Mwenyekiti wa CHADEMA Arumeru Magharibi ahamia ACT

Mwenyekiti wa CHADEMA Arumeru Magharibi ahamia ACT

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,892
Kisa adai hakuna demokrasia na uongozi


================

TAMKO LA NDUGU ERNEST E. SHESHE ALYEKUWA MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA ARUMERU MAGHALIBI 26 AGOST 2014.

Ninaitwa Ernest Sheshe. Nilikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA katika Jimbo la Arumeru Magharibi kuanzia mwaka 2009 hadi tarehe 25 Agosti 2014.

1. Niligombea nafasi ya uenyekiti tena katika uchaguzi wa chama unaoendelea. Nilishindwa kwa hila na Ndugu Gibson. Hila zenyewe ni pamoja na Mhe. Godless Lema kuwahonga wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo shilingi 30,000/= kila moja na kisha kuwaficha hadi siku ya uchaguzi. Aidha, wajumbe walipelekewa chakula mafichoni kilichobebwa kwenye gari ya mgombea mwenzangu, yote haya ikiwa ni kinyume na kanuni za uchaguzi ndani ya chama na Waraka Na.6 uliotolewa na Katibu Mkuu. Waraka huu, pamoja na mambo mengine, unapiga marufuku matumizi ya hongo ya aina yeyote katika chaguzi.

2. Siku moja kabla ya uchaguzi, Mhe. Godbless Lema aliwatangazia wanachama kwamba Mwenyekiti wao ni Gibson na ndiye atakayekuwa mgombea ubunge. Wagombea wengine wanaojipitisha ni mamluki na ni wasaliti wa chama na wananchi wa Arumeru.

3. Baada ya kutoridhika na matokeo ya uchaguzi kutokana na matukio ya hapo juu, nilikata rufaa kwa kuandika barua kwenye ngazi ya mkoa kama utaratibu unavyosema. Hata hivyo barua yangu ya rufaa ilipelekwa kwa Katibu wa Kanda Ndugu Amani Golugwa, ambaye ndiye aliyesimamia uchaguzi. Ndugu Golugwa ametamka wazi kwamba hakuna cha rufaa wala nini na kwamba yeye hajishughulishi na wasaliti na kwamba hiyo imetoka!

4. Mambo mengine yanayoendelea ndani ya chama katika Kanda ya Kaskazini ni:

a. Uongozi wa kanda hauko kikatiba na unafanya kazi kwa kuvunja katiba ya CDM

b. Mjumbe wa kamati kuu Godbless Lema ametengeneza chama ndani ya chama. Yeyote asiyekubaliana naye na asiye na hela hana thamani ndani ya chama. Nguvu yote hii ya Lema anaipata kutoka kwa mwenyekiti wa CDM taifa Freeman Mbowe kutokana na kwamba ni kabila lake.

c. Mhe. Godbless Lema ndiye anayepanga nani awe Kiongozi ndani ya chama na ndiye mwenye mamlaka ya kuamua nani atagombea ubunge katika uchaguzi ujao kwa majimbo ya Mkoa wa Arusha.

d. Katibu wa kanda Aman Gulugwa ni tatizo kubwa ndani ya CDM,anapenda kuburuza watu,hafuati katiba wala kanuni za uendeshaji wa chama.

5. Baada ya kutafakari hali ya mambo inavyoendelea ndani ya CDM, na kujiridhisha kwamba chama hiki kimetekwa na viongozi wachache na kuachana kabisa na misingi tuliokuwa tunaijenga, na kutokana na ukandamizaji wa demokrasia unaoendelea, nimeamua rasmi kujiunga na chama kipya kinachoitwa ACT_Tanzania ambacho viongozi wake ni waadilifu na baadhi yao pia wamedhulumiwa haki zao ndani ya CDM. Kunzia tarehe tarehe 26 Agosti 2014 siku ya Jumanne mimi sio mwanachama na kiongozi wa CDM tena. Ninajiunga na wazalendo wa ACT-Tanzania.

6. Pamoja nami, tupo na wazalendo wengine 14 kutoka kata 14 za Jimbo la Arumeru Magharibi. Kuanzia kesho kutwa tutaanza kukisimika chama cha ACT-Tanzania katika kata zote za Arumeru Magharibi na tutashiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa kadri utakavyopangwa.

Ndimi Ernest E. Sheshe,
Mwanachama wa ACT-Tanzania,
Arumeru Magharibi.

