Mwenye kupenda waridi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Ukilipenda waridi
Upende na miiba yake
Ukiwa na ukaidi
utaona tamu yake!

Ukilipenda waridi
Upende na rangi yake
Likiwa kwako zawadi
Mkononi ulishike

Ukilipenda waridi
Upende harufu yake
Furahia kama udi
Kama uko Chakechake

Ukilipenda waridi
Penda na madhari yake
Lipande kwa ustadi
Liwe lako siyo lake!

Ukilipenda waridi, lipende na miiba yake!!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji))
 
Ulipendapo waridi
Jali wake uchungu
Uchunguze muwaridi
Miba mingine michungu

Ukilitaka waridi
Chagua lilo stadi
Usilipende waridi
si rangi ilimradi

Ukilipenda waridi
Chagua lisokaidi
Ukilipenda waridi
Si lazima likuzidi

Ukilipenda waridi, changua likufaalo.
 
Utalipendaje na miiba yakemiiba ikikuchoma ?
FL1 huu msemo ulitumika sana kutuharibia mielekeo ya maisha yetu tulio wengi. eti ukimpenda mtu basi penda na mabaya yake sasa wenguine tukajisahau tukapenda na mabaya kufukia mwishowe tukajalia ah mie siku hizi sikubali

Nalichagua waridi
Lile linivutialo
Kwa rangie muwaridi
Na miba lisiwenalo
 
Ulipendapo waridi
Jali wake uchungu
Uchunguze muwaridi
Miba mingine michungu

Ukilitaka waridi
Chagua lilo stadi
Usilipende waridi
si rangi ilimradi

Ukilipenda waridi
Chagua lisokaidi
Ukilipenda waridi
Si lazima likuzidi

Ukilipenda waridi, changua likufaalo.

my dear MJ1 umenivutia kumbe na fani hii upo well done ,mie hata kujaribu siwezi
one day nitakuonyesha ufundi wa kucheza charanga !
 
Hilo ndilo nililogundua katika maisha; mtu anayetaka kumpenda mwingine ambaye hatomchoma inabidi asubiri hadi wakutane mbinguni. Ndiyo maana Mungu aliweka miiba kwenye waridi; wakati labda ni kwa ajili ya kulilinda hilo waridi siyo kudhuru wachumao!
 
khee at a touch of love everyone becomes a poet.....
 
Hilo ndilo nililogundua katika maisha; mtu anayetaka kumpenda mwingine ambaye hatomchoma inabidi asubiri hadi wakutane mbinguni. Ndiyo maana Mungu aliweka miiba kwenye waridi; wakati labda ni kwa ajili ya kulilinda hilo waridi siyo kudhuru wachumao!
Mwanakijiji ni ukweli usemavyo lakini kuna tofauti ya ukali wa miiba hiyo- kuna ile ambayo si mikali sana yenye kutoa ujumbe wa 'hey mie ni waridi so you should handle me with care' wakati kuna ile miiba ya 'usiniguse'

So yanatofautiana -ukiingia tu na wimbo wa ukipenda waridi penda na miiba yake unawezajikuta unafika mahali miiba inakuelemea ukalazimika kubwaga manyanga chini
 
Hilo ndilo nililogundua katika maisha; mtu anayetaka kumpenda mwingine ambaye hatomchoma inabidi asubiri hadi wakutane mbinguni. Ndiyo maana Mungu aliweka miiba kwenye waridi; wakati labda ni kwa ajili ya kulilinda hilo waridi siyo kudhuru wachumao!

Huu sasa msamiati wakutane mbiguni?
kama matendo ya mmoja hayakuwa mazuri akaenda motoni itakuwaje ??
 
Kwanini hakuna waridi la asili la rangi ya
kijani?

Naumiza mtima,kufikiri kwa makini.
Inanijia adhima,kukujibu kwa yakini.
Kwa heshima,nakuuliza Mkjj kulikoni?.
Eti ni vyema,Waridi kuwa kijani?

Wapi umeshaona,ya miguuni kuwa kichwani?
Au labda umesoma,ya bahari kuwa ziwani?
Samaki utasema,ila kweli hawafanani.
Eti ni vyema,Waridi kuwa kijani?

Mtume simama,Usifikili kama punguani.
Utaipata laana,kumpituka Manani
Yeye ajua maana,kaliweka mibani.
Eti ni vyema,Waridi kuwa kijani?
 
Hiyo kweli kabisa MMM.kuna wengine wanapenda waridi tu hafu miiba yake hawapendi.
 
Ukilipenda waridi
Upende na miiba yake

Ukiwa na ukaidi
utaona tamu yake!

Ukilipenda waridi
Upende na rangi yake
Likiwa kwako zawadi
Mkononi ulishike

Ukilipenda waridi
Upende harufu yake
Furahia kama udi
Kama uko Chakechake

Ukilipenda waridi
Penda na madhari yake
Lipande kwa ustadi
Liwe lako siyo lake!

Ukilipenda waridi, lipende na miiba yake!!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji))

Hivi waridi lina miiba?
 
Mimi nilifikiri hata ya asili hayana miiba.

52102-bigthumbnail.jpg
 

Aha,hivi hukuona hiyo rangi mkiani.
Mie,naona hiyo ni ile ya kijani.
Duh!inapendeza kama jezi za watani.
Mfano,ua lote likawa kijani.
Unadhani,Yanga wangecheza na nani?
Wa Kjj,au hauutaki utani?
Maisha yaendele lazima tuwe wapinzani.
Mmoja chini,mwingine Jukwaani.
 
Aha,hivi hukuona hiyo rangi mkiani.
Mie,naona hiyo ni ile ya kijani.
Duh!inapendeza kama jezi za watani.
Mfano,ua lote likawa kijani.
Unadhani,Yanga wangecheza na nani?
Wa Kjj,au hauutaki utani?
Maisha yaendele lazima tuwe wapinzani.
Mmoja chini,mwingine Jukwaani.
Inapendeza
hasa ukizingatia kweli haya ndo mambo ya ushairi
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom