MWIGULU alishindwa nini kuokoa bill.325 ?

MWIGULU alishindwa nini kuokoa bill.325 ?

Sikumsikia MWIZI na MUONGO walipokuwa wanamsulubisha Kafulila na Mnyika , leo mnaleta masifa kibao.Wote wezi tu hakuna cha Tembo Mkubwa wala Tembo mdogo wote wakunyongwa tu.
Wote ni wa moja. Ila najigomboa kiaina. Ila wote ni wezi na hela ni zao .kwani dili hiyo sio ya kwanza wameshapiga nyingi
 
Mwigulu wakati wa wizi huo hakuwa Naibu waziri.Ndio kwanza alikuwa kada mtiifu akiisurubisha CHADEMA

Ni kweli nilimshuhudia alivyoisurubu CHADEMA kule Arusha kwa kumuua Mwenyekiti wa CDM pale Usariver na kulipua bomu pale Soweto ikiwa nipamoja na kubumba kesi za UGAIDI kwa lwakatare na akina Kileo bila kusahau na kumuua yule kijana wa CDM kule Igunga pamoja na kumwagia tindikali kijana Musa tesha wa kule Igunga ili amtumie kuiangamiza CDM.
 
Mwigulu Nchemba ni tapeli la kisiasa ana shameless opportunist. Escrow ilikuwa mezani kwake tangu aingie Wizarani lakini hakusema chochote. Na hata wakati Kafulila anaaza kupiga kelele bungeni Mwigulu hakufungua domo lake. Sasa anaona issue imepamba moto, bila aibu anaanza kudandia hoja ili aonekane naye anapinga wizi. Upuuzi mtupu.

Hili nalo neno.....!!
 
Wote wanafiki hao maneno mengi tu kama anataka akamate mali za wafanyakazi wa TRA waliojimbilikia mali kwa pesa chafu na kwa njia sisizo halali, atakamata zaidi ya nusu ya wafanyakazi wake, atangaze zawadi tu kwa wananchi kuna watu watatokea kama mvua kuwataja na kuwaonyesha mali zao mbona wanawajua.
 
Kama ni kweli Mwigulu kafanya hayo, nampa hongera sana. Vita hii inapaswa kupiganwa ndani na nje ya CCM. Nje wako wengine wanoaipinga CCM. Ndani kumejaa mafisADI, Waoga, wanaojipendekeza (bootlickers) na outright thieves like the former AG. Kujitokeza kwa Mwigulu mwenye msimamo huo ni vema kwa CCM.

At least kuna kiongozi mwenye kujali umma wa Watanzania. Kidogo leo ntapata usingizi.

Mwigulu keep it up. History will absolve you.
 
Wote ni wa moja. Ila najigomboa kiaina. Ila wote ni wezi na hela ni zao .kwani dili hiyo sio ya kwanza wameshapiga nyingi

Zimepigwa hizo kwa ajili ya UCHAGUZI mwakani ndiyo maana alikaa kimya kwa wakati ule,ili atupumbaze ndiyo yuko busy kutudanganya.
 
Kama ni kweli Mwigulu kafanya hayo, nampa hongera sana. Vita hii inapaswa kupiganwa ndani na nje ya CCM. Nje wako wengine wanoaipinga CCM. Ndani kumejaa mafisADI, Waoga, wanaojipendekeza (bootlickers) na outright thieves like the former AG. Kujitokeza kwa Mwigulu mwenye msimamo huo ni vema kwa CCM.

At least kuna kiongozi mwenye kujali umma wa Watanzania. Kidogo leo ntapata usingizi.

Mwigulu keep it up. History will absolve you.
Hahaha ! Huyu mwigulu alikuwa anaujua mchezo mwanzo mwisho sasa hivi kimenuka anajifanya anataka kujisafisha.
Huyu ni mwizi tu na mnafiki pia
 
Ya kweli haya au hadithi za pwagu na pwaguzi!? Na lini atafuatilia mabilioni ya Uswiss $529 million ili yarudishwe nchini na wezi kufunguliwa mashtaka na kufisiliwa kwa wale ambao waliendelea kuchota pesa hizo kule Switzerland?




BREAKING NEWZZ KUTOKA DODOMA,MWIGULU AAMUA KUPIGANIA HAKI YA MASIKINI NA WANYONGE KWENYE SAKATA LA IPTL/ESCROW. AAMUA KUTANGAZA MISAMO WAKE WAZI WAZI MBELE YA MAWAZIRI WOTE,SOMA HAPA CHINI.

