Mwigulu: Kuna vyama vinaendeshwa kama SACCOS...

Mwigulu: Kuna vyama vinaendeshwa kama SACCOS...

Taswira

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2012
Posts
1,198
Reaction score
452
images

Mh.Mwigulu nchemba leo Tar.6/08/2013 amefanya mahojiano na mlimani tv ofisi ndogo za CCM-Lumumba.
Mwandishi wa mlimani tv alikuwa na uhitaji wa kujua nini maoni ya Mh.Mwigulu nchemba(Naibu Katibu mkuu wa CCM Tanzania bara) kuhusu utendaji kazi wa msajili wa vyama vya siasa aliye staafu Mzee J.Tendwa.

images

Mh. Mwigulu Nchemba alikuwa na haya ya kusema "Kwanza kabisa napenda kutoa pongezi za dhati kabisa kabisa,namshukuru sana Mzee wetu J.Tendwa kwa namna alivyotuongoza vyama vya siasa hadi kufikia hapa. Kimsingi mzee wetu ametulea,ametuvumilia sana na amekuwa na busara sana katika maamuzi yake.Naamini angeamua kushikilia sheria kuna vyama vya siasa leo hii visingekuwepo, yaani ingebaki CCM tu.


Uongozi wa mzee wetu J.Tendwa haukuwa wa kiimla,ameongoza kwa kuzingatia demokrasia ya vyama vingi na amekuwa sehemu na kiungo kikubwa cha ujenzi wa demokrasia halisi ndani ya taifa letu.
Nasema haya kwa sababu kunavyama vinaendeshwa kama SACCOS au NGO flani,havina demokrasia yoyote kama vinavyojipambanua.Kuna vyama ndani ya nchi yetu tangu Uongozi wa Rais Mstaafu Mwinyi,Rais Mkapa hadi Rais Kikwete havieleweki na havitabiliki ni lini vitafanya uchaguzi wa uongozi ndani ya vyama vyao. Yaani mwenyekiti ni yuleyule kuanzia chama kinaanzishwa enzi hizo hadi leo,Je hii ndio demokrasia?,Mzee J.Tendwa ametulea sana,na anastahili pongezi za dhati kabisa kabisa.
DSC00518.jpg

MALALAMIKO YA VYAMA VYA UPINZANI KUHUSU UTENDAJI KAZI WA MZEE J.TENDWA.

Mh.Mwigulu Lameck Nchemba ,Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara alikuwa na haya ya kusema "Kwanza napenda kusema hakuna kazi ya binadamu isiyokuwa na mapungufu,vivyo hivyo kwenye utendaji kazi wa mzee wetu J.Tendwa yawezekana kunasehemu alikuwa na mapungufu yake lakini asilimia zaidi ya 90 amefanya kazi yake vizuri na ameijengea nchi yetu heshima kubwa sana kitaifa na kimataifa kuhusu uimara wa demokrasia ya vyama vya siasa ndaniya nchi.
Lakini niseme jambo,hao hao mnaosikia wanalalamika kuhusu msajili wa vyama vya siasa,ukiwapa wao waendeshe nyumba hii ya siasa hawawezi,yaani chama/vyama chao chenyewe kimewashinda ndio wataweza kuendesha nyumba ya siasa?. Chama kinajipambanua kuwa nichakidemokrasia,lakini vita ya madaraka haziishi,Mwenyekiti na timu yake ya uongozi hakuna maelewano.Katibu na naibu wake ni kama paka na panya.Chama kuanzia matendo yake na uongozi wake ni NGO au SACCOS kama sio familia.

Sasa kama yakwao yamewashinda kiasi hiki cha kutisha,wataweza kuendesha nyumba ya siasa?. Mzee J.Tendwa amevilea vyama hivi vizuri sana licha ya uchanga wao kwenye ulimwengu wa siasa za vyama vingi. Biblia inasema usimnyime mtoto mapigo kwasababu atakufa. Hivyo hekima na busara za msajili wa vyama vya siasa aliyestaafu ndio imetufikisha hapa(vyama vya siasa) tunajivunia uwepo wetu katika ulimwengu wa siasa. Unajua hakuna jambo baya na hatari kama kujiona wewe ni bora kuliko mwingine,yaani mawazo yako ndio kila kitu.

