Ndugu ulikuwepo Zanzibar wakati wa vuguvugu lile la uamsho?
Ulihudhuria ile mihadhara yao iliyokuwa ikifanyika.? Kuanzia pale Darajani, lumumba, au kule mahonda.?
Unafahamu kilichokuwa kinatokea mitaa ya jang'ombe na kiembe samaki au kwa mchina baada ya mihadhara ile?
Unafahamu madhara waliyoyapata watu baada ya mihadhara ile..?
Hebu fikiri kidogo kama wasinge zuiliwa hii Nchi leo hii ingekuwa wapi? Unakumbuka wale mapadri walio uwawa kule zanzibar?
Unakumbuka zile tindikali walizomwagiwa watu kule unguja.? Tulia kidogo vuta kumbukumbu kisha waza kama hawa masheke! Wangekuwa huru leo hii zanzibar ingekuwa wapi?
Bila shaka hawa na wale wa Kibiti ni ndugu moja, na wale waliokuwa wanasema Pwani si Kenya ni hawa hawa na style zao ni zilezile.
Ndugu kukamua jipu ili kutoa usaha ndani kuna hitaji roho ngumu ni lazima anayekamuliwa alalamike sana.kwa maumivu lakini hiyo ndiyo dawa pekee.
Tunashukuru serikali kwa hatua makini walizo chukua ningekuwa na uwezo ningekutumia hapa hotuba zao, na madhara yaliyotokea kwenye jamii baada ya hotuba zile. Kama uko Unguja hadithi hizi sio ngeni kwako.
Ktk kudai haki lazima kuna madhara yatakayotokea....na ukiogopa kudhurika ukubali kupoteza haki yako"
Ktk dini imeelekezwa kudai haki na kupinga maonevu, kumbuka uamsho ilikuwa ni kikundi cha kidini"
Mihadhara waliokuwa wakifanya serekali ndo ilikuwa inatoa kibali\ kama ilivokuwa huku kipindi cha kampeni, wanatoa kibali, katikati ya mkutano poliss wanvamia na kutawanya watu.
Jaribu kuangalia video zao YouTube halafu upinge kwa hoja. (Ndo serkali ilipokwama)
Kuna njia nyingi za kudai haki, wale walipitia kwenye dini. (Ndo kada yao) ilitakiwa na makundi mengine ktk jamii yasapot
Nakuhakikishia majority ya wazanzibar wanawapenda uamsho, na ndio maana walikuwa wanafurika kwenye mihadhara yao, (ilikuwa ni mwiba kwa serkal) mpaka kesho bado wazanzbar wanachangia hela kwa ajili ya hawa masheikh.
Japo unaishukur serekali kuwaweka ndani lakini sijui ni kwa nn huoni kama ni uonevu kumuweka mtu ndani zaidi ya mika 5! Bila kumfungulia kesi!!
Unaweza kufurahia tu kwasababu yametokea upande wa Pili, (waislam)!!
Tunawajibu wa kuitetea jamii yetu thidi ya uonevu bila kujali dini kabila wala vyama"
Yaa rabii...wajaalie viongozi wetu, uwape hekima na mioyo ya imani watutendee mema wanaotuongoza'
"uwape stahamala masheikh wetu walioko mahabasu"
Mungu ibariki Tanzania yetu"