Farolito
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 11,634
- 26,373
Wakuu Salaam!
Njia za Kisasa za uzazi wa mpango ambazo zimekua zikitumika hasa nchi za kiafrika pamoja na kuwa na msaada lakini zimekua zikisababisha madhara makubwa ya Kiafya lakini Mara nyingi matangazo ya njia hizi yamekua yakisema ni maudhi madogo madogo tu.
Nimebahatika kusoma kitabu cha Shirika la Pro-life Tanzania ambacho kimeelezea njia zote na madhara yake kwa kila njia kiukweli madhara ni makubwa sana ikiwemo saratani nk.
Katika kupita mitandaoni nilibahatika kukutana na kifaa hiki kinachoitwa LADY-COMP
Hiki ni kifaa ambacho kinatumika kama mbadala wa njia za kisasa za uzazi wa mpango kwani hakiingizi kemikali wala kifaa chochote ndani ya mwili wa binadamu na hakina madhara yoyote .
Ni kifaa ambacho kina mfumo wa computer kwa ajili ya kupima na kuhifadhi taarifa za hali ya uzazi(Fertility) ili kukuonesha Siku ambazo ni salama na sio salama katika mzunguko wa mwanamke.
Kwa mujibu wa maelezo jinsi kinavyofanya Nazi ni rahisi sana kwani kinachotakiwa ni mwanamke kupima joto lake kila Siku asubuhi(mdomoni)na kuingiza kwenye kifaa hicho zoezi ambalo linachukua sekunde 30 tu,pia kama upo kwenye hedhi utatakiwa kuingiza taarifa hio na hapo kitakua kinaweza kuhifadhi na kukupa taarifa za Siku salama za zisizo salama kwa uhakika kwa asilimia 99.3 kwa kuonesha taa nyekundu, njano na kijani.
Najua humu kuna madaktari na wataaam mbalimbali lakini pia wapo watu pengine wameshakiona au kutumia kifaa hiki ,Je ni salama na kinafanya kazi kama inavyoelezwa?
Kifaa hiki kimeanza kutengenezwa nchini Ujerumani tangu mwaka 1986 ni kinatumika zaidi ya nchi 35 na wanasema ukinunua hakuna gharama zingine za ziada na kinauwezo wa kudumu zaidi ya miaka 10 na bei yake nimejaribu kuangalia inaanzia $375.
Karibuni tupeane uzoefu pengine inaweza ikawa msaada kwetu kukwepa madhara zaidi.
NB.kifaa hiki hakizuii magonjwa ya Zinaa.
Lady Comp Ovulation Calculator - Ovulation Calculation safe & easy
Sent using Jamii Forums mobile app