Mwenyekiti wa CHADEMA alala Mkutanoni

Mwenyekiti wa CHADEMA alala Mkutanoni

Dah,hii kali sana na alivyolala sasa na domo akaliacha kabisa wazi kiasi kwamba hata panya anaweza ingia na kufanya yake na kisha akatoka pasipo na mtaalamu huyu kujua chochote,hali inatisha sana kwa kweli.

Anyway,kusinzia katika sehemu kama hizi huwa ina visababishi vyake;


  • Hotuba iliyopo imelegea na haina msisimko wowote,
  • Matatizo binafsi ya mhanga wa hali hiyo,aidha alikotoka amekumbana na ugomvi binafsi na familia yake,ama kitu alichokuwa akikitarajia kukipata kwa wakati kimekwama,kwa hiyo mtaalamu lazima alale ili kujisahaurisha,
  • Kukumbana na hali isiyo ya kawaida kwa wakati usioutarajia na hivyo kitu/jambo hilo kuwa kama suprise kwako kwani haukutarajia kuwa katika hali kama hiyo;na
  • Kufikiria kitu kimoja kwa wakati mrefu bila kupata muda wa kukisahau,hivyo njia rahisi aliyotuumbia Mungu ni kupata usingizi kwa kipindi fulani ili kurejesha hali ya kawaida.


Nirudi katika hoja yangu ya msingi;kwanza tatizo kwa mleta mada kuwa,taarifa hii hajaifafanua kukidhi kile alichokuwa amewatamanisha wasomaji wake,nikiwemo na mimi kwa kile alichokiandika kuwa,'...viongozi wa chama wamkingia kifua...'na mbaya zaidi katika habari yake hakuonesha uhalisia wa habari ama statement hii,katika uandishi kitu kama hiki ni kibaya sana kwani huifanya habari kushindwa kukata kiu ya wasomaji.

Pili;nikiwa bado nipo kwa mwandishi,pia hajatuonesha chanzo cha habari hii,kwa maana ya kwamba habari hii ameitoa wapi na kwa njia gani. Katika uandishi pia tunashauriwa kuzingatia sana chanzo cha kile unachotaka kukiwasilisha kwa jamii ili kuepusha uzushi,uvumi na uongo. Hii pia huipa habari husika uzito wa kuaminika kwa wasomaji na kupunguza baadhi ya maswali,lakini pia kukutolea hatia kisheria. Vipi kwa mfano mtaalamu huyo anaamua kukufungulia shitaka juu ya ulivyomdharirisha kwa kuweka picha yake mtandaoni;sehemu ambayo unamwanika kwa dunia nzima! Lakini kama umeonesha chanzo cha habari yako,ni kitendo cha kusema tu kuwa fulani,taasisi fulani,chombo fulani alisema katika sehemu fulani,muda fulani,ni nzuri sana.

Niingie kwa upande wa pili wa mheshimiwa aliyelala fofofo kabisa na kusahau majukumu yake,kwanza nianze na kukihoji chama ama uongozi wa juu wa huyu mtaalamu,je kama habari hii ni ya kweli,ni sahihi kwao kufanya kitendo hicho? Maana ukweli ni kwamba unapomkosoa mwenzako hakikisha umejipanga vya kutosha kufunika kasoro zako hasa zinazoshabihiana na unazozikosoa kwa mwenzako. Katika kikao cha bunge la kumi,mtandao wa kijamii aina ya whatsapp ulijikita sana kusambaza picha kadha wa kadha za Mzee Wasira akiwa amelala fofofo kabisa na huku vikao vya majadiliano vikiendelea. Picha hizo ndizo aghalabu zilitumiwa sana na viongozi wa kambi ya upinzani katika kunadi sera zao kuwa,'...wabunge wanakula hela za bure tu na hakuna lolote wanalolifanya ila kusinzia kwenye mjengo tu...' Je,na mtalamu huyo aliyelala hapa pia anakula hela za bure za chama tu?

All in all;sijaona uzalendo wa kweli katika vyama vyetu vya siasa,maana wanaojisema ni wazuri,nao pia kumbe ni mbwa walewale.

 
attachment.php

Uyu je naye ukawa?
watu waanjadili mambo ya msingi kwa taifa yeye analala fofofo, poor maccm HAMNA PHOTOSHOP HAPO
 
Wapi kwenye habari yako panapoonyesha kuwa CHADEMA imemkingia kifua? Ndugu,uwe unaelewa kwanza habari yako kabla ya kuileta hapa. Bure kabisa!

Ndugu yangu Petro,CCM sio watu wa kubishana nao,wao hufuata upepo.Kitu wanachosema leo sio sawa,kesho wanasema ni sawa.
 
Mwenyekiti wa chama na waziri wa nchi wapi na wapi.mmeharibu nchi kwa miaka 54 mnatafuta kick kupitia mwenyekiti
 
WanaJF,

Kwa kipindi kirefu tu CHADEMA walikuwa wanamkebehi mzee Wassira kwa tabia yake ya kulala Bungeni, lakini wakati huo huo CHADEMA inawakingia vifua viongozi wa chama chao wanao kutwa wakiwa wamelala fofofo kwenye mikutano ya chama chao.

Mtazame mwenyewe huyu kiongozi wa ngazi ya juu kabisa CHADEMA, Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa na mjumbe wa baraza kuu taifa, akiwa amelala fofofo mkutanoni wakati hotuba iliyopooza ya Mbowe ikiwa inasomwa!

View attachment 307458

Udaku huu ungefaa Sana kwenye magazeti ya Shigongo au blogu ya Sinta au ya Le Mutuz
 
Hii vijana wa ccm awachukulia kama ajenda leo lumumba utalipwa buku8 badala ya 7 kwa kuandaa huu uwongo
 
sisi vazi letu ni kombati sio suti, ww unapga picha za kwenye kumbi za harusi unatulelea hapa?
 
huyo aliesinzia naona alikua anatakia awe na kiongozi wa korea kaskazini
ni kunyongwa
 
WanaJF,

Kwa kipindi kirefu tu CHADEMA walikuwa wanamkebehi mzee Wassira kwa tabia yake ya kulala Bungeni, lakini wakati huo huo CHADEMA inawakingia vifua viongozi wa chama chao wanao kutwa wakiwa wamelala fofofo kwenye mikutano ya chama chao.

Mtazame mwenyewe huyu kiongozi wa ngazi ya juu kabisa CHADEMA, Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa na mjumbe wa baraza kuu taifa, akiwa amelala fofofo mkutanoni wakati hotuba iliyopooza ya Mbowe ikiwa inasomwa!

attachment.php


Mbona huyo kama amelala kwenye sherehe na siyo kwenye mkutano, sioni kama hayo ni mandhari ya mkutano
 
Back
Top Bottom