Mwenyekiti wa Halmashauri Igunga atiwa mbaroni kwa agizo la Waziri Mkuu

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,091
1,922
Igunga, TABORA.

Jeshi la polisi wilayani Igunga limemtia mbaroni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Ndugu Peter Onesmo, kwa amriwa ya Waziri Mkuu Mh. Kasimu Majaliwa, wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Tabora.

Onesmo na wenzake wanatuhumiwa kwa makosa ya ubadhirifu wa Fedha za mashine ya kukobolea Mpunga zaidi ya milioni 30 na upotevu wa Fedha za mrabaha zilizokusanywa kutokana na makinikia karibia Shilingi Milioni 141 mali ya kijiji cha Bulangamilwa.

Agizo hilo la Waziri Mkuu lilitokana na kilio cha wananchi kupitia Mbunge wa Jimbo la Manonga Mh. Seif Khamis Gulamali.

Akielezea kero za Wananchi wa Jimbo hilo, Mh. Gulamali, alimweleza Waziri Mkuu kuwa pamoja na upotevu huo wa fedha bado Mtendaji wa Kijiji alihamishwa toka kijijini cha Bulangamilwa na kupandishwa kuwa Mtendaji wa Kata ya Igurubi.

Aidha, Polisi wanamshikilia aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji Bulagamilwa, Ndugu Ntemi James, kwa kuwa ndiye anatajwa kama mtuhumiwa wa kwanza katika sekeseke hilo la upotevu wa Mabilioni ya kijiji hicho.

Watuhumiwa wote wanatarajiwa kupandishwa kizimbani pindi upelelezi utakapokamilika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanyaga twende,, hakuna jiwe litakalo baki juu ya jiwe,,
Hapa Kazi Tu.
 
Back
Top Bottom