Mwenyekiti wa CHADEMA - London aenguliwa wadhifa

Ikiwa ni takribani miezi minne tangu tawi la CHADEMA UK lifunguliwe rasmi na Mr Godbless Lema, kumekuwepo na maendeleo makubwa ya ujenzi wa tawi hili lakini vile vile kumekuwepo na changa moto mbali mbali kutokana na uelewa wa watu ktk dhana nzima ya M4C. M4C ikiwa na maana ya Movement for Change, ni sharti mtu yeyote anayeingia ktk movement hii kwenye ngazi ya uongozi aelewe haya machache ya msingi:
1) Kwanza aone matatizo yanayomgusa yeye na jamii yake
2) Ajue na kutambua fika chimbuko la matatizo haya
3) Awe tayari kuwa kiini cha mabadiliko ya kweli anayoyataka kwa jamii
4) Aweze kutoa ufumbuzi kwa kukemea maovu, kuelimisha na hata yeye binafsi kuelimika
5) Ili afanikiwe ktk kipengele cha (4) ni sharti ajitambue yeye binafsi ya kwamba ni:
i) Lazima awe safi na mwenye sifa za kukemea waovu
ii) Aweke maslahi ya jamii mbele na si yake binafsi
iii) Awe na sifa za uongozi zinazotakiwa, nidhamu ikiwa nambari moja ktk orodha.
iv) Awe na msimamo wa kiitikadi
Kwa hiyo, uongozi wa CHADEMA UK kwa baraka za watetezi wa haki ya kweli (CHADEMA TZ) unawatangazia umma watanzania kokote mlipo kwamba kuanzia leo tarehe 12/12/12, Mr Christopher Lukosi amevuliwa rasmi uongozi na amesitishwa uanachama kutokana na kutokidhi mengi ya yaliyotajwa hapo juu.
Uongozi wa CHADEMA UK unamshukuru sana kwa mchango na ushirikiano wake mkubwa kwa kipindi ambacho matundu ya chujio yalikuwa makubwa. Tutaendelea kumkumbuka na hata kutumia misemo yake yenye maana nzito kwa jamii ya kitanzania, kama vile: -
i) Sisi sote ni ndugu, tatizo ni CCM
ii) Kila kwenye msafara wa mamba na kenge wamo
Uongozi unamwakikishia Mr Christopher Lukosi kwamba mamba wote wa CHADEMA UK kwa kushirikiana na wote wenye kuelewa mageuzi ya kweli, tutaliondoa tatizo ifikapo 2015. Tunamtakia kila la kheli katika maisha na ni imani yetu tutaendelea kuwa ndugu yake baada ya tatizo kutatuliwa !!!!.
“We fail in most of our endeavours because we too often underestimate People’s Power” [M4C UK, 2012]

Sorce: CHADEMA UK BLOG
http://chademauk.blogspot.co.uk/?m=1
 
Jamaa inasemekana tangu alipokuja karibuni nchini akifuatilia tender fulani za serikali, aliporudi Uingereza kachenji ile mbaya. Si yule Lukosi tena aliyekuwa anaona CCM pia ni sehemu ya tatizo la Watanzania.

Inavyoonekana ni kwamba ameahidiwa au ameshapata hizo tender za serikali ya magamba hivyo akapewa sharti hilo la kuasi na kusaliti course. Wenzake wamembaini mapema kabla hajachukua maamuzi aliyopanga kufanya.

Kuna mawasiliano amefanya akitaka iandikwe press realese eti itoke kwenye vyombo vya habari akiipondea CHADEMA na kusifia magamba kwenye vitu ambavyo hata mtu wa darasa la kwanza angehoji uwezo wake. Intelijensi ya CHADEMA nasiki ndiyo imefanikisha kunaswa kwa njama zinazopangwa na Lukosi ili eti a defect kwenda magamba huku akionekana kuleta athari kwa pipoooooooooooooz power. Amenoa. Ndiyo shida ya kupiga kabla ya kulenga.

