Mwenyekiti wangu CCM Jakaya Kikwete: Lowassa's buck stops with you!

hivi kosa la lowasa mpaka hapo ni nini, unajua siwaelewi?

kusaidia msikitini/kanisani ni kosa? mbona hamumkamati basi, mpelekeni mahakamani kwa kutoa rushwa..ya nini mnahangaika wakati mahakama zipo, si mumpeleke?

naona lowasa anawanyima usingizi na mnajua kuwa jamaa anapendwa ndio maana..huyu jamaa hamumuwezi bora mtafute utaratibu mwingine
 
Wanajamvi

Lowasa keshasema ameanza safari ya ndoto zake, na akasisitiza kuwa kwa nguvu za mungu atashinda. Hapa tunaona maudhui ya kauli ya Lowasa yamo kwenye hii theoretical concept ya 'safari', maana sio ajabu tafsiri ya 'safari' kwa Lowasa ni kubwa zaidi ya wengi tunavyofikiri, pengine ndio sababu Lowasa yupo kimya kabisa, hasemi lolote kuhusiana na wanaomrushia mawe, kumponda, kumnanga na kumdhihaki. Tunachoona ni kuibuka kwa conceptual institutions ambazo zipo zinazompinga kwa sauti kuu, na zipo zinazomuunga mkono bila kuuma maneno.

Hata hivyo taasisi ya CCM ni kama inaelekea kuelemewa na conceptual concept ya 'safari' toka kwa Lowasa, commentators nikiwamo mimi nasubiri kuona namna Lowasa, mwanasiasa nguli aliyelelewa kwenye misingi ya CCM atakavyofanikisha safari yake kwa nguvu za mungu hasahasa kwenye mazingira ambayo waliomlea, kumkuza na kumkubalisha kwa Watanzania wameanza kumkana kuwa hastahili kuwa miongoni mwao.

Tusubiri tuone

cc Masopakyindi
Mkuu E Lowassa ni nguli kwa kulelewa ndani ya CCM kwa misingi ipi haswa, wakati muasisi wa CCM alishasema hafai.
Na hii ni kutokana na kutumia uongozi wa umma kujitajirisha haraka haraka!!
 
Back
Top Bottom