Nyangomboli
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 3,501
- 1,955
Wana-JF!
Ingawa kumekuwa na upotoshaji wa aina yake humu jamvini na kwengineko, kuhusu kauli ya mhe. Pinda, ila ukweli utabaki palepale kuwa mhe. Pinda ametoa kauli sahihi kwa wakati sahihi.
Kauli ya mhe. Pinda imepewa tafsiri ya uongo, kuwa imevunja katiba, hali iliyo pelekea wengi wenu kustaajabu kuwa ina kuwaje mwanasheria mkongwe kama mhe. Pinda kufanya hivyo, ila ukweli wa kauli yake mhe. Pinda ni huu hapa;
Mhe. Pinda alivyosema polisi wapige tu, hakuwa ana maanisha kuwa polisi wapige tu raia hovyo hovyo, lah hasha, bali alimaanisha polisi wadhibiti kwa maana ya kuwapiga raia wenye kukaidi maagizo ya dola.
Wote humu jamvini tunajua ni wajibu wa polisi kulinda raia na mali zao, lakini kwa vurugu za hivi karibuni, usalama wa raia umekuwa hatarini, kutokana na fujo za vyama vya siasa, kwa hali kama hiyo, serikali ni lazima ingetoa kauli, kauli yenyewe ndio hiyo ya mhe. Pinda.
Kauli ya mhe. Pinda imekuwa faraja kwa wapenda amani na utulivu wa hapa nchini, lakini imekuwa ni mwiba kwa wapenda fujo na maandamano yasiyo na tija yoyote kwa taifa.
Mhe. Pinda asante, TAIFA LIPO SALAMA SASA.
sina uhakik kama unafahamu ulichoandika. Hakuna mtu anaruhusiwa kumpiga au kumtesa au kutoa adhabu yoyote yenye kudhalilisha. tena katiba imesrma wazi kwa kutumia nen
o maarufuku. police wanatumia nguvu pisipo na uazima. wanapaswa tumia silaha kwa mtu mwenye siaha n au kipigo kwa mtu anartumia nguvu ili wamkamate. nyie mshanfilieni tu huyu mzee lakini mtaona mwisho wake.