Mwenyekiti mpya wa kuivusha CHADEMA

Mwenyekiti mpya wa kuivusha CHADEMA

Mbowe hana ubaya lakini kila kitu kina muda wake; hapo ndio maana ccm wanawashinda kwani wao wana ukomo wa uongozi wa chama chao ndio maana wanakuwa na mabadiriko mara kwa mara!!
Never, CCM hawashindi kwasababu wana ukomo wa madaraka, wanashinda kwa sababu nyingine tofauti zinazojulikana kila mahali na kila mtu.
 
Kwa mwenendo huu wa kisiasa ni dhahiri sasa anahitajika kupatikana Mwenyekiti mpya wa kuitoa CHADEMA kutoka sehemu moja kwenda mbele zaidi .

Fikra zilezile na mawazo yaleyale ya Mwenyekiti wa sasa ni wazi zimeshindwa kuleta matokeo .

Ifike wakati sasa tukubaliane na hali halisi kuwa Mh Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo aliweza kufanya aliyoyaweza na ameshachoka kifikra katika kukikwamua chama.

Kwa hali na mwenendo wa kisiasa kwa sasa katika nchi yetu ni wazi anahitajika mtu Aggressive , anayesema jambo na likatekelezeka , anahitajika kiongozi asiyetegemea huruma za watawala , anahitajika kiongozi ambaye ataweza kuweka maslahi ya wananchi mbele na siyo maslahi ya Chama . Kiongozi anayepigania Chama pekee hatufai .

Wananchi wana issues nyingi ambazo viongozi wameziba masikio kana kwamba hawasikii .

Tujikumbushe wakati wa Dkt. Slaa kwa nafasi yake tu ya Katibu mkuu CHADEMA, nguvu na sauti ya kiongozi wa upinzani ilionekana na pengine kutiliwa uzito .

Kwa sasa hatuna tena viongozi . Tumebakiwa na viongozi wanaotegemea huruma za wanasiasa . Kwa mfano suala hili la wabunge 19 wa CHADEMA halikupaswa kufika hapa lilipofika , hawa wangeweza kudhibitiwa mapema asubuhi kabisa , cha kushangaza ati tunasikia Mwenyekiti wao alikuwa akiwaomba na kuwaita kuwabembeleza . Seriously!
Wenyewe CHADEMA wameomba uwasaidie kumtafuta mwingine?
 
CCM wanahitaji kashikashi... Kwa mwendo huu wa sasa, hakuna kitu kitatokea. Samia alikwishasema mpaka 2030...
Kwamba hiyo 2030 hakutakuwa na watu wanaohitaji kutumia hayo matobo ya katiba mbovu huko CCM? Hakuna mwana Ccm atakaekuja kuwapa katiba mpya kilaini hivyo maana kila anaeingia ni lazima akute mazingira mazuri ya kuendelea kuidumisha CCM madarakani.
 
Hamna shida kabisa Mkuu, japo hili la kukata pumzi niliona toka baada ya ujio wa Lowassa.
Wewe unafikiria kama mimi, Freeman amekata upepo tangu akubali kumpokea Lowassa.
 
Mbona unakubaliana na mimi? CCM wanahitaji kashikashi. Hawatoa kamwe katiba mpya kwa njia za kushikana mikono na kupiga picha pamoja kwa ajili ya magazeti na TV.
Kwamba hiyo 2030 hakutakuwa na watu wanaohitaji kutumia hayo matobo ya katiba mbovu huko CCM? Hakuna mwana Ccm atakaekuja kuwapa katiba mpya kilaini hivyo maana kila anaeingia ni lazima akute mazingira mazuri ya kuendelea kuidumisha CCM madarakani.
 
Upo sahihi kwa upande mmoja lakini haupo sahihi kwa upande mwingine. Upande ambao upo sahihi ni kwamba chadema inahitaji reforms na mbowe hawezi kuwa kiongozi wa hizo reforms. Upande ambao haupo sahihi ni kudhani kwamba udhaifu wa mbowe ni kuonekana kuwa soft kwa watawala au kwa akina mdee. Nope, udhaifu wa mbowe na udhaifu wa chadema kwa ujumla kwa sasa ni ukosefu wa utawala wa mfumo wa kitaasisi unaovuka utashi wa mtu au watu binafsi. Kama huo utawala ungekuwepo hiyo inshu ya akina mdee isiyotofautiana sana na inshu iliyopelekea Dr. Slaa kujitoa chamani wala isingetokea in the first place.
Wapinzani wamepitia magumu sana kipindi cha utawala wa giza wa jiwe
 
Kwa mwenendo huu wa kisiasa ni dhahiri sasa anahitajika kupatikana Mwenyekiti mpya wa kuitoa CHADEMA kutoka sehemu moja kwenda mbele zaidi .

