Mwenye kuhitahi kubadilishana Eneo, Dar na Dodoma

mkada

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
1,200
906
Wana bodi,
Nina eneo Dar lenye ukubwa wa heka moja, lipo mwasonga kigamboni, nimehamia Dodoma kama sehemu ya mpango ya uhamishaji wa shughuli za serikali kutoka Dar kwenda Dodoma...naomba mwenye eneo Dodoma maeneo ya Kisasa, Ilazo, Ntuka au sehemu yoyote lakini lenye umeme na maji tayari, tubadilishane na eneo langu la Dar....eneo lako liwe limepimwa. Eneo langu la mwasonga halijapimwa lakini ni zuri kwa kujenga na kulima.
Ahsanteni.
 
usijaribu tulia kwanza kwakuwa unayahitaji yote mawili usifanye papala na ardhi ardhi ya dodoma ipo vumilia kidogo
 
uza dar kanunue dodoma hiyo bartertrade itakuchukua muda mrefu na process ndefu za logistic
 
ungetulia kidogo, maana serikali haieleweki unaweza jikuta siku moja uko katavi, sijui utabadilishana na wa dodoma tena, nakushauri tafuta aridhi nyingine tu ununue unless kama makazi yako umeamua yawe dom milele. kiwanja cha kingamboni tafuta namna ukiendeleze,ila malengo yako ndo yakuongoze mkuu kila a kheri
 
Back
Top Bottom