Mwigulu ataka TAMISEMI 'wakate safari na Chai' kujenga madarasa

Mwigulu ataka TAMISEMI 'wakate safari na Chai' kujenga madarasa

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa maagizo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kwamba ifikapo mwisho wa Februari 2026 awe amefikisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Imani iliyopo Mkata Magharibi, kutokana na hali mbaya ya madarasa matatu ambayo hayatumiki kwa sasa.

"Muandikie kabisa Katibu Mkuu, mwisho wa mwezi hiyo fedha iwe imefika, na mkurugenzi anasikia na mkuu wa mkoa. Fedha itatoka wapi wakate safari, wakate chai, kila mtu anywe chai nyumbani kwake, fedha hiyo ije tutengeneze kizazi cha kesho hapa."

Amesema hayo Februari 13, 2026, katika ziara yake mkoani Tanga alipokuwa akiweka jiwe la msingi na kukagua kituo cha kupoza umeme Mkata, ambapo awali Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkata Magharibi, Mussa Ngana, aliibua hoja ya uchakavu wa madarasa ya shule hiyo.

Ngana amesema shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 1,000 na ina madarasa manne yanayotumika, huku mengine matatu hayatumiki, na mhandisi akikataza matumizi yake pamoja na nyumba ya mwalimu kutokana na uchakavu.

Akijibu kuhusu jambo hilo, Waziri wa Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe, amesema amewaelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni Vijijini na Katibu Mkuu wa wizara yake kila mmoja kupeleka Tsh. 50 milioni katika shule hiyo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mengine mapya.

"Shule hii ipo Mkata Magharibi, miaka miwili iliyopita tuliteta pesa ambayo imemalizia ujenzi wa shule mpya ya Julius Nyerere yenye madarasa 14, na tayari kuna wanafunzi wanasoma pale ambao ni 670," amesema Profesa Shemdoe.

 
Maigizo,chai wataendelea kunywa na posho za safari watajiripa.
 
Kwa nini yeye Mwigulu asiuze maviete yake??
 
yeye wenyewe mbona hajakata mabasi yake yale aliyoyakana? kiongozi mwizi watumishi wezi wananchi fukara yaani balaa tupu.
 
si uonevu huo yaani mtu safari za kikazi aache kwenda kisa madarasa kweli?si kuna hela kibao tu za misaada wanaweza chota wakajenga madarasa,kwani hela za uviko ziliishaga
 
Anafikiri kuiga falsafa za JPM kutamfanya wananchi wamkubali..
 
Kujenga madarasa hadi serikali kuu iingilie kati??
Hii nchi bado tuna safari ndefu
 
Back
Top Bottom