Hizi simu za mkopo hutolewa kwa mhusika au mkopaji mwenye kadi/kitambulisho chake binafsi cha NIDA,leseni ya udereva au kitambulisho cha kura. Masharti ya simu ya mkopo ni kuwa uwe na kiasi fulani cha kulipia mwanzoni walau asilimia 15- 25 kutegemeana na bei ya simu, muuzaji au masharti ya supplier hasa Simu nyingii za SAMSUNG wana bei zao fixed.Sijui kwa sasa. Malipo ya mkopo ni siku,wiki,mwezi, miezi 3,6 au 12 na si zaidi. Utaratibu wa malipo mtawekeana na mkopeshaji lakini huwa wanapendelea kulipia kwa njia ya mitandao ya simu Yas, M pesa nk na simu yako itakuwa blocked usipolipa na wanaitrack kama utaleta usumbufu.Mtasaini mkataba na utachukuliwa picha ukiwa na simu yako ya mkopo pamoja na alama za vidole kwa ushahidi zaidi. Kwa kufupi riba ipo ila hawatasema ila unajiongeza. Ni hayo tu.