Ukifanya jambo wewe na kuliongelea ndio lipo sahihi zaidi kuliko la mwingine, Ni hatari kuona watu wanatoka kwenye ramani kabisa ya siasa,baada ya kuwa wapinzani wa kisiasa sasa ni wapinzani wanchi.
Naamini amefanya kazi nzuri sana mzee wetu,wale wanaolalamika tunajua ndio tabia yao bila kulalamika hawaishi.Lakini itakuwa safi sana kama watajitazama wao kwanza ndipo wanyoshe kidole kwa mwingine.

Pia naomba wasije wakawa kama wale wa misri,walitumia nguvu sana kuiondoa serikali iliyokuwepo madarakani,wakaiweka serikali waliyokuwa wanataka,hata miezi sita haijaisha wanatumia nguvu kubwa zaidi kuiondoa serikali waliyoiweka wao wenyewe. Yaani haielweki nini wanakitaka? Mwisho wa siku ni vurugu na malumbano yasiyoa na tija.


UNAZUNGUMZIAJE KUHUSU MSAJILI MPYA ALIYETEULIWA WA VYAMA VYA SIASA HAPA NCHINI (MUTUNGI).


Mh.Mwigulu Nchemba alikuwa na haya ya kusema
"Niimani yangu kuwa Rais amefanya uteuzi sahahi kabisa,ameona mbali na amemuamini kuwa ataendesha nyumba ya siasa vyema kabisa.Nategemea na niombi kuwa awe mlezi wa vyama vya siasa,akishikiria sharia sana basi ipo siku nchi hii itabakia na chama kimoja tu CCM kwasababu vyama vingi havifuati misingi ya demokrasia,vinajiendesha kama SACCOS.
Tunaamini katika uongozi wake ataendana na katiba ya nchi kuhusu vyama vya siasa,hasa hii katiba mpya tunayoipigania.Tunaamini ataendeleza ujenzi wa demokrasia safi,siasa za sera na sio siasa za MISITUNI. Unazungumziaje kuhusu nane nane.

Mh.Mwigulu Nchemba amesema|"Nawatakia nane nane njema watanzania wote,wakulima watumie nafasi hiyo kujifunza njia mpya za uzalishaji bora,fusa za masoko nan chi iendelee kuneemeka na kilimo. Pia nawatakia waislamu wote kumaliza salama mfungo wa Ramadhani,tudumishe amani na upendo sisi sote ni ndugu,hakuna wa kututenganisha.Tuendelee kuliombea amani Taifa letu,tuwapuuze wote wanaojitahidi kuleta kauli za uchochezi,utengano na uvunjifu wa amani.

Asante.
 
Kaka Mwigulu kila analofanya anagonga mwamba,tekelezeni ahadi mlizo ahidi 2010 kama hamuwezi achieni ngazi kwa mh Lema
 
kila swali anajibu 'vyama', 'vyama', 'vyama'; si ataje tu cdm! Au basi aongelee chama chake. Sijui wasomi wote hasa wa grade one ndivyo walivyo hivi!!!
 
Jamani kwakweli mwigulu ni kituko,namuomba mwenyekiti wa ccm atuondoshee hili nduli mapema kabla chama hakija sambaratika.
 
Mbona hakuongelea kesi ya ugahidi aliyo wafungulia makamanda wa
cdm kule Tabora imeishia wapi?kweli gaidi hajitambui
 
Kuna wanasiasa wanaoweza wakasema kitu na ukakielewa lakini si huyu.
 
Nimechoka hata kusikia ya Mbunge wangu, maana ni majanga tu kila kukicha-ONA LEO KAIBUKIA HUKU TENA.
 
