Mwigulu: Kuna mchezo unachezwa, kwanini wanaouawa Pwani ni viongozi wa CCM pekee?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,936
19,129
Mwigulu amesema kuna mchezo unachezwa na anapatwa maswali, anasema mwanzo tafsiri ilikuwa ni kuhusu mkaa, lakini mkaa na viongozi wa mkaa na CCM kuna muunganiko gani?

Ikaja tafsiri nyingine ya misimamo mikali ya kidini, misimamo mikali ya kidini wapi na wapi na CCM?

Ikaja tasfiri ya ujambazi, lakini ujambazi na CCM wapi na wapi hadi watafutwe viongozi wa CCM hadi waliostaafu?

Ikaja tafsiri ya ugaidi, lakini ugaidi na CCM chuki itakuwa imetoka wapi? Na huyo anayeonyesha viongozi wa CCM ni nani, anaonyesha viongozi wa CCM waliostaafu na yeye atakuwa ni muuaji pia.

Na kwanini wengine wajipige kifua na kuwaambia wengine wewe ondoka tu huko CCM kwa kuwa utauawa?

Mwigulu anasema hawatawaacha wanaoua na wanaoshirikiana na wauaji.

Intelijensia iingie kazini tatizo hilo limalizwe mara moja. Yantuumiza na kutuchafua nchi yetu mauaji hayo
 
Serikali iache siasa. Ina kila vyombo ya kuweza kujua ni nani wanafanya hayo. Iwatafute na iwashughulikie.
 
Siasa inaingia Sasa kila kitu kitavurugika ,tukisema hawa jamaa wametuzidi akili sijui nani atabisha
 
Mh. Mwigulu maswali uliyotoa kujaribu kupata majibu ni mazuri, lakini unaposema pana ''ka mchezo kanachezwa na kuwatupia mpira waandishi wa habari wajaribu kupata majibu'' wakati hali inayoendelea mkoani Pwani ni ya hatari kwa usalama wa taifa. Vyombo vya habari na waandishi siyo wataalamu wa usalama na mbinu za medani ya kupambana na uhalifu kama huu wa mauaji yakupangwa. Waandishi wanasubiri Waziri wa usalama na viongozi wa kipolisi na kiserikali kutoa majibu.

Inabidi serikali yenyewe itoe kauli baada ya uchunguzi wake kina wa kiintelejensia ama sivyo serikali wakitoa ruhusa kila kikundi katika jamii kitoe tafsiri yake ni kama kuzidi kuhatarisha usalama wa nchi.

Serikali ndiyo inasubiriwa kutoa kauli isiyo na utata maana ina vyombo vyote vya ulinzi na usalama, fedha za kuendesha uchunguzi wa kina ndani na hata kushirikiana na vyombo vya nchi zingine kupata jibu sahihi na kukomesha mauaji haya.
 
Mwigulu amesema kuna mchezo unachezwa na anapatwa maswali, anasema mwanzo tafsiri ilikuwa ni kuhusu mkaa, lakini mkaa na viongozi wa mkaa na CCM kuna muunganiko gani?

Ikaja tafsiri nyingine ya misimamo mikali ya kidini, misimamo mikali ya kidini wapi na wapi na CCM?

Ikaja tasfiri ya ujambazi, lakini ujambazi na CCM wapi na wapi hadi watafutwe viongozi wa CCM hadi waliostaafu?

Ikaja tafsiri ya ugaidi, lakini ugaidi na CCM chuki itakuwa imetoka wapi? Na huyo anayeonyesha viongozi wa CCM ni nani, anaonyesha viongozi wa CCM waliostaafu na yeye atakuwa ni muuaji pia.

Na kwanini wengine wajipige kifua na kuwaambia wengine wewe ondoka tu huko CCM kwa kuwa utauawa?

Mwigulu anasema hawatawaacha wanaoua na wanaoshirikiana na wauaji.

Angeachia ngazi angeonekana ana akili sana na tungemuheshimu zaidi ila kwa kuzidi Kwake kung'ang'ania Uongozini wakati tayari ameshaonyesha failure ya hali ya juu katika huo Wadhifa wake wenye akili zetu zilizotukuka tunamuona ni wa hovyo hovyo. Binafsi nilishamdharau kitambo tu!
 
Labda kuna mambo ambayo serikali inafanya kwa kushirikiana na viongozi wa ccm ambayo yamezaa chuki; na kwa kuwa ninyi ndiyo watawala na Sheria zinasimamiwa na ninyi basi wenye Chuki watakuwa na bifu na viongozi wa Chama na serikali!! Hawa wengine hawasimamii Sheria yeyote wala hawana nguvu zidi ya wahalifu waziri! Mchango wangu kwa maswali ya waziri!
Wanajuaje? Kweli kiongozi aliyechaguliwa na Watu na yupo mstahili wa mbele katika uongozi wake atashindwa kujulikana waziri! Yaani kiongozi ashindwe kujulikana na Watu na eneo Lina uovu!
 
Angeachia ngazi angeonekana ana akili sana na tungemuheshimu zaidi ila kwa kuzidi Kwake kung'ang'ania Uongozini wakati tayari ameshaonyesha failure ya hali ya juu katika huo Wadhifa wake wenye akili zetu zilizotukuka tunamuona ni wa hovyo hovyo. Binafsi nilishamdharau kitambo tu!

Kinachonikera kila siku ni hawa viongozi wenye dhamana, wenye uwenzo na nguvu zote, wenye intelligensia za kipolisi, kijeshi, kiusalama lakini bado wanakuja kulalamika kwenye media. Sasa watu kama sisi tusiomiliki hata mkuki tufanye nini???

Huyu jamaa ameshakuwa naye kama nyuki wa mashineni tu.

Do something Mwigulu, sio kila siku unalalamika tu wakati huo huo tunapoteza wapendwa wetu huko.
 
Mh waziri,
huu si muda wa kujiuliza,
Mtu wa kwanza anauawa unajiuliza,
wa pili akiuawa unaamua....huu ni muda wa kuact usitueleze kujiuliza kwa sasa,sio wakati wake.
Kama, vijana wetu wazidiwa mbinu amua hata kukodi wenzetu wenye mbinu zaidi ya kwetu. Usituaminishe kuwa haya mauaji yanafanyika kisiasa, utasababisha mauaji kuendelea.
Huu ni wakati wa kuungana mh waziri na si wa kutafuta utengano wa aina yoyote.
 
Back
Top Bottom