Mwigulu aliposema Tanzania hakuna wizi wa mali za umma mbele ya Rais Wabunge wote walikaa kimya; leo ndio wamejua kuna ripoti ya CAG?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,105
Sakata la ripoti ya CAG lilishafungwa na Waziri wa Fedha. Asingeweza kutamka mbele ya Mhe. Rais kwamba hakuna wizi kama hizo taarifa siyo ya baraza la mawaziri. Wabunge wanapoona hakuna waziri bungeni wasishangae, kwa sababu hata mawaziri wakiwemo bungeni hakuna majibu wala jambo jipya watakipata kwa wabunge. Mawaziri wamejiridhisha kwamba hakuna wizi full stop.

Itoshe kusema wapo watu wanataka kumchokoza Rais. Wapo watu wanataka waonekane nao walisema kisa wameona uchaguzi mkuu unakaribia. Wapo wabunge wanataka kuonekana wapo smart kisa tu wamepewa nafasi ya kuzungumza ila ukweli hakuna mbunge anayeweza kusema ana uchungu na hii nchi.

Wewe uingie bungeni kwa wizi uje useme una uchungu na nchi, unaanzaje? Mwenyekiti wa kamati aingie bungeni kwa figisu then awe na uchungu na wananchi thubutu.

Bulaya anasema mzee Sirro ahojiwe anajua kazi Sirro aliyofanya hadi kumfanya awepo bungeni leo? Do she know how much this people suffered for them to be in parliament. Unapotaka kupigania haki lazima nafsi yako iwe ya haki. Kama umeona kura kwanini utake kutuaminisha kwamba wewe siyo mwizi wa fedha za umma?

Hakuna mbunge wakuwaambia wananchi yeye ni mwema, wote ni wezi isipokuwa mnazidiana kiwango na kwa kuliona ilo ndipo Mwigulu akaamua kuhitimisha hii hoja kwa kusema adharani Tanzania katika awamu ya sita hakuna wizi

Kama unaona wizi basi wewe ndiye mwizi mwenyewe..
 
Mkiendelea kupiga kelele tutamwambia Mwigulu acheleweshe posho tuone mtaishije
 
Wabunge uwanja wao kusema chochote ni bungeni.....wana kinga nje Bunge tena mvelevRais hana kinga kabisa....ataonekana kudharau mhimili huo...
 
Wabunge uwanja wao kusema chochote ni bungeni.....wana kinga nje Bunge tena mvelevRais hana kinga kabisa....ataonekana kudharau mhimili huo...
Kukemea wizi kunahitaji kinga ya bunge au kila mtu amepewa nafasi ya kukemea? Kwa hiyo tukitaka kukemea uovu tusubiri tuingie bungeni?

Hawa wamekosa nguvu ya kukemea rushwa toka walipoingia bungeni kwa rushwa........wakitaka wajiuzulu wakagombee upya warudi kwa sanduku la kura

Toka wameingia bungeni kinyume cha sheria wamelipwa kiasi gani cha fedha za umma kisichokuwa halali yao?
 
Kukemea wizi kunahitaji kinga ya bunge au kila mtu amepewa nafasi ya kukemea? Kwa hiyo tukitaka kukemea uovu tusubiri tuingie bungeni...
Rais hana nia dhati kupambana na wala rushwa na wezi.....period
 
Mambo ya kuvimbiwa
MTN.jpeg
 
Back
Top Bottom