumbe kuna majizi yanatafuna 80% ya kodi.
 
Adhabu kwa mkwepa kodi ni ndogo sana ndio sababu wataendelea bila uoga. Mabadiliko ya sheria ni lazima ili kokomesha ukwepaji kodi.
Kama serekali imeamua kutangaza vita kwa wakwepa kodi waonyeshe nia kwa vitendo sio ambushi inayofanywa na mawaziri.
 
Kama umeshajua tatizo letu Wabongo rudi kwenu Kenya nyang'au we.

Unataka tukuletee taarifa chumbani kwako?


Majibu ya usiku

kwani Ng'ombe moja ushuru kiasi gani. minada na machinjio duni kumbe kuna majizi yanatafuna 80% ya kodi.

Hawajataja ili kuficha aibu..maana mazingira ya machinjio hayaridhishi kabisa,wataje ili tujue mapato yanayokusanywa na maboresho ya machijio kama vinaendana,

Naamini wapo member humu wanaojua watataja gharama ya ushuru kwa kila ng'ombe ni ngapi


Screenshot_2016-01-02-04-17-31_zpsi9kje6ot.png


kuna nuka ?Naona huyu kaziba pua
 
Last edited:
Hii nchi ina vyanzo vingi kweli vya mapato. Sometimes unashangaa tunashindwaje kumudu huduma ndogo tu kama maji safi na salama kwa wananchi.
 
Wish every Tanzanian should be vegetarians. Look at those poor mbuzis and ng'ombez
 
Last edited:
Back
Top Bottom