Nimemaliza chuo mwaka huu pale Mbeya University of Science and Technology. Bahati mbaya nilikuwa na supp ambayo nilifaulu ila system ya chuo ilisumbua kwenye kuweka matokeo yangu.
Baada ya kufatilia wakaniwekea matokeo yangu Jumatano iliyopita. Shida inaanza Examination Officer ananiambia sitapata cheti mwaka huu itabidi nisubiri mwaka 1 maana vyeti huwa vinaagizwa mara 1 kwa mwaka, wanachoweza kunisaidia kwa mwaka huu ni kunipa provisional certificate.
Wasiwasi wangu ni kwamba, je hii provisional certificate itatambulika kwenye taasisi mbalimbali? Najua humu kuna HR na wazoefu.
Msaada tafadhali.