Mwenyekiti wa ACT ni katibu wa ADC

Mwenyekiti wa ACT ni katibu wa ADC

ZAMBI YANGU

Senior Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
163
Reaction score
44
DSC04924.JPG


Imefahamika kwamba Mwenyekiti wa Chama kipya cha Alliance for Change and Transparency (ACT) ngazi ya taifa pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha siasa Alliance For Democratic Change (ADC) Lucas Kadawi Limbu!.
Hali hiyo imezidi kuwachanganya wengi ambao wamekuwa wakifuatilia duru za siasa za Tanzania na kuziita "Siasa za maji taka" kutokana na wengi kukaririwa wakisema kwamba kuibuka kwa vyama vingi vidogo vidogo kunakoendelea kila kukicha ambavyo havina impact yoyote kwa Serikali iliyoko madarakani wala wananchi ni kwaajili ya maslahi ya watu wachache wanaothamini matumbo yao.

Zaidi kunaweza kuchukuliwa kwamba ni namna nyingine ya utapeli wa kisiasa kama ambavyo Mwenyekiti wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) Ndg. Lucas Kadawi Limbu alivyoweza kumiliki kadi za vyama viwili (ADC & ACT) kwa wakati mmoja, upande mmoja akiwa ni Mwenyekiti wa chama cha ACT ngazi ya taifa huku kwa upande wa pili akibakia katika nafasi yake ya awali ya Ukatibu
Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC).

Maisha Times ilipojaribu kuhoji kwa undani dhidi ya kitendo cha Ndg. Lucas Kadawi Limbu
kuwa na sura mbili katika vyama viwili tofauti vya siasa wengi walisema kwamba wanamuona kama ni mtu asiye na msimamo na tapeli wa kisiasa na kama ilivyo kwa vyama vingine vya siasa vilivyoingia kwenye ulingo wa siasa za Tanzania kwa fujo na kufa kibudu kama UDP, CCJ, CHAUMA, TLP nk ndivyo itakavyokuwa kwa ACT ambacho kinadaiwa kuundwa na viongozi na wanachama walioasi, kusaliti na kufukuzwa katika vyama vingine vya siasa
nchini!
DSC.11.JPG
 
[h=2]ACT ni mbadala wa CHADEMA[/h]
Wakuu,
Baada ya chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kupoteza uelekeo na kusambaratika, hatimae chama mbadala wa CHADEMA kimepatikana.
Chama hiki makini na mkombozi wa watanzania ni ACT.
ACT ni chama makini sana na viongozi wake ni wasomi hawajakimbia shule wala kupata division zero kwenye mitihani yao,
Sera kuu ya ACT ni maendeleo kwa vijana wote wa tanzania.
ACT ni chama cha watanzania wote hakina ubaguzi wa kidini, kikabila wala kikanda kama vyama vingine
Naomba serikali iboreshe daftari la kudumu la mpiga kura haraka ili vijana wajiunge na chama chao makini wanachokipenda cha ACT.
Naomba kuwakilisha hoja.​
 
hata kama angekuwa mwenyekiti wa nini, tuna imani naye. ACT dira ya mabadiliko
 
We muongo kweli huyu limbu alishaondoka adc siku nyingi sana usifanye kama watu hawajui mambo.
 
Mbona Shibuda ni mfuasi na mwanachama halali wa ccm lakini ni mbunge wa CHADEMA?
 
We muongo kweli huyu limbu alishaondoka adc siku nyingi sana usifanye kama watu hawajui mambo.
Mkuu, kuna watu wanajaribu kukipoteza mwelekeo chama hiki. Hakika CHADEMA wamenaswa ile mbaya
 
Siasa za maji taka na wizi wa ruzuku.!
 
Limbu political route:
ccm+Cuf+ADC+ACT then Ccm who knows????
 
Michepuko kwenye siasa za Bongo noma..Kula CCM kulala ACT
 
We muongo kweli huyu limbu alishaondoka adc siku nyingi sana usifanye kama watu hawajui mambo.

Siku nyingi unamaanisha nini? Huwa sibishani na mak*ma kama wewe. Endelea kuandika ujinga wako hapa ntakuja pm nikupe makavu yako ---- ww.
 
Mtowa mada hana jipya walewale atujuze kwanza. Dr slaa anakadi ya ssm na cdm je ni kipi anachozumikia?
 
Back
Top Bottom