Fikra zilezile na mawazo yaleyale ya Mwenyekiti wa sasa ni wazi zimeshindwa kuleta matokeo .

Ifike wakati sasa tukubaliane na hali halisi kuwa Mh Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo aliweza kufanya aliyoyaweza na ameshachoka kifikra katika kukikwamua chama.

Kwa hali na mwenendo wa kisiasa kwa sasa katika nchi yetu ni wazi anahitajika mtu Aggressive , anayesema jambo na likatekelezeka , anahitajika kiongozi asiyetegemea huruma za watawala , anahitajika kiongozi ambaye ataweza kuweka maslahi ya wananchi mbele na siyo maslahi ya Chama . Kiongozi anayepigania Chama pekee hatufai .

Wananchi wana issues nyingi ambazo viongozi wameziba masikio kana kwamba hawasikii .

Tujikumbushe wakati wa Dkt. Slaa kwa nafasi yake tu ya Katibu mkuu CHADEMA, nguvu na sauti ya kiongozi wa upinzani ilionekana na pengine kutiliwa uzito .

Kwa sasa hatuna tena viongozi . Tumebakiwa na viongozi wanaotegemea huruma za wanasiasa . Kwa mfano suala hili la wabunge 19 wa CHADEMA halikupaswa kufika hapa lilipofika , hawa wangeweza kudhibitiwa mapema asubuhi kabisa , cha kushangaza ati tunasikia Mwenyekiti wao alikuwa akiwaomba na kuwaita kuwabembeleza . Seriously!
Kwanini ccm mnamwogopa Mbowe kiasi hicho?!
 
Kwa mujibu wa mashabiki wa chadema, Mbowe akiachia uenyekiti chama kitakufa!

Hivyo Mbowe yupo sana tu ilo chadema iendelee kuwepo!

[emoji205][emoji205][emoji205][emoji205]
kwanini usijadili mrema aondoke TLP kwanza? wewe umeshupaa na mbowe tu? kwani yeye tu ndiyo mwenyekiti wa chama cha upinzani?
mlisoma shule gani nyie zilizowafundisha ujinga
 
Mbowe hana ubaya lakini kila kitu kina muda wake; hapo ndio maana ccm wanawashinda kwani wao wana ukomo wa uongozi wa chama chao ndio maana wanakuwa na mabadiriko mara kwa mara!!
Kama kachoka si ndiyo raha ya ccm, sasa tatizo hapo ni nini?
 
Kitendo cha Mbowe kutoka gerezani na kwenda straight kuonana na Rais kabla ya viongozi wenzake wa Chama ni dhahiri anategemea akili zake binafsi kufanya maamuzi yanayohusu Chama . sasa hii One man army kwenye ulingo wa siasa hawezi kukifikisha Chama popote
Ajabu sana hii, yaani wanaolalamika ni ccm
 
Kwa CHADEMA ya sasa chini ya Mbowe haifiki popote ni Ku buy time tu . Pengine aendelee kupambaia tu maslahi ya Chama na siyo Jambo lingine
Kwanini unateseka na chadema wakati wewe ccm?
 
Ndio hivyo mkuu . there is no collective responsibility hata hivyo . Maamuzi mengi anayafanya Mwenyekiti binafsi , mwisho wa siku viongozi waandamizi wanaishia kubariki tu , as I know haiwezekani all that time watu wote wakubaliane na wewe kwa kila kitu , lazima Kuna wakati anawaburuza lakini wanahofia kufunguka ili walinde ugali na nafasi zao
Acha kulialia mtoto wa kiume
 
kwanini usijadili mrema aondoke TLP kwanza? wewe umeshupaa na mbowe tu? kwani yeye tu ndiyo mwenyekiti wa chama cha upinzani?
mlisoma shule gani nyie zilizowafundisha ujinga
Kabisa mkuu, wao kila siku wanadili na chadema huku wanasema kimekufa.
 
Mimi ni CCM na namkubali Mbowe sana tu. Mbowe ni kiongozi haswaa....sisemi kuwa CHADEMA hakuna wengine wa kufaa, but huyu mwamba kaweza haswaa nafasi yake.

CHADEMA isipopata kiongozi mvumilivu itaparanganyika. Uongozi unahitaji hekima, uvumilivu na utulivu wa hali ya juu
 
Mpaka sasa Freeman mbowe ameonesha uwezo mkubwa wa kukiongoza Chadema kwa mitihani aliyopitia wakati wa utawala wa dikteta mwendazake. Tumpe muda ata hande hii issue kwa umakini mkubwa.

duuu 😂😂😂, sio mwenyekiti tu hata huyu kashachoka
 
Back
Top Bottom