Mwigulu bado naona anayo safari ndefu ya kuwa mwanasiasa makini mwenye kutoa hoja za kitaifa, kwa sasa naona yuko hovyo na kila jambo anasema bila kufikri hata waandishi wanaotaka kupata maoni ya mwigulu naona wamepungiwa upeo hivi hakuna watu wengine wa kuhoji waseme mambo ya maana_
 
Mwandishi yeyote wa habari anayeenda kuchukua maoni ya jambo lolote linahusu siasa na uchumi kwa Mwigulu Nchemba ana uwezo mdogo kifikra na ni kajanja. Hivi unategemea maoni gani ya maana kutoka kwa mtu kama Mwigulu? Huyu mtu ana akili ndogo atawezaje kutoa tathmini ya masuala ya kisiasa?

Mwandishi wa habari wakati mwingine inabidi ujiulize mara mbilimbili unapotaka kufikia uamuzi wa kwenda kumhoji Mwigulu, vinginevyo ni kujichafulia CV na integrity bure.
 
Huyu jamaa ni fyatafyata sijui kama anajua maana ya SACCOSS. Tukisema linalopoka mnabisha
 
haaaa haaa haaaa .... sasa hoja ya ugaidi ameshindwa amerukia saccos
 
Mh.Mwigulu nchemba leo Tar.6/08/2013 amefanya mahojiano na mlimani tv ofisi ndogo za CCM-Lumumba. Mwandishi wa mlimani tv alikuwa na uhitaji wa kujua nini maoni ya Mh.Mwigulu nchemba(Naibu Katibu mkuu wa CCM Tanzania bara) kuhusu utendaji kazi wa msajili wa vyama vya siasa aliye staafu Mzee J.Tendwa.

Mh. Mwigulu Nchemba alikuwa na haya ya kusema “Kwanza kabisa napenda kutoa pongezi za dhati kabisa kabisa,namshukuru sana Mzee wetu J.Tendwa kwa namna alivyotuongoza vyama vya siasa hadi kufikia hapa. Kimsingi mzee wetu ametulea,ametuvumilia sana na amekuwa na busara sana katika maamuzi yake.Naamini angeamua kushikilia sheria kuna vyama vya siasa leo hii visingekuwepo, yaani ingebaki CCM tu.

Uongozi wa mzee wetu J.Tendwa haukuwa wa kiimla,ameongoza kwa kuzingatia demokrasia ya vyama vingi na amekuwa sehemu na kiungo kikubwa cha ujenzi wa demokrasia halisi ndani ya taifa letu. Nasema haya kwa sababu kunavyama vinaendeshwa kama SACCOS au NGO flani,havina demokrasia yoyote kama vinavyojipambanua.Kuna vyama ndani ya nchi yetu tangu Uongozi wa Rais Mstaafu Mwinyi,Rais Mkapa hadi Rais Kikwete havieleweki na havitabiliki ni lini vitafanya uchaguzi wa uongozi ndani ya vyama vyao. Yaani mwenyekiti ni yuleyule kuanzia chama kinaanzishwa enzi hizo hadi leo,Je hii ndio demokrasia?,Mzee J.Tendwa ametulea sana,na anastahili pongezi za dhati kabisa kabisa.

MALALAMIKO YA VYAMA VYA UPINZANI KUHUSU UTENDAJI KAZI WA MZEE J.TENDWA
.

Mh.Mwigulu Lameck Nchemba ,Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara alikuwa na haya ya kusema “Kwanza napenda kusema hakuna kazi ya binadamu isiyokuwa na mapungufu,vivyo hivyo kwenye utendaji kazi wa mzee wetu J.Tendwa yawezekana kunasehemu alikuwa na mapungufu yake lakini asilimia zaidi ya 90 amefanya kazi yake vizuri na ameijengea nchi yetu heshima kubwa sana kitaifa na kimataifa kuhusu uimara wa demokrasia ya vyama vya siasa ndaniya nchi. Lakini niseme jambo,hao hao mnaosikia wanalalamika kuhusu msajili wa vyama vya siasa,ukiwapa wao waendeshe nyumba hii ya siasa hawawezi,yaani chama/vyama chao chenyewe kimewashinda ndio wataweza kuendesha nyumba ya siasa?. Chama kinajipambanua kuwa nichakidemokrasia,lakini vita ya madaraka haziishi,Mwenyekiti na timu yake ya uongozi hakuna maelewano.Katibu na naibu wake ni kama paka na panya.Chama kuanzia matendo yake na uongozi wake ni NGO au SACCOS kama sio familia.

