Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
FL1 huu msemo ulitumika sana kutuharibia mielekeo ya maisha yetu tulio wengi. eti ukimpenda mtu basi penda na mabaya yake sasa wenguine tukajisahau tukapenda na mabaya kufukia mwishowe tukajalia ah mie siku hizi sikubaliUtalipendaje na miiba yakemiiba ikikuchoma ?
Ulipendapo waridi
Jali wake uchungu
Uchunguze muwaridi
Miba mingine michungu
Ukilitaka waridi
Chagua lilo stadi
Usilipende waridi
si rangi ilimradi
Ukilipenda waridi
Chagua lisokaidi
Ukilipenda waridi
Si lazima likuzidi
Ukilipenda waridi, changua likufaalo.
wanaita full package, ndivyo waridi linavyokuja mama amna jinsi.Utalipendaje na miiba yakemiiba ikikuchoma ?
Mwanakijiji ni ukweli usemavyo lakini kuna tofauti ya ukali wa miiba hiyo- kuna ile ambayo si mikali sana yenye kutoa ujumbe wa 'hey mie ni waridi so you should handle me with care' wakati kuna ile miiba ya 'usiniguse'Hilo ndilo nililogundua katika maisha; mtu anayetaka kumpenda mwingine ambaye hatomchoma inabidi asubiri hadi wakutane mbinguni. Ndiyo maana Mungu aliweka miiba kwenye waridi; wakati labda ni kwa ajili ya kulilinda hilo waridi siyo kudhuru wachumao!
Hilo ndilo nililogundua katika maisha; mtu anayetaka kumpenda mwingine ambaye hatomchoma inabidi asubiri hadi wakutane mbinguni. Ndiyo maana Mungu aliweka miiba kwenye waridi; wakati labda ni kwa ajili ya kulilinda hilo waridi siyo kudhuru wachumao!
Kwanini hakuna waridi la asili la rangi ya
kijani?
Ukilipenda waridi
Upende na miiba yake
Ukiwa na ukaidi
utaona tamu yake!
Ukilipenda waridi
Upende na rangi yake
Likiwa kwako zawadi
Mkononi ulishike
Ukilipenda waridi
Upende harufu yake
Furahia kama udi
Kama uko Chakechake
Ukilipenda waridi
Penda na madhari yake
Lipande kwa ustadi
Liwe lako siyo lake!
Ukilipenda waridi, lipende na miiba yake!!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji))
Hivi waridi lina miiba?
nadhani mawaridi ya kichina hayana!
InapendezaAha,hivi hukuona hiyo rangi mkiani.
Mie,naona hiyo ni ile ya kijani.
Duh!inapendeza kama jezi za watani.
Mfano,ua lote likawa kijani.
Unadhani,Yanga wangecheza na nani?
Wa Kjj,au hauutaki utani?
Maisha yaendele lazima tuwe wapinzani.
Mmoja chini,mwingine Jukwaani.
Inapendeza
hasa ukizingatia kweli haya ndo mambo ya ushairi