Mwenye wimbo wa Tazama ramani

Dah!!!! Nimejikuta nacheka tu, mkuu umekubuka nini hadi kuuhitaji huo wimbo wa zamani hivo?????
 
Kwa jinsi watu wasivyo wazalendo ukimwambia aimbe wimbo wa Taifa bila kudesa hawezi!
 
Mwenye wimbo wa Tazama raman utaona nchi nzuri yenye mito na mabonde....... Anisaidie Audio
Mara ya mwisho kuusikia ilikuwa ibada maalum ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru, kanisani la Kristu Mfalme Tabata. Mpangilio wa sauti na kinanda ilikuwa baraa, hadi nikajiuliza maswali mengi sana.
 
Tazama ramani utaona nchi nzuri yenye mito na mabonde mengi yanafakaa
Nasema kwa kina halafu kwa kufikirii
Nchi hiyo yenye amani huitwa Tanzaniaaa

---

Mbali sana kwakweli. Nakumbuka miaka ilee tukiwa primary kila ijumaa lazima kuimba wimbo wa uzalendo.
 
Japo nimesoma zama za kikwete sisi hatukuuimba ila ni mzuri niliwahi kuusikia kwenye Radio mama yangu alinisimulia mengi juu ya uo wimbo enzi zao
 
Nyimbo hizi zilikuwa zinatufanya kuwa wamoja, siku hizi hamna anaye ona umuhimu wa hizi nyimbo, kila mtu yupo busy kuchochea ukabila, ukanda na udini
 
Back
Top Bottom