Mwenyekiti Mpya wa CHADEMA awe na sifa hizi:

Mwenyekiti Mpya wa CHADEMA awe na sifa hizi:

Indume

Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
81
Reaction score
37
Kumekuwepo na harakati nzuri sana ndani ya CHADEMA za kuhakikisha kuwa chama kinakuwa imara siku hadi siku. Kumekuwepo na viongozi wa kila aina ngazi zote ambao kwa kweli wamefanya kazi nzuri na kuhakikisha kuwa CHADEMA kimekuwa chama tishio kwa CCM.

Ili kuendelea sasa kuimarisha chama ni muda sasa kumpata Mwenyekiti ambaye ataendelea kukiimalisha chama na hatimaye kuwa chama kitakachoshika hatamu za uongozi.

Hili litaweza kutokea kama tukiwa na Mwenyekiti na kiongozi mwenye sifa zifuatazo kwa maandalizi ya uchaguzi wa 2015:

1. Awe na umri wa zaidi ya miaka 40. Lengo ni kupata mtu mwenye uwezo mpana kidogo wa kushawishi vijana na wazee.

2. Awe na elimu angalau ya digrii moja. Kwa jinsi mabadiriko ya kiuchumi na technology yanavyotokea kwa kasi sana, ingekuwa busara kuwa na mtu wa kuweza kuchanganua sera, mikakati na mipango ya kimaendeleo, na hili kwa kweli elimu ndo msingi wa yote.

3. Awe mbunifu wa shughuli na kazi za maendeleo. Asitegemee kuambiwa na kuelekezwa tu, ni vema na yeye aweze kubuni sera, mikakati na mipango mbalimbali ya maendeleo.

4. Awe mwanachama wa CHADEMA kwa takribani miaka 5 mfululizo. Hii ni kuweka imani kuwa angalau atakuwa ana uzoefu na sera za chama, mikakati na mipango ya chama. Uzoefu wa siasa za chama ni mzuri kwa kuendelea kuimarisha chama.

5. Awe na uwezo kifedha - ingawa wakati mwingine ni vigumu kujua uwezo wa kifedha wa mtu lakini uwepo mfumo wa uwazi ambao unaweza kuonyesha umiliki wa mali alizonazo. Hii itasaidia kumpata kiongozi ambaye ana uzoefu wa kuwekeza katika shughuli za uzalishaji, na tukiwa na imani kuwa hatakuwa fisadi na mwenye uchu wa pesa kupitiliza. Na ana uwezo wa kulipa ada na michango mbalimbali ya chama.

7. Awe na uzoefu wa kazi za kujiajili au kuajiliwa katika ngazi ya uongozi na utawala kwa takribani miaka 7. Hapa tunataka kuangalia uzoefu wake katika masuala ya Utawala na Uongozi. Kwa kuwa CHADEMA ni taasisi kubwa tunategemea kumpata mzoefu wa kuendesha na kuongoza hii taasisi kubwa nchini.

Mengine naomba mwendelezo.
 
Chadema is the talk of town hapa jamvini lazima kuwa na thread 100 kila siku kwa rate hiyo inaonyesha ndio chama tawala kwa sasa ndani ya mioyo ya watu wengi, mavoulunteers wakuitangaza chadema wapo wengi, wengi kiasi idadi yao huwezi jua lazima waje kwa namna waijuayo wao yaani ndani ya mioyo yao wanawaza chadema 24/7 kipropaganda,kimasilahi,kiupenzi nakadharika bravo mleta mada panua uwigo wa kutangaza chadema lakini pia uje na katiba yao hapo ukiqoute haya mapendekezo yako yanaangukia kwenye kipengele kipi cha katiba
 
soma katiba ya chama kwanza, pili m/kiti wa chadema ni MBOWE na katibu wake ni SLAA mpaka uchanguzi mkuu full stop.
 
Sifa hizo zote anazo mbowe, pamoja na hizo ambazo hujataja, kwa kuwa CHADEMA wanahitaji kiongozi mwenye msimamo na anayejua afanye nn wakati gani? bila kujali anaelimu ya uprofesa au ni DR. Kwa kuwa hata kama hujasoma hata darasa moja maishani mwako lakini kama unauwezo wa kukifanya chama kisonge mbele kama ilivyo kwa chadema hivi sasa, wala hatuhitaji ma DR waongoze chama wala maprofesa, swala lengo lifikiwe.
 
Kumekuwepo na harakati nzuri sana ndani ya CDM za kuhakikisha kuwa chama kinakuwa imara siku hadi siku. Kumekuwepo na viongozi wa kila aina ngazi zote ambao kwa kweli wamefanya kazi nzuri na kuhakikisha kuwa CDM kimekuwa chama tishio kwa CCM. Ili kuendelea sasa kuimarisha chama ni muda sasa kumpata Mwenyekiti ambaye ataendelea kukiimalisha chama na hatimaye kuwa chama kitakachoshika hatamu za uongozi. Hili litaweza kutokea kama tukiwa na Mwenyekiti na kiongozi mwenye sifa zifuatazo kwa maandalizi ya uchaguzi wa 2015:
1. Awe na umri wa zaidi ya miaka 40. Lengo ni kupata mtu mwenye uwezo mpana kidogo wa kushawishi vijana na wazee.
2. Awe na elimu angalau ya digrii moja. Kwa jinsi mabadiriko ya kiuchumi na technology yanavyotokea kwa kasi sana, ingekuwa busara kuwa na mtu wa kuweza kuchanganua sera, mikakati na mipango ya kimaendeleo, na hili kwa kweli elimu ndo msingi wa yote.
3. Awe mbunifu wa shughuli na kazi za maendeleo. Asitegemee kuambiwa na kuelekezwa tu, ni vema na yeye aweze kubuni sera, mikakati na mipango mbalimbali ya maendeleo.
4. Awe mwanachama wa CDM kwa takribani miaka 5 mfululizo. Hii ni kuweka imani kuwa angalau atakuwa ana uzoefu na sera za chama, mikakati na mipango ya chama. Uzoefu wa siasa za chama ni mzuri kwa kuendelea kuimarisha chama.
5. Awe na uwezo kifedha - ingawa wakati mwingine ni vigumu kujua uwezo wa kifedha wa mtu lakini uwepo mfumo wa uwazi ambao unaweza kuonyesha umiliki wa mali alizonazo. Hii itasaidia kumpata kiongozi ambaye ana uzoefu wa kuwekeza katika shughuli za uzalishaji, na tukiwa na imani kuwa hatakuwa fisadi na mwenye uchu wa pesa kupitiliza. Na ana uwezo wa kulipa ada na michango mbalimbali ya chama.
7. Awe na uzoefu wa kazi za kujiajili au kuajiliwa katika ngazi ya uongozi na utawala kwa takribani miaka 7. Hapa tunataka kuangalia uzoefu wake katika masuala ya Utawala na Uongozi. Kwa kuwa CDM ni taasisi kubwa tunategemea kumpata mzoefu wa kuendesha na kuongoza hii taasisi kubwa nchini.

mengine naomba mwendelezo.
Mkuu,kwani katiba ya chama chenu inasemaje kuhusu mambo hayo? Nilidhani cha muhimu ni mabadiliko ya katiba yenu ili iwezeshe kuwa na kiongozi wa aina unayotaka
 
Sifa hizo zote anazo mbowe, pamoja na hizo ambazo hujataja, kwa kuwa CHADEMA wanahitaji kiongozi mwenye msimamo na anayejua afanye nn wakati gani? bila kujali anaelimu ya uprofesa au ni DR. Kwa kuwa hata kama hujasoma hata darasa moja maishani mwako lakini kama unauwezo wa kukifanya chama kisonge mbele kama ilivyo kwa chadema hivi sasa, wala hatuhitaji ma DR waongoze chama wala maprofesa, swala lengo lifikiwe.
Hivi mbowe ana degree ngapi?
 
Nimeandika haya maoni nikijua kuwa Mbowe na Dr. Slaa na viongozi wengine ni viongozi halali na wanaweza pia kuchaguliwa kukiongoza chama. la pamoja na Katiba nzuri ya Chadema, ni vizuri kuangalia tunahitaji mtu wa namna gani kwa kipindi kichacho. kama Mbowe, Zitto, Mnyika , Tundu, Sugu na wengine wanaweza kuwa na sifa hizo pouwa tu chama kitakuwa imara sana. cha msingi ni namna ya kuimarisha chama bila kuangalia anatoka kanda gani au dini gani.

Chadema ni cama imara hadi muda huu.
 
Binafsi napendekeza , pindi uchaguzi utakapofanyika mbowe aendelee kuongoza, maana chini ya uongoz wa kamanda wa anga, chama kimekua sana ndo maana ccm wana ha ha kila siku, na ikumbukwe kuwa ccm kwa sasa wana copy na ku paste from chadema kama kutumia helicopter kwenye kampeni, naona vazi lao la kijani siku hizi nao wanalishona kama ngwanda mfano baathi ya mavazi ya nape, yapo mambo mengi ila kwa ujumla kamanda wa anga arudi mzigoni kuongoza hatamu ya chama. polen sana vijana wa lumumba na buku 7 7 zenu njaa itawapeleka pabaya
 
soma katiba ya chama kwanza, pili m/kiti wa chadema ni MBOWE na katibu wake ni SLAA mpaka uchanguzi mkuu full stop.

Tatizo lenu ndio hilo,Ina maana hakuna wengine wenye uwezo wa kukisogeza Chama mbele kidogo ya hapa kilipifika?Mnawavunja moyo Makamanda wengine waliokuwa na ndoto ya kukifanyia Chama hiki mambo makubwa zaidi ya haya na zaidi mnakinyima Chama fursa ya kuwapata Viongozi walio bora zaidi.
 
1.awe anatokea kaskazini
2. awe mchaga
3. awe anajua kuongea kichaga, kimbulu au lugha hizi zote
4. awe mkiristo
5.ajue kutukana vizuri awapo jukwaani
6....
7..
 
Pole sana ni wapi tena utakuta story za cdm embu tujuze kama ulikuwa hujui jf ni cdm product pole sana endelea kujitekenya na ucheke mwenyewe.

Back
Top Bottom