Mwenyekiti UVCCM, Kheri James aomba radhi kwa watu wote waliokerwa na kauli yake

Hizo kauli ndio Huwa zinasababisha upungufu wa wapigakura. Mwisho wa siku watajikuta makamanda na makada tu kwenye foreni ya kura huku wananchi wanawaangalia tu. Bora umeomba radhi.
 
"Nachukua nafasi hii kuwaomba Radhi Watanzania Wenzangu wote walio kerwa na ujumbe huo,na ninawashukuru viongozi wote wa kisiasa na kiraia walio nikosoa na kunikemea kwa maslahi mapana ya Taifa letu,ninawashukuru sana" Kheri James Mwenyekiti UVCCM Taifa

View attachment 822683

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James ametengua kauli yake inayosema ‘CCM ndiyo inayoamua maendeleo yaje au yasije na hakuna mwananchi anayeweza kuchukua hatua yoyote dhidi ya chama hicho’.

Akimnadi mgombea wa udiwani Kata ya Bagara, mkoani Manyara, Nicodemus Tlaghasi James alisema CCM haiwezi kupeleka maendeleo kwenye maeneo yanayoongozwa na upinzani.

James alitoa kauli hiyo wiki iliyopita katika mtaa wa Mpya wilayani Babati akisema CCM haiwezi kupeleka maendeleo kwa wananchi waliochagua viongozi wa upinzani badala ya CCM.

Akizungumza leo Julai 30, 2018 na Mwananchi James amesema amefikia uamuzi huo baada ya kupokea simu za kumkemea na kumuonya juu ya kauli hiyo.

“Anayepokea sentensi hiyo, hawezi kujua mwanzo ulisema nini na mwisho ulisema nini, nimeamua kufanya kitu cha kiungwana kwamba ilimradi kilichopokelewa kwenye jamii ni kibaya, tumeamua kuomba radhi bila kujali mwanzoni na mwisho nilisema nini,” amesema James.

Chanzo: Mwananchi
. Mimi mmojawapo wa alionikera tena sana. Eti hatuna la kuwafanya sisi tulionyimwa maendeleo. Jimbo langu ni la Upinzani ila tuko wanaCCM ambao kura zetu hazikutosha. Why tuteseke kwa umaskini wakati hatuna kosa Bali wengi wape? Hata hivyo tumetambua kwa nini jimbo la Kawe barabara ni mbovu.
 
Huyo Heri awe na hekima next time afikiri kabla ya kutenda, kawa muungwana kaomba Radhi
 
Sura yake tu muda wote ipo kama ya MTU anaekata gogo...
 
Alichokisema huyu jamaa huo ndio msimamo wa ccm, ila tu kilichomshinda ni namna ya kuyschezesha maneno kwa ghiriba.

Kimantiki kabisa hana kosa la lolote, kusema ukweli siyo kosa hata kidogo na alichokisema ndio ukweli wenyewe.
 
. Mimi mmojawapo wa alionikera tena sana. Eti hatuna la kuwafanya sisi tulionyimwa maendeleo. Jimbo langu ni la Upinzani ila tuko wanaCCM ambao kura zetu hazikutosha. Why tuteseke kwa umaskini wakati hatuna kosa Bali wengi wape? Hata hivyo tumetambua kwa nini jimbo la Kawe barabara ni mbovu.
Mbona nchi nzima hali ni mbaya tu bila kujali upinzani 2020 ccm itarudisha majimbo yote kinguvu tuone ka tutapiga maendeleo wanayotaka
 
N
Hii ni hadithi ya Nyani na Jiwe!

Katika pita pita zake baada ya kushiba mema ya nchi hata kuvimbiwa kwa kula kile ambacho hakukilima au kikipanda akaamua apumzike juu ya Jiwe (mwamba) na hata kuujambia!

Kwa kuwa mwamba ulikuwa umepata joto kutokana na shida ya jua kali, uliamua kumuunguza NYANI matako yake na hata kubabuka!

Nyani akaruka kwa kuungua kule, ...akaondoka zake huku akitoa maneno ya kashfa kwa JIWE, ..."pamoja kwamba umeniunguza, nimekujambia"

Kati ya haya nani ni Nyani na Nani ni Jiwe?

Ameshasema, ameshaleta madhara hawezi kuponyesha nafsi zilizoraruliwa kwa kauli yake!...anaenda zake huku akisema "amekemewa kwa kauli yake"
Nyani Ngabu ndiye Nyani.... Jiwe...sijui
 
Nikakumbuka maandiko , Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa naam wapate kupumzika kwa kuwa matendo yao hufuatana nao.

Ndiyo shida anayokutana nayo leo Mkulu mpya wa Kisarawe, yeye anatamani leo matendo yake ya nyuma yafutike na yasikumbukwe tena bila kujali kuwa yalileta athari kiasi gani katika jamii.

Vivyo hivyo radhi anayoomba huyo Kheri ni vyema tu ajue kuwa matamshi aliyotoa hayatafutika katika fikra za watu kirahisi kama anavyofikiri.

Kwa nchi ambazo viongozi ni wastaarabu na wanajua maana ya dhamana ya uongozi, alipaswa kujiuzulu haraka sana.
 
"Nachukua nafasi hii kuwaomba Radhi Watanzania Wenzangu wote walio kerwa na ujumbe huo,na ninawashukuru viongozi wote wa kisiasa na kiraia walio nikosoa na kunikemea kwa maslahi mapana ya Taifa letu,ninawashukuru sana" Kheri James Mwenyekiti UVCCM Taifa

View attachment 822683

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James ametengua kauli yake inayosema ‘CCM ndiyo inayoamua maendeleo yaje au yasije na hakuna mwananchi anayeweza kuchukua hatua yoyote dhidi ya chama hicho’.

Akimnadi mgombea wa udiwani Kata ya Bagara, mkoani Manyara, Nicodemus Tlaghasi James alisema CCM haiwezi kupeleka maendeleo kwenye maeneo yanayoongozwa na upinzani.

James alitoa kauli hiyo wiki iliyopita katika mtaa wa Mpya wilayani Babati akisema CCM haiwezi kupeleka maendeleo kwa wananchi waliochagua viongozi wa upinzani badala ya CCM.

Akizungumza leo Julai 30, 2018 na Mwananchi James amesema amefikia uamuzi huo baada ya kupokea simu za kumkemea na kumuonya juu ya kauli hiyo.

“Anayepokea sentensi hiyo, hawezi kujua mwanzo ulisema nini na mwisho ulisema nini, nimeamua kufanya kitu cha kiungwana kwamba ilimradi kilichopokelewa kwenye jamii ni kibaya, tumeamua kuomba radhi bila kujali mwanzoni na mwisho nilisema nini,” amesema James.

Chanzo: Mwananchi

CCM Zig Zag
 
Mbona nchi nzima hali ni mbaya tu bila kujali upinzani 2020 ccm itarudisha majimbo yote kinguvu tuone ka tutapiga maendeleo wanayotaka
Nadhani kila Jimbo kutakuwa na maji 24hrs, hospitals zenye madaktari, dawa na vifaa tiba, shule nzuri kama za private ya Feza, lami hadi vitongoji, Machinga watamiliki Super markets na mama Ntilie 5star hotel. Ajira kwa kila Mhitimu wa Chuo, list ya maendeleo kila Jimbo 2020 yaendelea.
 
Alivyoongea shit kulikuwa na video live iweje wakati wa ku make an apology tunaona maandishi tu ?
 
Back
Top Bottom