kilagalila
JF-Expert Member
- Nov 8, 2018
- 320
- 154
Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana Uvccm taifa Kheri james amepiga marufuku vijana kote nchini kukaa bila kufanya kazi ili kuondokana na umaskini unaotokana na uzembe
Mwenyekiti huyo amepiga marufuku hiyo mkoani Njombe alipokuwa akizungumza na vijana pamoja na wanachama wa chama cha mapinduzi CCM mjini Njombe katika ukumbi wa Turbo akitokea katika kata ya Makowo iliyopo katika halmashauri ya mji huo alikokuwa akikagua miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa na ilani ya chama hicho.
James amesema kuwa anapata tabu anapoona vijana wanakaa bila kazi wakati wana nguvu za kufanya kazi na kuwaacha wazee vijijini wakihanagaika bila usadidizi.
“mwenye nguvu za kupasua mbao akapasue,mwenye uwezo wa kulima aklime na mwenye uwezo wa kufanya biashara akafanye biashara ni marufuku kijana kukaa tu, ukiona kijana wako amekaa tu ujue amejiandalia aibu mbele ya safari heshima ya kijana ni kazi, maisha mazuri utayapataje bila kazi tunataka vijana mkafanye kazi”alisema mwenyekiti
Aidha mwenyekiti huyo amesema kuwa halmashauri zote nchini kupitia ilani ya chama cha mapinduzi zimelekezwa kutenga asilimia nne ya makusanyo ya ndani ili kuwawezesha vijana waliotayari kufanya kazi.
“ilani ya chama imeelekeza halmashauri zote nchini kutenga asilimia nne za fedha ya makusanyo ya ndani ili kuwawezesha vijana ambao tayari wameamua kufanya kazi na sisi tupo tayari kuwawezesha vijana waliotayari, na ukikopa pesa utailejesha ile ile bila riba ukikopa kumi unaludisha kumi Raisi wetu amesema lengo la fedha hizo ni kuwawezesha wanyonge bila riba”alisema Kher james
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amesema kuwa halmashauri zimeelekezwa kutenga maeneo maalumu ya kilimo na kwa ajili ya biashara kwa vijana ili kuondoa sababu kwa vijana za kuto kufanya kazi.
Mara baada ya kuzungumza na vijana pamoja na wanachama mwenyekiti amewakabidhi kadi vijana na wanachama wapya zaidi ya mia moja ambao wamejiunga na chama hicho.
mr.mtaani/mc.amiri