Mwenyekiti Halmashauri ya Iramba ashauri Uchangudoa uhalalishwe kuongeza mapato

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iramba mkoani Singida, Simon Tyosela amesema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua ukusanyaji mapato ya Halmashauri mbalimbali
-
Alitoa ushauri huo, kutokana na kauli ya Mkuu wa Mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi aliyoitoa wakati wa Kikao Maalumu cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) kuwa madada poa na machangudoa wote mjini hapo watakamatwa
-
Tyosela alieleza “Niseme sikubaliani kamwe na suala la ushoga. Lakini hili la machangudoa nashauri lirasimishwe ili Serikali iweze kujipatia mapato. Iwapo watashindwa kulipa kodi, basi watakuwa wamejiondoa kwa hiyari yao wenyewe."
-
Hata hivyo, Meya wa Manispaa ya Singida, Gwae Mbua alipinga ushauri huo kwa madai kuwa hatua hiyo itadhalilisha Taifa kwani wanaojiuza ni ndugu zetu, dada zetu na watoto wetu.
 
unaongea kitu ambacho unajua kuwa n kinyume na imani yako, kinyume na sheria ya nchi, unakubali kuhalalisha uchafu kwa vile na wafaransa wanafanya,, fikiria mtoto wako aje kufanya hayo utajiskiaje. acha kuwa na fikra nyembamba. sio kila kilichoruhusiwa ni halali, pombe sigara etc
Acha unafiki, baadae unaenda kupiga short time..
 
unaongea kitu ambacho unajua kuwa n kinyume na imani yako, kinyume na sheria ya nchi, unakubali kuhalalisha uchafu kwa vile na wafaransa wanafanya,, fikiria mtoto wako aje kufanya hayo utajiskiaje. acha kuwa na fikra nyembamba. sio kila kilichoruhusiwa ni halali, pombe sigara etc
MBONA MNAFANYA UZINZ? MBONA MNACHUKUA WAKE ZA WATU? MBONA MNASODOMA NA GOMORA NA MBONA MNATEMBEA NA WATOTO WADOGO WANAFUNZI HAYO HAMYAONI? TUWE WAKWELI KWA KILA JAMBO TUSIFANYE NDIMI ZETU ZIKAWA ZA KINAFKI WAKATI MNAFANYA YOTE NA JE HAYO YOTE MMELETEWA NA WAZUNGU?

SHERIA ZIPO ZIPO NA JE ZINAFUATWA? KWA HAKI FIKIRI MARA MBILI UTAJUA NINI NA MAANISHA HUWEZ KUSEMA KUHALALISHA BIASHARA YA KUUZA MWILI NI KINYUME CHA SHERIA WAKATI HAO WASIMAMIA SHERIA NDIO WAVUNJA SHERIA WAKUBWA WAMEJIVIKA NGOZI YA KONDOO
 
Ili wapate number ya mlipa kodi lazima wafanyiwe blood test

Tena itapendeza kama wakipewa vitambulisho vya tsh20,000
 
Bravo well said! Watu hawapendi kuambiwa uhalisia, yaani ni full unafiki that's why tumekuwa miongoni mwa wanaoongoza kwa hili gonjwa duniani. Na kwa unafiki huu hata pepo huenda tusiione wallah!.
MBONA MNAFANYA UZINZ? MBONA MNACHUKUA WAKE ZA WATU? MBONA MNASODOMA NA GOMORA NA MBONA MNATEMBEA NA WATOTO WADOGO WANAFUNZI HAYO HAMYAONI? TUWE WAKWELI KWA KILA JAMBO TUSIFANYE NDIMI ZETU ZIKAWA ZA KINAFKI WAKATI MNAFANYA YOTE NA JE HAYO YOTE MMELETEWA NA WAZUNGU?

SHERIA ZIPO ZIPO NA JE ZINAFUATWA? KWA HAKI FIKIRI MARA MBILI UTAJUA NINI NA MAANISHA HUWEZ KUSEMA KUHALALISHA BIASHARA YA KUUZA MWILI NI KINYUME CHA SHERIA WAKATI HAO WASIMAMIA SHERIA NDIO WAVUNJA SHERIA WAKUBWA WAMEJIVIKA NGOZI YA KONDOO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kwa mwenye CV za huyu mtu atusaidie kuweka hapa, itapendeza zaidi ukiweka na picha yake ili tumfahamu vizuri.
Ahaante.
 
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Iramba mkoani Singida, Simon Tyosela ameishauri serikali kuhalalisha biashara ya akina dada wanaoujiuza, maarufu machangudoa.

Amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua ukusanyaji mapato ya halmashauri mbalimbali nchini.

Alitoa ushauri huo, kutokana na kauli ya Mkuu wa Mkoa, Dk Rehema Nchimbi kueleza kuwa madada poa na machangu doa wote mjini hapa watakamatwa.

Dk Nchimbi alitoa kauli hiyo wakati wa Kikao Maalumu cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichopitia na kupitisha Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2019/2020.

Tyosela amesema kutokana na halmashauri nyingi nchini kukwama kukusanya mapato, ingekuwa jambo jema kama serikali ingehalalisha biashara ya machangudoa kama zilivyo biashara nyingine.

“Niseme sikubaliani kamwe na suala la ushoga. Lakini hili la machangudoa nashauri lirasimishwe ili serikali iweze kujipatia mapato,”alisema na kuongeza:

“Iwapo watashindwa kulipa kodi hiyo, basi watakuwa wamejiondoa kwa hiyari yao wenyewe kwenye biashara hiyo, badala ya utaratibu uliopo wa polisi kuwakamata”.

Meya wa Manispaa ya Singida, Gwae Mbua alipinga ushauri huo, kwa madai kuwa hatua hiyo itadhalilisha taifa.

“Wanaojiuza ni ndugu zetu, dada zetu na watoto wetu... wamekuwa wakitutia aibu. Sikubaliani na wazo la Mwenyekiti wa Iramba kuhalalisha biashara hiyo kwa kuwa ni kinyume na utamaduni wa Mtanzania,” alisema.

Aliongeza; “Naomba wabunge waliopo humu wajifanye kama vile hawajasikia ushauri wa ndugu yangu huyu. Kuna namna nyingi za halmashauri kujipatia mapato, kinachotakiwa ni watendaji wetu kuwa wabunifu zaidi katika kubuni vyanzo vipya halali vya mapato na sio hii ya kuuza miili.”

Awali, kwenye kikao hicho cha RCC, Mkuu wa Mkoa, Dk Nchimbi alisema hakuna taifa linaloweza kuwa nchi ya viwanda na kuingia kwenye uchumi wa kati kwa kuendekeza vitendo vya kipuuzi kama vile akina dada kujiuza miili yao.

Alisema kuwa katika kuhakikisha mkoa unakuwa tulivu na unashughulika zaidi na maendeleo ya wananchi, umejipanga ipasavyo kuwaondoa machangudoa

Chanzo: HabriLeo

Sent using Jamii Forums mobile app

Namuunga mkono mwenyekiti, Kama watu wanafanya na wateja wapo kwanini isiwe biashara halali tusifiche ukweli kwa kujifanya tunajificha katika kichaka cha maadili wakati ikifika jioni tunawatufuta, tumeona hata wakati wa bunge pale Dododma mabinti huwa wanaenda kuuza nyapu zao.
 
unaongea kitu ambacho unajua kuwa n kinyume na imani yako, kinyume na sheria ya nchi, unakubali kuhalalisha uchafu kwa vile na wafaransa wanafanya,, fikiria mtoto wako aje kufanya hayo utajiskiaje. acha kuwa na fikra nyembamba. sio kila kilichoruhusiwa ni halali, pombe sigara etc
Wengi watakupinga na wengine kwa chuki tu za dini kama kwamba ile dini nyingine inaruhusu mambo Haya ila upo sahihi kabisa
 
pumbavu sana. mmoja wapo wa hao wafanyabiashara awe mtoto wake, dada yaka, shangazi yake, au hata aliyemzaa kama yupo
Wewe unadhani wasipohalalisha ndo wataacha kujiuza? Wateja mpo Sasa kwanini msilichangie taifa. Leo mtapinga ila ipo siku isiyo na jina hii biashara itahalalishwa.
 
Back
Top Bottom