 
Lema amewageuza wanachadema arusha mandondocha
 
Ni kugawana mbao tu, watu wamechoka umwinyi na umimi
 
Mbona watu mnaenda kama kuku aliyekatwa kichwa ? Huyo Mwenyekiti anaitwa nani ni wa ngazi gani .......
 
chadema arusha wameanza kujitambua,, Wamechoka kufanywa misukule na lema
 
Kupitia star tv taarifa saa mbili wamemuonyesha jamaa mmoja anaitwa Erenest sheshe kwamba alikuwa m/kiti wa CDM arumeru magharibu na amejuzuru nafasi za uongozi na kujiunga na act.

Cha kushangaza kuna kadi alikuwa ameweka mfukoni kama 7 hivi alipofika mezani akazitoa. ukiziangalia zile kadi ni mpya kabisa. alikuwa anawaonyesha waandishii wa habari na hakusema chochote kuhusu zile kadi na alikuwa mwenyewe na waandishi wa habari. sasa najiuliza yeye mwenyewe ndio amehama lakini ana kadi mpya za kuonyesha waandishi wa habari.

Kitu ambacho hakiingii akilini amesema walikuwa na malalamiko kwa viongozi lakini hajasema tatizo hata moja.

Jaman nilikuwa nasikia kuna wanaume jina leo nimeanza kuamini,yaani mwanaume unampa mwanaume mwenzio akili zako akutunzie. hawa wamekuwa kama nzi hawana utashi.
Mimi nawashauri act waache propaganda. Ukiacha ofisi huondoki na nyaraka ulizokabidhiwa sasa huyu anaondoka na nyaraka za ofisi

ACT mtuambie mna wanachama kutoka ccm wangapi? hizo bilion mlizopewa bora mngewape hata walemavu
 
Sio lema ni sera ya mbowe hiyo maana lema awapiga arusha mbowe anawapiga ndani ya kamati kuu kama alivyompiga shabani mambo wa kigoma
 
Umbea huo hakuna mwenyekiti wa chadema ameamia act huyo huyu sheshe ni kapurwa wa awaida msaka tonge wala si mwenyekiti mwenyekiti ni mh gibson meseyeki sasa mtu kushindwa kwenywe uchaguzi uhamie chama kingine ana uroo wa adaraka huyo boya

Huyo Sheshe alitumwa na Lowassa aje agombee uenyekiti wa chadema, alipopigwa chini baada ya kupata namba ya kiatu karudi nyumbani CCM kupitia wakala wao ACT
 
Chadema inasikitisha, nguzo yao iliyobaki ni UKAWA tu, na siku wakimkorofisha Lipumba basi wamekwisha!
 
Kuna tofauti ya asili ya mtu na anako ishi na Hiyo ni katiba yako unaleta hapa, lowasa nae mbona yupo monduli na wakati siyo kwao? Au katiba ishabadilishwa kuwa kila mtu agombee anakotokea?@laki si pesa
 
Habari za leo naomba nijibu hoja za uongo uliozushwa eti mwenyekiti chadema kuhamia ACT si kweli ni uwongo mwenyekiti wetu wa wilaya Arumeru magharibi mh Gibson ndiye mwenyekiti mteule huyo kapi msaka tonge anaitwa sheshe mamluki ccm b waliopandikiza baada ya kugombania uwenyekiti akapata kura 8 mh Gibson akapata kura 113 akaenda ACT shauri ya kukosa cheo hatuwaitaji watu wa hovyo CHADEMA huyo ni mrohoo wa madaraka msaka tonge

Huyo hana mpya CHADEMA ni kazi kazi mamluki stop chadema hii ndiyo tumaini la watanzania hatuna nafasi ya wasaka tonge humu nampa pole huyu limbukeni wa siasa kuwa chadema ni kazi kazi tu huku mamluki stop alikuwa pandikizi alileta makundi ndani ya chama wananchi wakamchinjia baharini msaliti huyo hivi mwana chadema wa ukweli ukose cheo uhamie chama kingine kinaingia akili wadau jamani huyo mi snich r.i.p sheshe kisiasa umepotea kwenye medali ya kisiasa kalime huna mpya chadema ndiyo tumaini la watanzani act ni kikundi cha wasaliti aluta contunua
 
Taka taka lile na ACT kinatafuta uadui na chadema watu wakigundua kinawahujumu chadema badala ya mambo hayo kufanywa na ccm basi wasishangae siku wakipigwa mawe

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Nimeamini tatizo la ccm ni Chadema na sio umaskini wa watanzania.
 
Chadema inasikitisha, nguzo yao iliyobaki ni UKAWA tu, na siku wakimkorofisha Lipumba basi wamekwisha!
Chuo cha ngapi bibie ........huyo Mwenyekiti ni wa Arusha ipi? Usikurupuke bana , wantia fedheha miye .......
 
Fikiria kwanza unachojadili na utajijibu vizuri mwenyewe@pesa si laki
 
Back
Top Bottom