Mwenyekiti mpya wa kuivusha CHADEMA

Mwenyekiti mpya wa kuivusha CHADEMA

Never, CCM hawashindi kwasababu wana ukomo wa madaraka, wanashinda kwa sababu nyingine tofauti zinazojulikana kila mahali na kila mtu.

na sababu za mbowe kua mwenyekiti mda mrefu je? ama ni siri? umeshalipa ada yako ya uanachama lakini maana uchumi umependa bosi anataka kupiga bapa
 
Kwa mwenendo huu wa kisiasa ni dhahiri sasa anahitajika kupatikana Mwenyekiti mpya wa kuitoa CHADEMA kutoka sehemu moja kwenda mbele zaidi .

Fikra zilezile na mawazo yaleyale ya Mwenyekiti wa sasa ni wazi zimeshindwa kuleta matokeo .

Ifike wakati sasa tukubaliane na hali halisi kuwa Mh Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo aliweza kufanya aliyoyaweza na ameshachoka kifikra katika kukikwamua chama.

Kwa hali na mwenendo wa kisiasa kwa sasa katika nchi yetu ni wazi anahitajika mtu Aggressive , anayesema jambo na likatekelezeka , anahitajika kiongozi asiyetegemea huruma za watawala , anahitajika kiongozi ambaye ataweza kuweka maslahi ya wananchi mbele na siyo maslahi ya Chama . Kiongozi anayepigania Chama pekee hatufai .

Wananchi wana issues nyingi ambazo viongozi wameziba masikio kana kwamba hawasikii .

Tujikumbushe wakati wa Dkt. Slaa kwa nafasi yake tu ya Katibu mkuu CHADEMA, nguvu na sauti ya kiongozi wa upinzani ilionekana na pengine kutiliwa uzito .

Kwa sasa hatuna tena viongozi . Tumebakiwa na viongozi wanaotegemea huruma za wanasiasa . Kwa mfano suala hili la wabunge 19 wa CHADEMA halikupaswa kufika hapa lilipofika , hawa wangeweza kudhibitiwa mapema asubuhi kabisa , cha kushangaza ati tunasikia Mwenyekiti wao alikuwa akiwaomba na kuwaita kuwabembeleza . Seriously!
Wewe unataka tupelekwe kwenye mbogax2 ndiyo hatua unayotaka usijifiche!
 
Ngoja kwanza makamanda waje wakunyooshe.
Hii post yako nai-print nai-laminate na nai-frem niweke ukutani.

That is Socratic reasoning, thought can't be acknowledged by power-graft-stooges.

Infact the incumbent deserves being a sidekick of a new blood.

The incumbent brain needs someone to backstop it to steer the party further and farther; wherefore and therefore history can be documented positively.
 
Suluhisho pekee la kuikomboa hii nchi ni kuiteketeza CCM kwa njia yoyote ile sio lazima kupitia CHADEMA tu.

Iwe kwa mtutu au kwa amani ila siku CCM inang'ooka ndio siku ya kwanza ya tumaini kwa Tanzania.
Itapoondoka itakuwa tyr imeacha vibaraka, mamluki, vipandikizi na mawakala ndani ya upinzani ambao wataendelea kuwahakikishia bata hata wakiwa nje.
 
Wapinzani wamepitia magumu sana kipindi cha utawala wa giza wa jiwe
Wakati chadema wanajichanganya kuhusu inshu ya kumweka Lowassa kuwa mgombea wao napo mtamlaumu Magufuli? Hiko chama kinahitaji reforms, basi, na hiyo tabia ya chadema nje ya kutafuta mchawi nje wakati wachawi ni wao wenyewe itawacost sana.
 
Suluhisho pekee la kuikomboa hii nchi ni kuiteketeza CCM kwa njia yoyote ile sio lazima kupitia CHADEMA tu.

Iwe kwa mtutu au kwa amani ila siku CCM inang'ooka ndio siku ya kwanza ya tumaini kwa Tanzania.
Ukiachana na siasa chafu , za kishamba na za kipumbavu zinazosimamiwa na viongozi wa ccm, Tanzania ni moja ya nchi Tajiri sana. Kama focus ingewekwa kwenye utumiaji wa rasilimali tulizonazo kwa maendeleo ya taifa letu.
 
Mtoa mada ana hoja na asibagazwe,

Ni wkt Sasa lisu au lema kushika hatamu ya chama, mbowe is so lenient hawezi tena kuongoza kwa siasa zake laini laini
Haikupi shaka kwamba watu kama Lissu na Lema leo hii wako ukimbizini? Wataweza kupambana na mitulinga ya CCM kweli?

Anyway, kama Mbowe anaonekana laini laini, suala kubwa zaidi ni hili: wanachama na wafuasi wa CHADEMA na wananchi kwa ujumla wakoje?; wako tayari kupigania haki zao, demokrasia na utawala bora nchini? Wako tayari kutoa back up ya uhakika kwa uongozi imara wa CHADEMA mara wakihitajika kwa mapambano?
 
Mbowe hana ubaya lakini kila kitu kina muda wake; hapo ndio maana ccm wanawashinda kwani wao wana ukomo wa uongozi wa chama chao ndio maana wanakuwa na mabadiriko mara kwa mara!!
CCM kisiasa , kimfumo na kiuongozi hawana weledi wowote wa kuishinda CHADEMA bali wanamiliki vyombo vya dola, hazina ya taifa na katiba ya kidikteta. Hivi sasa CHADEMA ndio tishio kuu kwa uwepo wa CCM. Lakini wamefanikiwa kuidhibiti kwa miaka zaidi ya 15.

Sasa wanasubiri kwa shauku mabadiliko ya Mwenyekiti yaweke mtu AMA ananunulika kirahisi wamnunue na kuigeuza CHADEMA kuwa ACT W, at best, TLP, at the worst. AU mtu modeli ya firebrand alianzishe, wakamilishe hoja ya chama cha magaidi na kukifutilia mbali. Baada ya hapo hawatajisahau tena kuruhusu usajili wa chama cha “kishari”.

Naendelea kusoma comments za uzi huu kubaini wenye CHADEMA moyoni kweli kweli na walio kibaruani.
 
Nasikia kuna muda anatoa pesa zake mfukoni kukisaidia chama, huyo mwingine ataweza? Mwacheni mbowe akae madarakani at least kwa mika 45, ndio kwanza ana miaka 15.
 
Suala sio kubadilisha sura na jina la kiongozi pekee, ili ku deal vizuri na uozo wa CCM na serikali yake inabidi pawepo na vision kubwa zaidi ya hapo, kwa sasa sioni nyingine zaidi ya sacrifice.
Anzisha chama, ufuate itikadi unayoitaka
 
Wakati chadema wanajichanganya kuhusu inshu ya kumweka Lowassa kuwa mgombea wao napo mtamlaumu Magufuli? Hiko chama kinahitaji reforms, basi, na hiyo tabia ya chadema nje ya kutafuta mchawi nje wakati wachawi ni wao wenyewe itawacost sana.
Mim nimezungumzia kipindi cha utawala wa yule dhalimu mpaka Mungu akaingilia kati.
 
Mim nimezungumzia kipindi cha utawala wa yule dhalimu mpaka Mungu akaingilia kati.
Huyo unayemwita dhalimu hakuvumilia ujinga na upuuzi wa aina yoyote ile. Siasa za Chadema zisingeweza kupenya chini ya utawala wake.
 
Back
Top Bottom