Sasa kama yakwao yamewashinda kiasi hiki cha kutisha,wataweza kuendesha nyumba ya siasa?. Mzee J.Tendwa amevilea vyama hivi vizuri sana licha ya uchanga wao kwenye ulimwengu wa siasa za vyama vingi. Biblia inasema usimnyime mtoto mapigo kwasababu atakufa. Hivyo hekima na busara za msajili wa vyama vya siasa aliyestaafu ndio imetufikisha hapa(vyama vya siasa) tunajivunia uwepo wetu katika ulimwengu wa siasa. Unajua hakuna jambo baya na hatari kama kujiona wewe ni bora kuliko mwingine,yaani mawazo yako ndio kila kitu.

Ukifanya jambo wewe na kuliongelea ndio lipo sahihi zaidi kuliko la mwingine, Ni hatari kuona watu wanatoka kwenye ramani kabisa ya siasa,baada ya kuwa wapinzani wa kisiasa sasa ni wapinzani wanchi. Naamini amefanya kazi nzuri sana mzee wetu,wale wanaolalamika tunajua ndio tabia yao bila kulalamika hawaishi.Lakini itakuwa safi sana kama watajitazama wao kwanza ndipo wanyoshe kidole kwa mwingine.

Pia naomba wasije wakawa kama wale wa misri,walitumia nguvu sana kuiondoa serikali iliyokuwepo madarakani,wakaiweka serikali waliyokuwa wanataka,hata miezi sita haijaisha wanatumia nguvu kubwa zaidi kuiondoa serikali waliyoiweka wao wenyewe. Yaani haielweki nini wanakitaka? Mwisho wa siku ni vurugu na malumbano yasiyoa na tija.

UNAZUNGUMZIAJE KUHUSU MSAJILI MPYA ALIYETEULIWA WA VYAMA VYA SIASA HAPA NCHINI (MUTUNGI).

Mh.Mwigulu Nchemba alikuwa na haya ya kusema
“Niimani yangu kuwa Rais amefanya uteuzi sahahi kabisa,ameona mbali na amemuamini kuwa ataendesha nyumba ya siasa vyema kabisa.Nategemea na niombi kuwa awe mlezi wa vyama vya siasa,akishikiria sharia sana basi ipo siku nchi hii itabakia na chama kimoja tu CCM kwasababu vyama vingi havifuati misingi ya demokrasia,vinajiendesha kama SACCOS. Tunaamini katika uongozi wake ataendana na katiba ya nchi kuhusu vyama vya siasa,hasa hii katiba mpya tunayoipigania.Tunaamini ataendeleza ujenzi wa demokrasia safi,siasa za sera na sio siasa za MISITUNI. Unazungumziaje kuhusu nane nane.

Mh.Mwigulu Nchemba amesema|”Nawatakia nane nane njema watanzania wote,wakulima watumie nafasi hiyo kujifunza njia mpya za uzalishaji bora,fusa za masoko nan chi iendelee kuneemeka na kilimo. Pia nawatakia waislamu wote kumaliza salama mfungo wa Ramadhani,tudumishe amani na upendo sisi sote ni ndugu,hakuna wa kututenganisha.Tuendelee kuliombea amani Taifa letu,tuwapuuze wote wanaojitahidi kuleta kauli za uchochezi,utengano na uvunjifu wa amani.

Asante.

Savimbi Nchemba; (May burn in hell!) hawezi kukiri udhaifu wa Tendwa kwa sababu ndio uliomuwezesha kuendesha siasa za chuki, mabomu, polisi kubambikia watu kesi hewa za ugaidi na matumizi ya jeshi la polisi kufanya ghasia na kusigina demokrasia.
 
Hapa aliyepungukiwa akili ni huyu mwandishi aliyeenda kumhoji Mwigulu..Maana amekuwa kama yule aliyetoka uchi akimfukuza kichaa aliyebeba nguo zake wakati anaoga!! Ukienda kumhoji mtu kama Nchemba unategemea jipya gani??
 
Back
Top Bottom