Dondoo Kutoka Kikao cha Ndani ya Baraza la Mawaziri kilichofanyika jana Dodoma kilichofanyika
Ofisi za TAMISEMI. Kikao rasmi cha kujadili sakata la IPTL/ESCROW namna wahusika watakavyowajibishwa au kuokolewa.

1.Misimamo ya Mawaziri tofauti tofauti. Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu waziri wa Fedha anatajwa kuwa Waziri wa kwanza kuonesha msimamo wake wazi wazi kuwa Sakata la IPTL/ ESCROW ni hujuma dhidi ya Uchumi wa Nchi.acharuka,AAGIZA MALI ZOTE NA PESA ZOTE ZILIZOLIWA, ZILIZOTAWANYWA ZIKAMATWE.Naibu huyu ambaye mara kadhaa amekuwa akitajwa na vyombo vya habari kwa juhudi zake za kuokoa matumizi mabaya ya fedha na hata Watanzania wengine kuamua kumbatiza jina la Sokoine wa pili ikiwa ni kufuata nyayo za aliyewahi kuwa Kiongozi Makini Nchini hayati Moringe Sokoine. Mwigulu ndani ya kikao hicho cha siri anatajwa kuendeleza ujasiri wake kuhusu mambo yenye masilahi ya Taifa. Wakati watu na tetesi mbalimbali zilikuwa zinaongelea kujiuzulu, Mwigulu amejitokeza kwenyw kikao hicho na kusema CAG ameshamaliza utata, sasa mali zote, fedha zote za IPTL zikamatwe na wahusika wote wakamatwe. Nanukuu kama nilivyosikia"Tumezoea kusema eti tumewajibisha watu kwa wao kujiuzuru, "Kujiuzuru ni kupewa Likizo ya kwenda kula fedha ulizo ziiba"anasema Mwigulu, Hili ni jambo la mazoea, sasa, CAG ameshasema pesa zile zilikuwa mali ya umma, sasa zikamatwe zote, na wahusika wote wakamatwe" Mwigulu alienda mbali zaidi na kusema hata ambao walishastaafu na wamehusika kulihujumu taifa wakamatwe na akaunt zao zikamatwe, zifilisiwe zirudishwe kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Naibu huyo anayeshughulikia mambo ya sera, Mwigulu ameagiza mtumishi wa TRA aliyepewa 1.6bilion afukuzwe kazi, akamatwe, na akaunti ifilisiwe fedha irudi serikalini. Pia mitambo ya IPTL ikamatwe irudishwe serikalini. Utamaduni wa watu kujiuzulu na kuhesebu kuwa ni adhabu ni jambo la zamani, sasa ili kukomesha wizi, uzembe na ufisadi sasa tuwakamate wahusika wote, tuwafilisi na tuwaweke ndani na tuwafunge. Habari za uhakika kutoka kikao cha baraza la Mawaziri zinasema, jana Mwigulu Nchemba aliongea kwa sauti ya mamlaka mbele ya Waziri mkuu nakusema kujiuzuru sio adhabu stahiki kwa wizi Mkubwa kama huu wa Mali ya Umma,Hisia hizo zikiwa zimegubikwa na maisha yake halisi ya umasikini aliyokulia na huku akihusisha Wizi wa fedha na hujuma dhidi ya Watanzania Masikini.Mbunge huyo wa iramba anasisitiza kwa kusema " Tazama wanafunzi, watoto wa masikini zaidi ya elfu 40 wamekosa mikopo, madawa hospitalini hakuna masikini wanakufa, watu wasio na hatia wanafungwa kwa kukosa michango ya maabara, walimu wanadai, wazabuni wanauziwa nyumba zao na mabenki huku wakiidai serikali kwa huduma walizotoa, leo wezi tuwape adhabu ya kujiuzuru? Tuwape likizo ya kwenda kutumia fedha walizo waibia masikini? Hapana, "Enough is enough" ndg Waziri mkuu tuwakamate, tuwafilisi, tuwafunge. Pesa na mali virudi serikalini."

Kwa yule mtumishi wa TRA aliyekula fedha za IPTL zaidi ya 1.6 B,Mwigulu akatoa agizo kuwa "Nimemwagiza kamishna wa kodi amfukuze kazi yule wa TRA iliyoko chini ya wizara yangu, na afilisiwe, pia mitambo na kodi vikamatwe, na wahusika wakamatwe. Hatuwezi kuendeleza mazoea ya kufunga masikini na kuwapa likizo wezi wakatumie fedha. Walio serikalini na walioko kwenye siasa wakamatwe na tuwafilisi fedha irudi serikalini."

