Kwa mwenendo huu wa kisiasa ni dhahiri sasa anahitajika kupatikana Mwenyekiti mpya wa kuitoa CHADEMA kutoka sehemu moja kwenda mbele zaidi .
Fikra zilezile na mawazo yaleyale ya Mwenyekiti wa sasa ni wazi zimeshindwa kuleta matokeo .
Ifike wakati sasa tukubaliane na hali halisi kuwa Mh Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo aliweza kufanya aliyoyaweza na ameshachoka kifikra katika kukikwamua chama.
Kwa hali na mwenendo wa kisiasa kwa sasa katika nchi yetu ni wazi anahitajika mtu Aggressive , anayesema jambo na likatekelezeka , anahitajika kiongozi asiyetegemea huruma za watawala , anahitajika kiongozi ambaye ataweza kuweka maslahi ya wananchi mbele na siyo maslahi ya Chama . Kiongozi anayepigania Chama pekee hatufai .
Wananchi wana issues nyingi ambazo viongozi wameziba masikio kana kwamba hawasikii .
Tujikumbushe wakati wa Dkt. Slaa kwa nafasi yake tu ya Katibu mkuu CHADEMA, nguvu na sauti ya kiongozi wa upinzani ilionekana na pengine kutiliwa uzito .
Kwa sasa hatuna tena viongozi . Tumebakiwa na viongozi wanaotegemea huruma za wanasiasa . Kwa mfano suala hili la wabunge 19 wa CHADEMA halikupaswa kufika hapa lilipofika , hawa wangeweza kudhibitiwa mapema asubuhi kabisa , cha kushangaza ati tunasikia Mwenyekiti wao alikuwa akiwaomba na kuwaita kuwabembeleza . Seriously!