Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Vijijini akamatwa na polisi kwa tuhuma za kijinai ikiwa ni pamoja na uchochezi

Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Vijijini akamatwa na polisi kwa tuhuma za kijinai ikiwa ni pamoja na uchochezi

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limetangaza kumkamata na kumshikilia Bi. Getruda Japhet Lengesela, Mkazi wa Nsalala- Mbalizi na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Taarifa kwa Vyombo vya habari iliyotolewa leo Ijumaa Januari 23, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Benjamin Kuzaga imesema Mtuhumiwa huyo alikamatwa jana Januari 22, 2026 saa tatu usiku eneo la Nsalala, Mji mdogo wa Mbalizi kwa tuhuma mbalimbali za kijinai ikiwa ni pamoja na uchochezi.

Kulingana na Polisi, upelelezi unakamilishwa na hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yake mara baada ya upelelezi kukamilika.

ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MBEYA KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI.webp
 
Polisi wangeachana na hizo mambo zinachochea hasira na baadae kuleta vurugu sijui wanakwama wapi wao hawawazi kitu zaidi ya kubambikiana kesi tu..
 
Kuwa kiongozi wa CHADEMA tu, hilo tayari ni kosa ambalo polisi watalijengea visababu vya kumtia ndani mtu.!

Kutahitajika marekebisho makubwa ndani ya jeshi hilo baada ya ukombozi wa taifa hili toka mikononi mwa watu waovu wanaoshikilia madaraka kwa kuitegemea mitutu ya bunduki.
 
Back
Top Bottom