Mwenzi asiyeelewa!

Amanda187

Member
Mar 19, 2012
7
0
Habari za Ijumaa,Naomba niwaulize wenzangu,ivi unafanyaje unapokuwa na mwenza wako ambaye haelewi,yaani ulimwengu uko huku na yeye yuko huku?halafu hashauriki kwa maana anajiona yuko sahihi,hana mipango dhabiti,anapanga kutokana na wenzake wanavyopanga,anaweza akaamka kitandani bila mpango wowote akaenda kununua gari ambalo halikuwepo kwenye mipango na huku nyumba kapanga.....Nauliza ili kujifunza namna ya kumsaidia huyu na kujisaidia mimi mwenyewe.Karibuni.
 
Habari za Ijumaa,Naomba niwaulize wenzangu,ivi unafanyaje unapokuwa na mwenza wako ambaye haelewi,yaani ulimwengu uko huku na yeye yuko huku?halafu hashauriki kwa maana anajiona yuko sahihi,hana mipango dhabiti,anapanga kutokana na wenzake wanavyopanga,anaweza akaamka kitandani bila mpango wowote akaenda kununua gari ambalo halikuwepo kwenye mipango na huku nyumba kapanga.....Nauliza ili kujifunza namna ya kumsaidia huyu na kujisaidia mimi mwenyewe.Karibuni.

Jambo zuri ni kumshauri, lakini kama hashauriki, basi inapaswa kuangalia namna ambavyo wewe huwa unamshauri. Inawezakana wakati wa kumshauri hutumia jazba na ukali, au humuonyesha dharau na kutomheshimu. Mazingira kama haya, hata umshauri vipi hawezi kukuelewa. Inapaswa kuchagua wakati wa kushauriana mkiwa wote na furaha na amani huku ukionyesha hali ya unyenyekevu na heshima, naamini atalainika na kukubali ushauri. Kumbuka ushauri hauhitaki nguvu! Unaweza jaribu kumkumbusha/kumuomba akupe mipangilio ya mambo anayopanga kuyafanya kwa mwaka huu, mjadiliane ili anapofanya kitu isitokee kwako kuwa suprise isiyo na tija.


Pia jenga mazingira ya wewe kuomba ushauri toka kwake kwa kila unalofanya ili umjenge kisaikolijia ajue kuwa kukaa wawili ni kushirikishana, kusaidiana na kushauriana. Ukishindwa kabisa, Jaribu kukaa na watu unaowaamini sana (ndugu au marafiki zake) wale wenye nia njema ambao wako karibu sana na mumeo uwaombe waweze kumsadia huyo mwenzi wako kimawazo.
 
if you cant fight 'em JOIN THEM.....natumai umenielewa. kama huwezi kum-convince atumie mipango yako ya maendeleo HUNA BUDI kutumia mipango yake ya maendeleo. kwa mfano mie na mwenzangu tulishakubaliana kutofautiana ila kuheshimiana wakati wa utekelezaji wa yale machache tunayoamini kuwa ni msingi mkuu wa maendeleo yetu..

huwa tunafanya hivi...mwaka huu mama analeta mipangomiji yake ya maendeleo then inakuwa implemented ingawa mie nakuwa sifurahii ila sina budi kutii..next year inakuwa zamu yangu kuweka mipangomiji..hapo lazma anitake..kama plan ni kupiga gambe kila siku kurudi home saa 9 lazma atoe ushirikiano hata kama hapendii..so ningewashauri muwe mnapeana nafasi ya kutekeleza matamanio yenu kila mmoja kwa nafasi yake na utashi wake except..ushirikiano uwepooo.
 
umejicontradict! Mwanzo umesema anafanya anavyojisikia, baadaye ukasema anafanya wafanyavyo wengine!

Sema hasikii ushauri wako wewe! Lkn pia kununua gari si lazima uwe umejenga; na utajenga kila mkoa? Kupanga hakiepukiki!

Jaribu kumuelewa, na si kila unachokiona wewe ni sahihi!
 
umejicontradict! Mwanzo umesema anafanya anavyojisikia, baadaye ukasema anafanya wafanyavyo wengine!

Sema hasikii ushauri wako wewe! Lkn pia kununua gari si lazima uwe umejenga; na utajenga kila mkoa? Kupanga hakiepukiki!

Jaribu kumuelewa, na si kila unachokiona wewe ni sahihi!
Ukweli mtupu, sio kila uonacho wewe sawa, na wenzako lazima wakione sawa...nice point :cool2:
 
Kichwa kimeruka!!
Kuna watu wa ushauri, unaweza enda waona mkiwa pamoja!
 
Unapomshauri mtu USITEGEMEE AFANYE VILE ULIVYOMSHAURI

Na huyu mtu unasema hashauriki lakini tambua Ushauri ni TAALUMA, watu wanasomea

Unayo hiyo Taaluma ???????????

Kama La Tafuta kwanza taaluma ndipo ufanye huo ushauri

UNAWEZA KUWA WEWE NDIO SABABU YA HUYO NDUGU KUFANYA HAYO ANAYOYAFANYA
 
weee hapo ni kusepa tuu maana huyo atabadilika pale atakapo amuwa kubadilika mwenyewe
 
UNAWEZA KUWA WEWE NDIO SABABU YA HUYO NDUGU KUFANYA HAYO ANAYOYAFANYA ......


Mimi kuwa sababu sidhani kwani ukweli ni kuwa tunakaa na kupanga mipango kamili ya mwaka,lakini anaibuka na tendo wala sio mpango au wazo bali kitu kilichokamilika na kukitenda bila kukileta kwa ajili ya mjadala au ili kiwekwe kwenye mpango......Na anaponifahamisha ni kama taarifa iliyokamilika na sio wazo au mpango.Karibuni tuzidi kupeana mwanga.
 
]Ukweli mtupu, sio kila uonacho wewe sawa, na wenzako lazima wakione sawa...nice point :cool2:........

Ni kweli sio kila nionacho mimi ni sahihi.....Lakini issue hapa sio nani yupo sahihi na nani hayupo sahihi,bali swala ni kupeana taarifa pale wazo la tofauti linapojitokeza ili liwekwe mezani lijadiliwe muafaka ufikiwe sio kuibuka na kitu kilichokamilika.Sidhani kama hapo nataka usawa wa kufikiri au maafikiano.Tusaidiane mawazo kupata mwangaza wandugu.
 
unajua hata mtoto ukimwelekeza kwa mdomo tu kila siku hawezi kuona tabu kurudia kosa maana anajua mama atanielekeza kwa mdomo yataisha, sometimes you need to take serious decision labda ataanza kugutuka na kushaurika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom