Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi ajiuzulu. Adai Kamati Kuu ya CHADEMA imefanya maamuzi ya kijuha!

Ni kweli kuwa pamoja na mambo mengine Baraza kuu la Chama iliridhia pendekezo lililetwa kwake na Kamati Kuu kuhusu jambo hili.Na katika utekelezaji wake Kamati Kuu ya juzi iliridhia kuwa, uteuzi wa Wakurugenzi watano ambao ni:-
1. Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika (Mb).
3. Mkurugenzi wa Fedha na uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.

Uteuzi huu hauonyeshi sura ya Kitaifa Wakurugenzi wote watano ni Wakristo kanakwamba CHADEMA hakuna Waislamu wenye uwezo wa kushika nafasi hizo.

Lakini pia hauzingatii mgawanyo wa kijamii kwa kuwa kati ya kurugenzi hizo sita wakurugenzi wanne kati yao wanatokea mkoa mmoja wa kilimanjaro

antaja halafu anahitimisha kwa kusema kuwa wakurugenzi wanne wanatokea Mkoa wa Kilimanjaro.......nijuavyo mimi ni kuwa wacKilimanjaro hapo ni Mrema na Komu , sasa sijui waliobatizwa kuwa ni wa Kilimanjaro ni Kigaila na Lwakatare au ni Mnyika .

Hoja ya Udini , hebu tulitazame Secretariat ya CCM Kwa dini zao,
1. Abdulrahman Kinana......Muislamu
2. Vuai Ali Vuai..........Muislamu
3. Mwigulu Nchemba ...........Mkristo
4.Asha Rose Migiro..........Muislamu
5. Zakhia Meghji .........Muislamu
6. Seif Khatibu..........Muislamu
7. Nnape Nnauye .......Muislamu

Hebu atujulishe nini kinaendelea hapo CCM ambako ndio anasema Lindi itaelekea pamoja na Gesi itoke au is itoke...........naomba jibu kutoka kwa CCM na washirika wao....
 
Mbowe na slaa walidhani dunia ya leo yakutumia nguvu wataipata fresh yao watamjua zitto kuwa ni nani.
 
Nina shauri sasa Chama kiwe na vingozi wakubwa kama wenyeviti wa mikoa na Wilaya watu wenye maisha yao .Chitanda ninakujua vyema .Baba yako alikuwa NCCR na wewe mwenyewe lakini mapema baba yako alirudi CCM na sasa ana cheto kikubwa .Leo ndiyo unaona ukanda ? Unasemea JF ? Kwa sasa sasa wewe unatangaza vita ya Udini ?Kwa kuwa Zitto muislam nawe umeamua kutoka kumpa tafu muislam mwenzako ? Kitila dini gani ? Mbona hamsemi ni Mchaga aua mkiristo gani alifanya madudu akaisumbua Chadema na leo anapeta ?Chitanda ungalikuwa real ungalibakia NCCR na nashauri sasa kwa kuwa umeshapata uzoefu anzisheni chama .

Chitanda nafasi zinatolewa kwa uwezo .Na ulikuwa kiongozi mbona hukuyasema haya huko ndani wakati huo ? Zitto kavuliwa hajafukuzwa .Unatokea Lindi tunajua umesha vuta mapema mambo ya gesi nk .Zitto hawezi kuwa na mtandao mkubwa kama mko na asiwape pande . Chitanda sasa leo unalia na udini na ukabila ina maana sisi watu wa kigoma pia hututakaki ? Maana hatutoki ukanda wako japokuwa dini moja .Chadema watu wako kikazi na si udini, ukabila nk ndiyo maana umeweza kushika nafasi nyeti sana huku ukiwa muislam .Ondoka na watu wako toka Chadema uone inavyo pepea .

Mwisho huna hadhi ya kujiita Mwenyekiti wakati umesha jiuzuru .Wewe sasa ni Mtanzania tu si mwana Chadema lla najua mtakuwa mmesha chukua cheni mapema huko CCM.
Swali sasa .Je Zitto akisja jieleza na akaelewana na Chama chake akabaki kuwa Mbunge na Mwanachama nawe huko umesha mwaga mboga utataka nawe ujadiliwe urudi ? Shule yako ndogo inakusumbua lakini pia naelewa kwa nini Lindi kama Kigoma hakuna maendeleo maana watu wote majungu mno na kuwaza mabaya kwa wenzao.Nenda salama sisimizi .
 
Kama Ccm wanadhani haya mambo ya ubaguzi wa kidini yanaweza kumwagwa Chadema na Cuf peke wanajidanganya sana!! Twendeni huko mbele tutajua
 
CDM ina wanachama wengi sana! Moja akiondoka kwa hiari yake sawa tu. Kuna wengi ambao wanarubuniwa ili watangaze kuondoka na hatuna tatizo na hilo. Wakati wa kupepeta, ngano inabaki katika ungo na makapi hupeperushwa na upepo. Hili ni pepeto linalopita CDM. Usiogope ukisikia mtu katangaza kuondoka. Fahamu kuwa kumbe, alikuwa ni kapi!!
 
kila la heri ndugu chitanda , nilishangazwa sana wewe kuwa kiongozi wa cdm ! Maana uliyoyafanya ulikotoka hakuna aliyeyasahau , hata hivyo hoja ulizoainisha ni mbovu hata kuliko ubovu wenyewe , mlikuwa 50 , sijui mpaka sasa wamebaki wangapi ?
 
Jana tuliambiwa kwenye mkutano kuwa kuna wasaliti 45 watakaoshughulikiwa inawezekana kabisa huyo yupo kwenye list

Vipi hoja zake?

Kwanini usijibu hoja zake moja baada ya nyingine?

Meku, naona mnaongezeana posho tu makao makuu!!!
 
Ndugu Chitanda ona usivyo kuwa na akili sasa .Unasema siyo waraka .Lakini waandishi wa Waraka akina Kitila wamesema ni kweli waraka ni wao na hata waonekana ulikuwa Chadema unaongelea ukabila ,udini na posho tu .Hapa panasemaje hapa chini ?

dani ya Katiba ya Chadema toleo la 2006. Katika Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama. Sura ya 10, Ibara ya ix, imeandikwa: "Kiongozi asijihusishe au kushiriki na vikundi vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya Uongozi wa Chama au Wanachama wake."

Na katika Katiba hiyo hiyo Sura ya 7 kuhusu kazi za Kamati Kuu, Ibara ya 7, Ibara ndogo t, imeandikwa: "Kufanya uamuzi juu ya mapendekezo ya kufukuza Mwanachama." Na Ibara ndogo v, imeandikwa: "Kumwachisha ujumbe wa Kamati Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume na Katiba, Kanuni na Maadili au kushindwa kukidhi matakwa ya kuteuliwa kwake."
 
Kila aina ya uchafu uliokuwa umejificha ndani ya chadema utajitokeza wenyewe.

Tunakutakia kilalaheri huko uendako ndugu bwana Chitanda.

Chadema ipo na itakuwepo ikulu 2013 kwa ridhaa ya Watanzania
 
....
...
MAAMUZI MENGINE YA UBORESHAJI WA MAKAO:
Ni kweli kuwa pamoja na mambo mengine Baraza kuu la Chama iliridhia pendekezo lililetwa kwake na Kamati Kuu kuhusu jambo hili.Na katika utekelezaji wake Kamati Kuu ya juzi iliridhia kuwa, uteuzi wa Wakurugenzi watano ambao ni:-
1. Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika (Mb).
3. Mkurugenzi wa Fedha na uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.

Uteuzi huu hauonyeshi sura ya Kitaifa Wakurugenzi wote watano ni Wakristo kanakwamba CHADEMA hakuna Waislamu wenye uwezo wa kushika nafasi hizo.

Lakini pia hauzingatii mgawanyo wa kijamii kwa kuwa kati ya kurugenzi hizo sita wakurugenzi wanne kati yao wanatokea mkoa mmoja wa kilimanjaro
Literally kuna ukweli lakini katika maisha halisi huwa natamani kuona mgonjwa anafikishwa emergency pale Bugando, Muhimbili au kwingineko na kabla ya kuanza kuhudumiwa unamuuliza nesi au dokta kuwa "wewe ni kabila gani", ..."wewe ni dini gani" ili kama sio wa upande wako basi ukatae huduma yake.
Na pia sina uhakika kama mtu akipanda ndege alafu akasikia rubani au kapteni anajitambulisha kwa jina ambalo sio la dini yake anaomba ashushwe.
Maana yangu ya ndani ni kuwa bado Watanzania kama nchi tuna safari ndefu kuelekea ukombozi. Na ndio maana leo tunashuhudia baadhi ya wabunge ambao wametoka kwenye list ya Forbes lakini kumbukumbu hazionyeshi kama waliwahi kuuliza swali Bungeni au kuchangia chochote. Waliingia mle wakiwa na mali za kawaida tu na wamekaa mle kunusa kila mradi na tenda iliyonona na leo wanaongelea US $$$$$2 Billion huku sisi kwa mamilioni tukiendelea kusalitiana usiku na nchana.
Kuhusu kutoka mkoa mmoja yaweza kuwa sawa lakini mbona huwa hatujiulizi ni kwa nini watu wa mkoa tajwa ndio wamiliki wa biashara kubwa kubwa (wazalendo) wakati huo huo shoe shiners katika miji mingi ni wao pia bila kuongelea vyeo!
Inasikitisha sana.

Ndugu Chitanda ona usivyo kuwa na akili sasa .Unasema siyo waraka .Lakini waandishi wa Waraka akina Kitila wamesema ni kweli waraka ni wao na hata waonekana ulikuwa Chadema unaongelea ukabila ,udini na posho tu .Hapa panasemaje hapa chini ?

dani ya Katiba ya Chadema toleo la 2006. Katika Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama. Sura ya 10, Ibara ya ix, imeandikwa: "Kiongozi asijihusishe au kushiriki na vikundi vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya Uongozi wa Chama au Wanachama wake."

Na katika Katiba hiyo hiyo Sura ya 7 kuhusu kazi za Kamati Kuu, Ibara ya 7, Ibara ndogo t, imeandikwa: "Kufanya uamuzi juu ya mapendekezo ya kufukuza Mwanachama." Na Ibara ndogo v, imeandikwa: "Kumwachisha ujumbe wa Kamati Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume na Katiba, Kanuni na Maadili au kushindwa kukidhi matakwa ya kuteuliwa kwake."

Unazungumziaje swala la watu kuongezeana posho maradufu huku wengine wakiambiwa wavumilie na kujitolea?
 
Back
Top Bottom