General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,303
- 23,055
Ewe Mwenyekiti wangu wa chama Chetu pendwa CCM Dk John Magufuli tunaomba kwa kulinda heshima yetu ya serikali na chama tunaomba umfukuze Uanachama wa Chama Cha Mapinduzi Mbunge wa jimbo la Mtama Ndugu Nape Mnauye.
Tunashuhudia kijana huyu akikukosea heshima wewe, serikali na chama chetu.
Nape sio mtu wa kwanza kuondolewa kwenye Baraza la Mawaziri.
Walisha ondolewa Mawaziri wengi ambao mimi nimeshuhudia nikiijua siasa kipindi cha JK lakini sijawahi shuhudia Waziri aliye enguliwa kuendelea kuiandama serikali.
Juzi Kitwanga ulimtumbua lakini kwa heshima ya serikali na Chama Kitwanga alikaa kimya, na hakuzungumza chochote.
Tumeshuhudia Wakuu wa Mikoa wakiondolewa lkn hakuna hata mmoja aliye lalamika na kupiga makelele.
Kwa sasa Nidhamu yaa Nape ktk serikali yako na hata Chama imepungua, ni wazi kwamba huyu ni Mwanachama asiye mtiifu, asiye weza tunza siri za Chama na hata serikali.
Kwa heshima ya chama Chetu na hasa sisi wanachama ambao hatupendezwi na mambo anayofanya Nape tunaomba umvue uanachama.
Nakuomba Mwenyekiti wangu uwe jasiri katika hili, usiogope!!
Kukaa na nyoka ndani ipo siku atakuuma!!
Asante!!