Kuna mambo hapa yatawekwa yanamhusu huyu bwana kisha waungwana ndiyo mjue, njaa si kwa wasiokuw na pesa tu. Jamaa kafika bei hivyo....

Soma haya maelezo yake hapa chini
 
Nafikiri kuna shida kubwa mahali na pia kama Taifa nahisi tunaelekea pabaya sana hasa hatma ya haya masuala ya mitandaoni na propaganda, kuna jambo silioni vema
 
Tatizo la watanzania walio wengi wanaingia kila mahali kutaka kujaza matumbo yao. Huyu jamaa ni akili ndogo sana. he is seriously emotional guy and usually thinks with his emotions. CHADEMA waliingiwa na shetani gani kumpa uenyekiti sijui, lakini ilikua ni suala la muda tu kujua huyu jamaa ni dhaifu sana.

Nadhani anasemekana ni UWT, na tunajua walivyo na sifa ya kufuata upepo! Chris Lukosi is a Useless character!
 
Habari zilizopatikana hivi punde kutoka kwenye vikao vya CHADEMA kupitia Kurugenzi ya Mambo ya Nje, Mwenyekiti wa CHADEMA tawi la London Bwana. Lukosi, amesimamishwa kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA London kutokana na maswala ya kinidhamu.

Inasemekana Bw. Lukosi alienda nchini Tanzania mwezi Septemba mwaka huu na kukutana na wakuu wa Serikali ambapo aliahidiwa kupewa tenda kubwa ya kuclear mizigo ya Serikali. Kutokana na ahadi hiyo Bw. Lukosi alirudi jijini London na kuanza kuivuruga CHADEMA hali ambayo imesababisha kusimamwishwa kwake kuwa mwenyekiti wa CHADEMA -LONDON.

Stay tuned for more details...

Binafsi namfahamu Lukosi, nimewahi kumuona London, naijua kampuni na biashara yao nafsi yangu inaamini ni kijana mwerevu na muelewa sana, lakini zaidi hata hilo tawi la CHADEMA UK , yeye ndiye kajitoa muhanga likaimarika, namfahamu na jitihada zake katika masuala ya kijamii hasa kwa kusafirisha mizigo ya huko madibira Iringa, narudia kusema kumdhihaki lukosi kwa maneno ya hujuma athari yake kwa CHADEMA itakuwa kubwa sana.

Huyu kijana sio lala njaa Uingereza, narudia tena kuna tatizo mahali na siasa za vyama Tanzania ni za ovyo kuliko.
 
Tatizo hapa kuna mchanganyiko mkubwa sana wa watu wa aina tofauti na huyu jamaa ni tofauti sana na wenzake, jamaa hajaenda shule lakini akili inachemka mara mia ya wenzake, jamaa kaona hakuna mwelekeo kaamua kuruka kabla boti haijazama kawaacha wenzake hawajui hata kupiga makasia.

Tusubiri na tuone watafika wapi manake jamaa alikuwa anatumia fwedha yake kukiendesha chama sasa sijui kama watu wataacha kwenda kulinda tesco wakahutubie mikutano ya M4C. Chadema ni chama cha kikabila na kidini pia , hebu niambieni kuna waisilamu wangapi chadema?

Na kama chadema kina nguvu basi wale madiwani waliopita mngechukua walau nusu sio wanne tu kati ya 30. Hapo nasikia viongozi wengine wa chadema taifa wanatafutwa na polisi UK kwa kesi za kubaka UK, au mnataka tuweke mambo hadharani?
 
Lukosi, kama ulifukuzwa usalama wa taifa kwa tatizo la kimaadili, nadhani unapaswa sasa utafute solution. Una shida ya pupa, hasira, you are full of confusion. Uenyekiti wa chama kama cha chadema ulikuwa mkubwa sana ukilinganisha na kichwa chako.

Wewe ulianza Uenyekiti kwa makeke, kelele nyingi lakini wenzio wanakuangalia tu! Wewe ni timing bomb! I can understand the man, biashara yake ni muhimu kuliko kitu chochote, anaweza saliti binadamu yeyote, jamaa ni kichaaaa!
 
Back
Top Bottom