Taarifa za uchunguzi zunasema tayari TRA imechukua hatua." Naibu Waziri KILIMO Mh.Godfrey Zambi wanusurika Kukunjana na Werema(Mwanasheria Mkuu wa Serikali). Wakati kikao kikiwa kimepanda joto la juu,Mawaziri wakifikia makubaliano kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na madini Maswi na Mawaziri waliohusika ni lazima waachie ngazi,Ndipo Werema alipotaka kumkunja Mh.Zambi baada ya kutoleana maneno machafu dhidi ya mali ya uma. Madai yanakwenda mbali kuwa,Zambi alikuwa anapigia kelele kuwa inawezekanaje Mwanasheria mkuu kubariki wizi wa Fedha za Umma?.Ni wapi watu wa msoma wakasifika kwa wizi wa mali za Umma?.Chokochoko hizo ndio zilipelekea Ugomvi kati ya Zambi na Werema.

Mbali na Mawaziri hao,Mh.Tibaijuka amekuwa Mwizi wakwanza wa IPTL kukubali kuwajibika katika sakata hili mbele ya kikao cha baraza la Mawaziri. Ni wakati Muafaka sasa kwa Watanzania wote kuunga kupaza sauti kama akina Zitto walivyofanya,Kuunga mkono zaidi Machozi ya akina Mwigulu waliojitolea kutetea Masikini wakati huo huo wanahujumiwa na Mawaziri wenzao ndani ya Chama tawala,Mwigulu ameanua kujilipua Mzima mzima bila kujali yeye ni nani ndani ya Chama kwa Malengo kuwa CCM haipo tayari kukumbati waovu na wezi. UPDATEs zitawajia Kesho baada ya kikao cha leo Usiku kingine.
 
Aliyewaambia Mwigulu yupo serious na kazi ni nani? yule ni tamaa ya madaraka tu ndo inamsumbua. hajamaliza hata miaka mitano ya ubunge anataka u rais is he serious?
 
Nini cha maana alichokifanya Mwigulu hadi atuaminishe ya kuwa anafaa kuwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania? jimboni kwake tu hapendeki ashukuru uzembe wa CDM kumtimua Kitila Mkumbo otherwise asingepita.
Mwigulu hafai waulizeni waliosoma UDSM anatabia ya kupenda madaraka na kujipendekeza kwa wakubwa.
 
Alisha okoa zipi? Hizo porojo zake anatafuta huruma ya maskini baada ya kuuwa raia wasio na hatia, anawezaje kuwa muuaji achukie wizi? Gamba ni gamba tu hata ukilitia mafuta litabaki kuwa gamba.
 
Katika Gazeti la Mwananchi la leo Jumapili
23.11.2014
Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba
katika maoni yake kama kiongozi wa Nchi na
mmoja wa Vijana shupavu Nchini wasio na
chembe ya Kashfa yoyote katika Nchi hii kama
historia yake inavyojieleza kuwa ni Mtoto wa 10
katika Familia ya Mzee Madelu,Mtoto pekee
aliyesoma katika Familia hiyo,akiwa na historia
ya kujisomesha kwa kuchunga Ng'ombe hadi
anamaliza kidato cha sita na Baadae UDSM
kwa Mkopo wa Serikali,Naa baadae Masters
aliyoisoma akiwa anafyatua tofali kama kibarua
pale Tegeta Maji.Na sasa akiwa Mwanafunzi
wa PHD na Msomi wa Uchumi Daraja la kwanza
anasema.
"HAOTOSHI,HAITOSHI,HAITOSH I Mafisadi wa
ESCROW/IPTL kujiuzulu nyadhifa zao kwani ni
sawa na kuwapa Likizo wakatumie fedha za
Watanzania,Fedha zilizopaswa kuelekezwa
kwenye Miradi ya Maendeleo
(Shule,Hospitalin.k).
Mafisadi wa ESCROW ni wahujumu Uchumi wa
Nchi,Wanatakiwa
Wakamatwe,Wafilisiwe,wafungwe" .
Kesi kama hii haiihitaji kwenda Mahakamani
kwasababu CAG ameshatoa ripoti inayotia
hatiani wahusika.
Chanzo.Mwananchi la leo Jumapili
 
Back
Top Bottom