Mwenyekiti wangu Magufuli, usitubu!

Mwenyekiti wangu Magufuli, usitubu!

Askofu Zakary Kakobe mpuuze na hoja igeuze. Huna haja wala hoja ya kutubu kwa toba kwakuwa unatoa tiba kwa miiba ya Tanzania. Unatibu bila tabu yaliyokuwa majaribu mujarabu kwa watanzania. Usitubu! "Hakuna asiye Na dhambi maishani ,lakini kuna watu wa aina mbili,wanaojitahidi kutofanya dhambi Na wasiojali kama wanatenda dhambi"

Usijali. Tunakuombea na kukujibia. Tutamjibu kwa mbwembwe kuliko kunyoa kwa wembe hadi Askofu ajione mzembe. Tutampa majibu ya mbali na karibu hadi aulaumu utaratibu uliomsibu. Usitubu!

Jijenge, jitenge na waingize mkenge. Jifagilie, jiandalie na jifurahie. Ni wakati wako chamani na Serikalini. Kataza hata kwa kuliza fujo za hovyo za mikutano na kuhutubia kwa kujielezea. Huna haja ya kutubu!

Kula nanasi kunahitaji nafasi. Unayo nafasi bila kufosi ya kujinafasi bila wasiwasi na kutajwatajwa wewe tu. Hutubia, tumbua, kemea, kamatia, zingatia, puuzia, koromea na kagua. Ni wewe tu, usitubu!

Demokrasia huleta ghasia. Mikutano hubadili mtazamo. Giza husaidia. Giza hulinda na kuunda. Tuache bila mikutano wala mitazamo. Tukusikie na kukufuata wewe tu. Usitubu, usijipe tabu!

Mambo ya expansion joints hayo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (mapumzikoni Nairobi,Kenya)
Kamwambie Babako atubu kwanza kwa kukuzaa!
 
Hivi Leo mmepandikizwa matusi? Sasa Vuta Nikuvute kakukosea nini hapo? Si kamwambia Mr. Haambiliki asitubu maana yeye ni mtakatifu? Aendelee na ubabe tumsikie yeye, ikiwezekana asiruhusu TV kurusha habari ya MTU mwingine ila yeye tu.

kama northkorea
 
Hiyo kazi unayoifanya ni ya kishetani.
Mwenzako anaambiwa atubu wewe unamzuia.
 
Hovyoo! Mapenzi mazito kuliko hata Janeth mpaka unaonyesha ubwege mkubwa. Au wewe ni yule aliyetunukiwa nyumba za serikali wakati ule?
Unaongelea wakati ule wa waziri mkuu Sumaye?
 
Uliyeambiwa na Mch KAKOBE kutubu, chagua moja ; Kutubu ama kutubu. Endapo utajifanya kutofata ushauri tutashuhudia ndoto ya Mh Lema ikitimia soon.
 
Mnatapatapa sana aisee!

Mbaya zaidi huyo jamaa mnaemsema kawapiga pin kila kona na hamna la kumfanya.... [emoji6]

Uchungu!
 
Nafikiri wachangiaji wengi hawajamuelewa mmtoa mada anamaanisha nini
Ametumia mafumbo sana na unahitaji kufumbua ubongo sana ndiyo utaelewa nini kimeongelewa.
Hii pia inanikumbusha mstari mmoja katika mada moja humu JF kwamba vijana wengi wa sasa wana kumbukumbu nyingi lakini pia wana ndoto chache sana na hiyo kutosumbua ubongo kutafakari kabla ya kujibu ama kuchangia hoja.
 
"Fasihi" fani adhimu sana [emoji16][emoji16] si kama hisabati ya moja jumlisha moja,inapendeza zaidi pale hadhira inaposhindana na fanani wake [emoji16][emoji16] tamu sana
 
Boss VUTA-NKUVUTE Nimekusoma Mwisho Mwanzo na sio Mwanzo Mwisho. Nimekusoma kwa Opposite yake. Hata Sala ya Bwana nayo ni Kutubu, Maana inasema utusamehe makosa yetu ... !!! Hakuna Binadamu mkamilifu, Kutubu huondoa makosa. Hivi tunaendaga Kanisani au Misikitini kufanya nini??? !!!

Askofu Zakary Kakobe mpuuze na hoja igeuze. Huna haja wala hoja ya kutubu kwa toba kwakuwa unatoa tiba kwa miiba ya Tanzania. Unatibu bila tabu yaliyokuwa majaribu mujarabu kwa watanzania. Usitubu!

Usijali. Tunakuombea na kukujibia. Tutamjibu kwa mbwembwe kuliko kunyoa kwa wembe hadi Askofu ajione mzembe. Tutampa majibu ya mbali na karibu hadi aulaumu utaratibu uliomsibu. Usitubu!

Jijenge, jitenge na waingize mkenge. Jifagilie, jiandalie na jifurahie. Ni wakati wako chamani na Serikalini. Kataza hata kwa kuliza fujo za hovyo za mikutano na kuhutubia kwa kujielezea. Huna haja ya kutubu!

Kula nanasi kunahitaji nafasi. Unayo nafasi bila kufosi ya kujinafasi bila wasiwasi na kutajwatajwa wewe tu. Hutubia, tumbua, kemea, kamatia, zingatia, puuzia, koromea na kagua. Ni wewe tu, usitubu!

Demokrasia huleta ghasia. Mikutano hubadili mtazamo. Giza husaidia. Giza hulinda na kuunda. Tuache bila mikutano wala mitazamo. Tukusikie na kukufuata wewe tu. Usitubu, usijipe tabu!

Mambo ya expansion joints hayo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (mapumzikoni Nairobi,Kenya)
 
Ni kwanini asitubu, mbona yeye mwenyewe hua anajitanabaisha kama mkristo safi na anataka aombewe yeye tu! Sasa sala zetu zitamfikia vp kama yeye ni jeuri na hataki kutubu, au hajui kibuli kikizidi ni machukizo kwa alie Mkuu na anaweza asifike 2020.

Hakuna aliemsafi, afanye kutubu tu na baraka zimfikie.

Nb: inashauriwa ukiwakosea watu hadharani basi ukatubu hadharani, kimya kimya ni sawa na kufanya kazi bure.

Kuna haja ya kutubu.
 
Kwa kutuma watu wasiojulikana ili wamuue Lisu pia anatakiwa akatubu maana hats Mungu aliweza muokoa Lisu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom