Mwenyekiti Halmashauri ya Iramba ashauri Uchangudoa uhalalishwe kuongeza mapato

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,644
2,000
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Iramba mkoani Singida, Simon Tyosela ameishauri serikali kuhalalisha biashara ya akina dada wanaoujiuza, maarufu machangudoa.

Amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua ukusanyaji mapato ya halmashauri mbalimbali nchini.

Alitoa ushauri huo, kutokana na kauli ya Mkuu wa Mkoa, Dk Rehema Nchimbi kueleza kuwa madada poa na machangu doa wote mjini hapa watakamatwa.

Dk Nchimbi alitoa kauli hiyo wakati wa Kikao Maalumu cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichopitia na kupitisha Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2019/2020.

Tyosela amesema kutokana na halmashauri nyingi nchini kukwama kukusanya mapato, ingekuwa jambo jema kama serikali ingehalalisha biashara ya machangudoa kama zilivyo biashara nyingine.

“Niseme sikubaliani kamwe na suala la ushoga. Lakini hili la machangudoa nashauri lirasimishwe ili serikali iweze kujipatia mapato,”alisema na kuongeza:

“Iwapo watashindwa kulipa kodi hiyo, basi watakuwa wamejiondoa kwa hiyari yao wenyewe kwenye biashara hiyo, badala ya utaratibu uliopo wa polisi kuwakamata”.

Meya wa Manispaa ya Singida, Gwae Mbua alipinga ushauri huo, kwa madai kuwa hatua hiyo itadhalilisha taifa.

“Wanaojiuza ni ndugu zetu, dada zetu na watoto wetu... wamekuwa wakitutia aibu. Sikubaliani na wazo la Mwenyekiti wa Iramba kuhalalisha biashara hiyo kwa kuwa ni kinyume na utamaduni wa Mtanzania,” alisema.

Aliongeza; “Naomba wabunge waliopo humu wajifanye kama vile hawajasikia ushauri wa ndugu yangu huyu. Kuna namna nyingi za halmashauri kujipatia mapato, kinachotakiwa ni watendaji wetu kuwa wabunifu zaidi katika kubuni vyanzo vipya halali vya mapato na sio hii ya kuuza miili.”

Awali, kwenye kikao hicho cha RCC, Mkuu wa Mkoa, Dk Nchimbi alisema hakuna taifa linaloweza kuwa nchi ya viwanda na kuingia kwenye uchumi wa kati kwa kuendekeza vitendo vya kipuuzi kama vile akina dada kujiuza miili yao.

Alisema kuwa katika kuhakikisha mkoa unakuwa tulivu na unashughulika zaidi na maendeleo ya wananchi, umejipanga ipasavyo kuwaondoa machangudoa

Chanzo: HabriLeo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

MAMESHO

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
719
1,000
pumbavu sana. mmoja wapo wa hao wafanyabiashara awe mtoto wake, dada yaka, shangazi yake, au hata aliyemzaa kama yupo
 

abdi ally

JF-Expert Member
Dec 4, 2018
1,568
2,000
mbona ufaransa ipo kabisa hyo biashara na karibu nch zote za ulaya na america sema ziwekwe taratibu stahki na kuwahakikishia usalama wao na hata ukizuia haitokaa kuisha kabisa watuu wanauza kwa simu tu siku hzi
 

MAMESHO

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
719
1,000
mbona ufaransa ipo kabisa hyo biashara na karibu nch zote za ulaya na america sema ziwekwe taratibu stahki na kuwahakikishia usalama wao na hata ukizuia haitokaa kuisha kabisa watuu wanauza kwa simu tu siku hzi
unaongea kitu ambacho unajua kuwa n kinyume na imani yako, kinyume na sheria ya nchi, unakubali kuhalalisha uchafu kwa vile na wafaransa wanafanya,, fikiria mtoto wako aje kufanya hayo utajiskiaje. acha kuwa na fikra nyembamba. sio kila kilichoruhusiwa ni halali, pombe sigara etc
 

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
2,367
2,000
unaongea kitu ambacho unajua kuwa n kinyume na imani yako, kinyume na sheria ya nchi, unakubali kuhalalisha uchafu kwa vile na wafaransa wanafanya,, fikiria mtoto wako aje kufanya hayo utajiskiaje. acha kuwa na fikra nyembamba. sio kila kilichoruhusiwa ni halali, pombe sigara etc
Nchi haiendeshwi kwa misingi ya kidini hii, ambayo ni taratibu za waarabu kuishi karne ya 7 huko

Inaendeshwa kwa sheria za wanadamu walizozitafakari na kuona zina faida kuliko madhara....
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,495
2,000
Uchangudoa ukiruhusiwa Kisheria Huenda ukapungua maana Kuna Binadamu flavor Yao ni kula vilivyokatazwa

Anaacha kula Mbuzi anaenda kula Nyani

Anaacha kutumbukiza Kwenye uke anaenda kutumbukiza Kwenye Bomba la kutolea Moshi

Anaacha Mwanamke anaenda kuburuza Mwanaume mwenzake
 

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
11,497
2,000
Huyo kaichoka kazi yake au inawezekana anakaribia kustaafu kwahiyo kaamua kuropoka...
 

jocefhurs

Senior Member
May 14, 2018
125
225
Watanzania kwa kujidai watakatifu wenye kufuata dini na wenye mila na desturi safi hatujambo....but tujiulize inakuwaje nchi yetu ni miongoni mwa zinazoongoza kwa kuwa na waathirika wengi wa HIV.
unaongea kitu ambacho unajua kuwa n kinyume na imani yako, kinyume na sheria ya nchi, unakubali kuhalalisha uchafu kwa vile na wafaransa wanafanya,, fikiria mtoto wako aje kufanya hayo utajiskiaje. acha kuwa na fikra nyembamba. sio kila kilichoruhusiwa ni halali, pombe sigara etc

Sent using Jamii Forums mobile app
 

CROSSFIRE

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
466
1,000
Hii hoja haipaswi kuungwa mkonyo hata kidogo maana ina-promote maambukizi ya magonjwa ya zinaa na ukimwi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom