Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,076
- 144,511
Nimewahi sema humu mara nyingi sana kuwa Mungu hayuko upande wa CCM na hii ni kutokana na matendo ya baadhi ya viongozi wa chama hiki kwa miaka mingi yaliyopelekea mateso na dhiki kwa watu wasio na hatia na hivyo Mungu amewachoka na sasa kaamua kuwanyima maarifa ili utawala wa chama chao ufike mwisho.
Niliwahi sema pia,CCM wasifikiri wanapambana na wapinzani,bali wajue wanajaribu kupambana na nguvu za Mungu kupitia upinzani na ndio maana licha ya mabavu yote ya dola yanayotumika dhidi ya upinzani,wanaoharibikiwa na kuporomoka kisiasa kila siku ni CCM na kamwe si wapinzani.
Ndugu zangu, hata kwa tukio la leo huko katika msiba wa Mzee Mengi,binafsi naona ni muendelezo tu wa kuporomoka kwa CCM na inawezekana kabisa Mwenyezi Mungu ana makusudio yake katika tukio hili la leo ingawa sisi binadamu tunaweza tusilione hili na hata tukiliona,bado tunaweza tusiliewe ni kwanini limetokea na kwanini tukio hili linaweza lisiwe la mwisho
Naomba niseme tu hata hivi viburi na majivuno ya watawala na wateule wa watawala hawa, huenda pia ni mpango wa Mungu ili kupita viburi hivi,utawala wao ufike mwisho na kumbukeni hata Baba Akofu alionya kuwa Mungu atawashusha wenye viburi na labda lugha sahihi ingawa ilikuwa si rahisi kuitamka moja kwa moja pale madhabahuni ilipaswa kuwa ataishusha CCM.
Jambo moja tunalosahau wanadamu ni kuwa,katika huu ulimwengu uliodumu kwa mamilioni ya miaka,hakuna jambo jipya linalotokea leo hii bali yote yanajirudia tu na kilicho kipya katika dunia ya leo labda ni teknolojia tu na maboresha yake na hakuna kingine.
Hata wanasayansi wanagundua tu vitu vya kiasili ambavyo kiuhalisia vilikuwepo ila huko nyuma havikuwa kugundulika hivyo hata katika sayansi hakuna jipya(kuna ugunduzi mpya tu ila wa vitu visivyo vipya) bali kipya leo hii ni teknolojia tu na maboresho yake kama nilivyosema hapo mwanzoni.
Tukiridi na kuangalia baadhi ya tawala mbalimbali katika ulimwengu wa leo,ni wazi pia hakuna linalofanywa na watawala wa leo ambalo halikuwa kufanywa na baadhi ya watawala walioshi katika miaka ya nyuma au katika karne zilizopita na ambalo baadae lilipelekea anguko lao kama ilivyokuwa wakati ule wa mitume na manabii(enzi za kina Farao,n.k) na pia katika miaka ya hivi karibunui(kama ilivyokuwa kwa kina Idd Amini,Maliyamungu,Mobutu na wengineo wengi).
Vile vile hakuna ishara au dalili mpya ya anguko la watawala au chama chchote cha siasa ambaloo halikuwa kuonekana katika miaka ya nyuma au katika karne zilizopita, hivyo hata haya tunayayashuhudia leo hii(viburi,kejeli,dharau,kufukuru,n.k) ni mundelezo tu wa ya yale yaliyofanywa na kina Farao katika karne zilizopita na wakina Gaddafi na wengine wengi katika miaka ya nyuma lakini wote tunajua nini ilikuwa hatima yao.
Hata katika dunia ya leo,ukiaka kuonekana Nabii au mtu mwenye uwezo wa kuona mbali,tafsiri yanayotokea leo hii kwa kuyalinganisha na yanayofafana nayo katika historia au kwa kuyarudia maandikio matakatifu yanasema nini na hakika kila siku utaonekana kama mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuona mbali kumbe ukweli ni kwamba katika dunia ya leo hakuna jipya bali yote ni marudio tu na mengine yameelezwa katika vitabu vitakatifu.
Hivyo, kwa hawa wa leo kama wanafikiri kwao itakuwa ni tofauti,basi wajue tu wanajidanganya ila dalili zote zinaonyesha mwisho wao na wa vyama vyao kukaa madarakani umewadia na kwamba Mungu ndio muhusika mkuu katika hili na ndio maana kawanyima maarifa ili waanguke na hakika wataanguka tu.
Mzee huyu na kiongozi wa CCM ameshasoma alama za nyakati na kuanza kukiri kuwa kuna dalili ya anguko la CCM japo si kwa maneno ya moja kwa moja.