Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Ukilipenda waridi
Upende na miiba yake
Ukiwa na ukaidi
utaona tamu yake!
Ukilipenda waridi
Upende na rangi yake
Likiwa kwako zawadi
Mkononi ulishike
Ukilipenda waridi
Upende harufu yake
Furahia kama udi
Kama uko Chakechake
Ukilipenda waridi
Penda na madhari yake
Lipande kwa ustadi
Liwe lako siyo lake!
Ukilipenda waridi, lipende na miiba yake!!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji))
Upende na miiba yake
Ukiwa na ukaidi
utaona tamu yake!
Ukilipenda waridi
Upende na rangi yake
Likiwa kwako zawadi
Mkononi ulishike
Ukilipenda waridi
Upende harufu yake
Furahia kama udi
Kama uko Chakechake
Ukilipenda waridi
Penda na madhari yake
Lipande kwa ustadi
Liwe lako siyo lake!
Ukilipenda waridi, lipende na miiba yake!!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji))