Mwenyekiti wangu CCM Jakaya Kikwete: Lowassa's buck stops with you!

Amebwagwa rasmi, ametumia pesa muda wote lakni zimeshindwa kumsafisha, aliweka mayai yote kwenye kikapu kimoja, sasa chali kama mende.

Maskini EL, sasa JK kaweka wazi unajipendeeza na vita ya Malawi??? Kama ulivova uPM vua hata huo unyekiti wa ulinzi na mambo ya nje vua, kimenuka. Unajitafutia umaarufu kwa Malawi???

Unatoa rushwa makanisani na miskitini, vijanawa boda boda

Nawasilisha
 
CCM inamtihani mgumu kuliko unavyo weza kufikiri.Kumuacha agombee wana wasiwasi na siri zao.Kumtema anaweza kukimalizia chama chote
 
Leo nilikuwa Mbeya,tena karibu kabisa na Mwenyekiti katika sherehe za kuzaliwa kwa chama chetu. Kinatarajia kutimiza miaka 37 hapo ifikapo tarehe 5/2/2014. Nimejionea jinsi CCM yetu 'inavyojitahidi' kukonga nyoyo za watanzania. CCM leo imepokea wanachama wapya kibao:kama 20 hivi!

Nimejionea jinsi watu tuliokwenda Mbeya tulivyopendezesha sherehe zetu.Nimeshuhudia jinsi watumishi wa Serikali jijini Mbeya walivyokaidi agizo za dola la kuhudhuria matembezi na baadaye mkutano. Nimeshuhudia mengi kama wenzangu wengine walivyojionea kwenye luninga.

Pia nimesikia hotuba.Tena hotuba ya Mwenykiti J.M.Kikwete.Hotuba ilikuwa nzuri.Lakini kuna sehemu siiamini.Haiingii akilini kabisa.Labda wenzangu. Kwamba eti (Lowassa) anapita kugawa rushwa na anaropokaropoka kutafuta sifa. Hasa kuhusu mgogoro na Malawi.Mwenyekiti alitaka kumkemea Lowassa.Mbele ya kadamnasi.Lakini,ngumu kumuamini.

Yeye ndiye rafiki nambari moja wa Lowassa.Yeye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM mwenye usemi wa mwisho kuhusu nidhamu za chama na Serikali. Yeye ndiye aliyeita kujiuzulu kwa Lowassa kwa kashfa ya Richmond kuwa ni 'ajali ya kisiasa'. Leo anakemea;anaonya;anatahadharisha mtu huyo huyo. Anayefanya na kusema yale yale kila kukicha. Mimi siamini.

Kimantiki, ni ngumu kuamini alichosema Mwenyekiti. Mwenyekiti hupenda 'kutoonekana mbaya'. Nadhani leo amefanya upande mmoja hadharani.Upande mwingine ataufanyia wapi? Nasema,mimi siiamini kauli ya Mwenyekiti juu ya Lowassa.

Mzee Tupatupa wa Dar es Salaam
 
50thebe Mkuu Lowassa asingeweza kufanya fujo zote hizo anazofanya bila kuwa na confidence ya utawala.
Zaidi ya hapo mungu unayemsema wewe na Lowassayupo kwa kila mtu, na mbaya zaidi licha ya michango mingi maknisani, mhe. Lowassa a tuhuma za kupora viwanja vya kanisa KKKT Mbezi Beach.

Kwa hiyo sina uhakika kama Lowassa unayemuongelea na ka-mungu kake ka tamaa ya mali ndiko anakokatumainia.
 
Last edited by a moderator:
Kama kweli ccm ipo makini ni wamfukuze uwanachama mamvi,vinginevyo bado kitakuwa chama kisichokuwa na maamzi na kulindana kwa maslahi ya kuwanyonya watanzania.
 
Maamuzi ya ccm siyo kama chadema kwamba mbowe na mtei wakiamua mtu afukuzwe lazima afukuzwe ccm ni vikao hutoa majibu yote.

Nani aliamua kufukuzwa kwa Abdu Jumbe? Kama we ni mtoto, nyamaza tunaoweza kusoma ya nyuma tuseme. CCM haina tofauti na TLP, CDM, CUF, DP, n.k.

Toa sifa inapostahili.
 
Vuta nikuvute,
tumia kichwa kufikiri. Wp kikwete alimtaja lowassa? Kwa hiyo lowassa anagawa rushwa? Thibitisha maswali haya, vinginevyo wana jf wenye akili timamu tukupuuze halafu mods wakupige ban kwa uzushi, uongo na uzandiki
cc.
invisible
fang
melo
 
Anayesema jk amemsema lowasa, anakubali kuwa lowasa anatoa rushwa
 
lini mswahili akaaminika na asiye mswahili?mswahili kwa kiapo na imani haruhusiwei mtosa mswahili mwenzie..ndio maana diri an akuuaza sembe sembe kudhalilisha nchi walimzika ka nguli wa siasa na shujaa..
 
Wafuasi wa Sitta sisiem vpi? Kwani chama chenu kinamzuia m2 kuendesha harambee ktk shughuli anuai za maendeleo ya jamii? Acheni kuweweseka Lowasa hajavunja katiba ya chama chenu cha mizigo na ndo maana anawachora 2 mnapohangaika km mama anaetaka kujifungua. Tunatamani EL apite ili 2we na kaz rahisi next yr.
 
Back
Top Bottom