Mwenyekiti wa ACT ni katibu wa ADC

Mwenyekiti wa ACT ni katibu wa ADC

Mtowa mada hana jipya walewale atujuze kwanza. Dr slaa anakadi ya ssm na cdm je ni kipi anachozumikia?
tatizo limbu anakadi ya CCM,CUF,ATC na ADC.kwa vile huna akili huoni tatizo???
 
Hivi BK7 tayari wamehamia ACT?

Tiba
Hao huwa wanaenda popote ili mradi kuna mshiko wa kufanya waishi mjini. Ingawa ACT lengo lake ni kuwa kaidara kadogo ka usaidizi katika propaganda za CCM. Kwa sasa ruzuku yao iko Lumumba.
 
Lucas Kadawi Limbu amekaimu tu kwa muda wakati suala la MM bado linajadiliwa mahakamani. MM ndiye mwenyekiti wa ACT
 
[h=2]ACT ni mbadala wa CHADEMA[/h]
Wakuu,
Baada ya chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kupoteza uelekeo na kusambaratika, hatimae chama mbadala wa CHADEMA kimepatikana.
Chama hiki makini na mkombozi wa watanzania ni ACT.
ACT ni chama makini sana na viongozi wake ni wasomi hawajakimbia shule wala kupata division zero kwenye mitihani yao,
Sera kuu ya ACT ni maendeleo kwa vijana wote wa tanzania.
ACT ni chama cha watanzania wote hakina ubaguzi wa kidini, kikabila wala kikanda kama vyama vingine
Naomba serikali iboreshe daftari la kudumu la mpiga kura haraka ili vijana wajiunge na chama chao makini wanachokipenda cha ACT.
Naomba kuwakilisha hoja.​

Mkuu ni mbadala wa CCM manake lengo ni kuiondoa CCM madarakani au lengo la ACT ni kupambana na CHADEMA??
 
We muongo kweli huyu limbu alishaondoka adc siku nyingi sana usifanye kama watu hawajui mambo.
Mkuu,alikoondoka siku nyingi ni C.U.F. Adc bado yupo. Km alishaondoka adc hebu tuambie katibu wa sasa wa adc ni nani!?
 
Ndiyo maana tunasema chama pekee cha upinzani Tanzania na kinachoogopeka ni CHADEMA tuuuu!! Wengine wote ni chumia tumbo tuuuu!!! Wekeni details ili Zitto na Kitila wakiwa majukwaa tuwawekee movies!! Magamba wanatumia kodi zetu kufadhili vyama vya kudidimiza CDM huku ndugu zetu walioajiriwa serikalini hata mshahara hawana. OC hawapati wamekaa tu maofisini hakuna kazi wanafanya. Wameshatukopa weeee January hii ada hawawezi kulipa mashuleni. Ukiwauliza serikalini kuna nini hawana majibu ila poa SSM wajue kuwa hata watumishi wa serikali wameshawachoka!!! Subirini 2015.
 
Hao ni matapeli wa kisiasa waanaochukua fedha za mafisadi kujengea vyama uchwala!
 
mbona mnapozungumzia ACT lazima muizungumzie na CDM? Jamani chondechonde ACT bado mkinda kwenye ugomvi wa vyama! Na muwaache walale.
 
DSC04924.JPG


Imefahamika kwamba Mwenyekiti wa Chama kipya cha Alliance for Change and Transparency (ACT) ngazi ya taifa pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha siasa Alliance For Democratic Change (ADC) Lucas Kadawi Limbu!.
Hali hiyo imezidi kuwachanganya wengi ambao wamekuwa wakifuatilia duru za siasa za Tanzania na kuziita "Siasa za maji taka" kutokana na wengi kukaririwa wakisema kwamba kuibuka kwa vyama vingi vidogo vidogo kunakoendelea kila kukicha ambavyo havina impact yoyote kwa Serikali iliyoko madarakani wala wananchi ni kwaajili ya maslahi ya watu wachache wanaothamini matumbo yao.

Zaidi kunaweza kuchukuliwa kwamba ni namna nyingine ya utapeli wa kisiasa kama ambavyo Mwenyekiti wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) Ndg. Lucas Kadawi Limbu alivyoweza kumiliki kadi za vyama viwili (ADC & ACT) kwa wakati mmoja, upande mmoja akiwa ni Mwenyekiti wa chama cha ACT ngazi ya taifa huku kwa upande wa pili akibakia katika nafasi yake ya awali ya Ukatibu
Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC).

Maisha Times ilipojaribu kuhoji kwa undani dhidi ya kitendo cha Ndg. Lucas Kadawi Limbu
kuwa na sura mbili katika vyama viwili tofauti vya siasa wengi walisema kwamba wanamuona kama ni mtu asiye na msimamo na tapeli wa kisiasa na kama ilivyo kwa vyama vingine vya siasa vilivyoingia kwenye ulingo wa siasa za Tanzania kwa fujo na kufa kibudu kama UDP, CCJ, CHAUMA, TLP nk ndivyo itakavyokuwa kwa ACT ambacho kinadaiwa kuundwa na viongozi na wanachama walioasi, kusaliti na kufukuzwa katika vyama vingine vya siasa
nchini!
DSC.11.JPG

Hiki chama hao wanaojitangaza ni viongozi wake ni washika pembe tu mwenye nacho anasubiri muda wake huko aliko ambako anapata mshahara na posho uishe ili ajitokeze. Hawezi kufanya hivyo sasa hivi kwasababu za kiuchumi kwani akitoka atapoteza mshahara, posho namarupurupu kibao
 
Naomba serikali iboreshe daftari la kudumu la mpiga kura haraka ili vijana wajiunge na chama chao makini wanachokipenda cha ACT.
acha umburura wewe,kuna uhusiano gani wa kuboresha daftari la wapiga kura na kujiunga na chama? na mtajamba jamba kwa kushabikia usaliti wakati umeambiwa mtu mmoja anashikilia vyama viwili,hata akil yako haushughulishi au ndo njaa yenyewe.
 
vyama vingine hivi ni sawa na vikoba.
 
Dr, Slaa ana kadi mbili CCM na Chadema mbona huongei hilo

kuwa na kadi sio inshu,hata mimi ninazo 3,ya nccr niliyopewa na mrema enzi hizo na ya cuf niliyokabidhiwa na mapalala na zote nimezitunza kwa kumbukumbu!! inshu ni kuwa kiongozi wa vyama viwili tofauti! kama sio uchumia tumbo ni kitu gani???
Kuna huyu MM naye anaangukia kwenye kundi la wachumia tumbo,wanafiki na watu waliokosa msimamo anang'ang'ania cdm ili kulinda maslahi binafsi na tumbo lake huku akiwa act,huu ni unafiki wa hali ya juu na watu kama hao si watu wa kuamini hata kidogo!!! wapo radhi hata kuuza nchi kwa tamaa zao za mali na umaarufu wa kijinga!!
 
Back
Top Bottom