Wana haja ya kuandikiwa hints kabla ujatoa hutuba,ndo shida ya kutokuwa na vyuo vya uongozi ujifunze,maana maneno ya kibaguzi utolewa na wasio na DNA za kitanzaniaSisi wenye akili tulijua sio kosa lake ni kosa liloanzia juu toka siku aliyoropoka

Aliyarudia maneno yaliyowahi tamkwa na makonda na mnyeti ingia GoogleKwani alisemaje??
Msajili yuko kimyaaaa na NEC ndiyo wameufyata kabisa wanamgwaya ankali.Huyu alitakiwa ashitakiwe kwa uchochezi na uhaini,cha ajabu wapinzani tu ndio huandamwa na bad enough hata wanasheria binfasi wa nchi hii wamelala tu!!!
True kosa alilofanya ni kuomba radhi ukweli,Mimi binafsi sijakerwa na speech ile,kwangu ilikuwa ukweli,ukweli,ukweli..msema kweli ni mpenzi wa mungu.
Wa kulaumiwa ni machinga ndo aliyetuletea dhahama zote. Msoga aliyaona haya.Ndicho tulichokifanya 2015 mkuu ipo sk tutalia na kusaga meno!
"Nachukua nafasi hii kuwaomba Radhi Watanzania Wenzangu wote walio kerwa na ujumbe huo,na ninawashukuru viongozi wote wa kisiasa na kiraia walio nikosoa na kunikemea kwa maslahi mapana ya Taifa letu,ninawashukuru sana" Kheri James Mwenyekiti UVCCM Taifa
View attachment 822683
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James ametengua kauli yake inayosema ‘CCM ndiyo inayoamua maendeleo yaje au yasije na hakuna mwananchi anayeweza kuchukua hatua yoyote dhidi ya chama hicho’.
Akimnadi mgombea wa udiwani Kata ya Bagara, mkoani Manyara, Nicodemus Tlaghasi James alisema CCM haiwezi kupeleka maendeleo kwenye maeneo yanayoongozwa na upinzani.
James alitoa kauli hiyo wiki iliyopita katika mtaa wa Mpya wilayani Babati akisema CCM haiwezi kupeleka maendeleo kwa wananchi waliochagua viongozi wa upinzani badala ya CCM.
Akizungumza leo Julai 30, 2018 na Mwananchi James amesema amefikia uamuzi huo baada ya kupokea simu za kumkemea na kumuonya juu ya kauli hiyo.
“Anayepokea sentensi hiyo, hawezi kujua mwanzo ulisema nini na mwisho ulisema nini, nimeamua kufanya kitu cha kiungwana kwamba ilimradi kilichopokelewa kwenye jamii ni kibaya, tumeamua kuomba radhi bila kujali mwanzoni na mwisho nilisema nini,” amesema James.
Chanzo: Mwananchi
Wanaigilizia anayoyasema Mkuu wao! Na kiburi cha watanifanya nini, polisi ni wetu na kauli nyingi kama hizoSisi wenye akili tulijua sio kosa lake ni kosa liloanzia juu toka siku aliyoropoka
Pole, Lisu alisema tukimnyamazia Mtakatifu huyu, NCHII ITAANGAMIA KAMA HAIJAANGAMIA TAYARIMfano halisi; Huyu mtoto anazungumza hayo, halafu mtu umelazimishwa kukatwa 15% ya mshahara kulipia Mkopo wa Elimu ya Juu, na asilimia nyingine zaidi ya 15% kodi na kubakiwa na Shs187,000/= una familia, umepanga, hujapanda cheo kwa miaka 7 hujaongezwa ongezeko la mwaka la mshahara tangu 2015, halafu huyu anazungumza kwa kiburi cha wazi kabisa. Mungu atatulipa sisi ambao leo tunasema, 'Heri wapole .....
Hahaaaa umenikumbusha Waitara was ukonga!Nikiona yeyote anayejiita mwanachama wa ccm, namuona ni tahira au mpumbavu wa kiwango cha lami...
Si kuna mtu anataka ndugu zake wote wawe viongozi, haya ndio madhara yake. Lazima watajaa kiburi tu, ila siku si nyingi watajutia tu.
dahHii ni hadithi ya Nyani na Jiwe!
Katika pita pita zake baada ya kushiba mema ya nchi hata kuvimbiwa kwa kula kile ambacho hakukilima au kikipanda akaamua apumzike juu ya Jiwe (mwamba) na hata kuujambia!
Kwa kuwa mwamba ulikuwa umepata joto kutokana na shida ya jua kali, uliamua kumuunguza NYANI matako yake na hata kubabuka!
Nyani akaruka kwa kuungua kule, ...akaondoka zake huku akitoa maneno ya kashfa kwa JIWE, ..."pamoja kwamba umeniunguza, nimekujambia"
Kati ya haya nani ni Nyani na Nani ni Jiwe?
Ameshasema, ameshaleta madhara hawezi kuponyesha nafsi zilizoraruliwa kwa kauli yake!...anaenda zake huku akisema "amekemewa kwa kauli yake"
Si wanaiga, mtoto umleavyo ndio akuavyo. Mbona aliwahasa vijana wamchague mtu atakae kuwa na uwezo wa kuonana nae mara kwa mara!!Mtu kama huyu baadae unamkabidhi uongozi nyeti kwa Taifa hili alafu ukarajia ataamashisha wananchi kuleta umoja/muungano na maendeleo
Only in Tz
Hajaomba radhi kabisa. Huu ni usanii.