The Analyst
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 464
- 246
Naomba niseme sijamuelewa vizuri sana rais wetu mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mh. JK lakini kama haya ndiyo anayomaanisha basi ni vizuri akaanza kuona haya aka aibu. This is not the time. Please JK settle down.
Mara kadhaa amejaribu kumshawishi Rais "awakumbuke vijana waliokipigania CCM kwenye mitandao ya kijamii wakikesha nk nk" Je hii ina maana wateuliwe katika nafasi za juu kwenye serikalini au watafutiwe fedha za kifuta jasho? Kama hii ndiyo maana yako basi tunapaswa kukuombea maana una matatizo makubwa!
Kama nia yako ni kumwambia rais aliyepo madarakani awaone na kuwapa mkono wa pongezi na shukrani hiyo ni kazi yako wewe na wanachama wenzako katika chama lakini si majukumu ya msingi ya urais as an office/institution. Wananchi wa kawaida hata hatupaswi kujua.
Labda nikukumbushe mambo machache Mh. Mwenyekiti.
Mbinu zenu chafu (kupitia mtandao wenye umafia ndani yake) ndiyo chanzo cha Tanzania kukosa kiongozi bora wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005. Tungeweza kuwa na Magufuli wakati ule au hata Salim A. Salim na yeyote mwingine for that matter. Lakini wenye uwezo walikatishwa tamaa na kupitia ujanja ujanja sawa na aliojaribu rafiki yako Edo ukashinda kwa kishindo na wenye kufaa kihalisia wakapotezwa kiaina. Kumbuka gazeti la Rai dhidi ya Magufuli then!
Hukuwa na mpango wowote wa kuisaidia Tanzania kama nchi. Hata ukikataa leo rohoni unajua hukuwa na plan yoyote JK!
Wanamtandao mlitumia mbinu na fedha nyingi kupata madaraka lakini hamkuwa na moja la kuitoa nchi ilipokuwa imefikia. Mwenzio pamoja na machafu yake kapunguza madeni wewe na rafiki zako mkawa mnatumia tu!
Ulitarajia nini? Maisha yaboreke au familia yako ineemeke?
Ulikuja na "Baraza la Marafiki" sikumbuki idadi lakini 60 ilitajwa mara kwa mara. What exactly did you expect? Kuboresha maisha ya wanyonge waliokushabikia wakidhani utasaidia kwa kuwa na utitiri wa mawaziri?
Leo kaingia kiongozi mpenda wanyonge na mzalendo (zaidi yenu wanamtandao wote) unataka kumshawishi afuate nyayo zako mbovu ili kuwafurahisha nyie wachache? Ona aibu bosi! Huu siyo wakati. Nani asiyejua kwamba hakuwa chaguo lako kwanza. Kama Magufuli alikuwa chaguo lako tangu awali "Unpopular Membe" aliingiaje tano bora? Wacha zako hizo!
Magufuli akifuata ushauri wako kwa kuwakumbuka waliokipigania chama kwa njia mbalimbali katika kipindi kigumu hasa wakati rafiki yako kipenzi Edo akitishia hali (kwa tafsiri ya favours na vyeo) basi ni wazi yafuatayo lazima yatokee.
1. Ulaji mpya wa mali ya Umma hasa miongoni mwa wateule favour/shukrani "pigania chama".
2. Kudorora kwa vita dhidi ya rushwa. (Nani asiyejua baadhi ya wakwepa kodi ni wachangiaji katika kampeni zenu katika mtandao).
3. Kufa kwa juhudi za kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya. (Wengine rafiki na familia zenu na mnajua).
4. Kuporomoka kwa mapato ya serikali kufuatia ukusanyaji mbaya wa kodi/ushuru na maduhuli ya serikali.
The list goes on and on!
Naomba nirudie tena "Bw. JK kama ushauri wako ni kumtaka rais apendelee watu waliomsaidia kushinda uchaguzi ni wazi umeishiwa na bora hata ukaona aibu na kung'atuka uwenyekiti mapema tu kuwapisha watu wanaoamini potential ya taifa letu katika kupata maendeleo.
Nakumbuka wewe uliamini tunaweza kuifikia Japan kwa msaada wa Marekani na Ulaya. Hahahaaaa!
Your time is over.
Kama umeondoka madarakani ukiwa unpopular sana ilikuwa choice yako mwenyewe! Huwezi ku-graduate Uchumi ukashindwa kujua dollarlization ya uchumi kwa nchi inayoimport takriban kila kitu kama Tanzania ni kutafuta mfumuko wa bei usio wa lazima!
Asante kwa kusoma!