GE2025 Mwenyekiti UVCCM Taifa Mohamed Kawaida: Tupeleke watu ambao hatutapata shida kuwanadi, historia ya chama chetu hatuwezi kupata shida kuomba kura

GE2025 Mwenyekiti UVCCM Taifa Mohamed Kawaida: Tupeleke watu ambao hatutapata shida kuwanadi, historia ya chama chetu hatuwezi kupata shida kuomba kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mwenyekiti Wa Jumuiya ya Umoja Wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Ccm Taifa Na Mjumbe Wa Kamati Kuu ya Ccm Taifa Ndg Mohamerd Kawaida Amesema Kuwa Chama cha Mapinduzi Kitaleta Wagombea Ambao wanauzika kwa Wananchi Ili Chama Hicho Kiweze Kushinda Kwa Kishindo Katika Uchaguzi Mkuu Ambao Unatarajia Kufanyika Mwaka Huu

Mwenyekiti Wa Uvccm Taifa Ameyasema Hayo Katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Ccm Mkoa Wa Kagera Kilichofanyika Katika Ukumbi Wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Humo,Kawaida Wakati anazungumza na Wajumbe Wa Halmashauri Kuu ya Ccm Mkoa Amesema Kuwa Chama cha Mapinduzi Kitaleta wagombea ambao wanauzika kwa Wananchi Ili waweze Kushinda kwa Kishindo.

“Katika Chama Chetu tunakubaliana,Tunapanga,Tunaratibu Mambo Yote Kupitia Vikao kwa Hiyo unapofika Mda Wa Vikao tunaitana kwa Ajili ya Kufanya maamuzi ya Pamoja na tukaondoka na uelewa Wa Pamoja Ili kuleta wagombea Wetu Ambao wanauzika kwa Wananchi”Amesema Kawaida Mwenyekiti Wa Uvccm Taifa





Chanzo: Channel Ten
 
Kuna chama wanafanya mambo yao bila vikao??
 
UCHAGUZI WOTE WA RUSHWA DIWANI,MBUNGE,RAIS UNATEGEMEA NINI HIVYO VIKAO VINASAIDIA NINI
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Ndg. Mohamed Kawaida, amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kitaleta wagombea wanaokubalika na wananchi ili chama hicho kiweze kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa ameyasema hayo katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera kilichofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi mkoani humo. Kawaida, wakati akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa, alisisitiza kuwa chama hicho kitaleta wagombea wanaokubalika na wananchi ili waweze kushinda kwa kishindo.

“Katika chama chetu tunakubaliana, tunapanga, tunaratibu mambo yote kupitia vikao. Hivyo, unapofika muda wa vikao tunaitana kwa ajili ya kufanya maamuzi ya pamoja na kuondoka na uelewa wa pamoja ili kuleta wagombea wetu ambao wanakubalika kwa wananchi,” amesema Kawaida, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa.
 
Angesema tu sio anapindisha huyo wa juu pia ngumu kumnadi
 
Back
Top Bottom