Mwenye Degree yake anafanya haya, kweli vyuma vimekaza

PR-means Public Relations hivyo anahusika moja kwa moja katika kufanya advertising, marketing and media relations ili kufikisha tarifa husika kwa umma. Na kwa kitendo cha wewe kumpost humu umemrahisishia kufanya marketing through social network. Ni dhahiri kwa juhudi zake atakuwa PR mkubwa sana mbeleni
 
10c6e707c140687245fd68ad9a9c385e.jpg
a5516cde15aa084f1288b0a18acde19d.jpg
4c90dbb1ed7de792ab24fe143a73c4ef.jpg

Jamaa ana degree yake ya PR toka pale SAUT kaamua kujilipua kihivi
Hii ni kiashiria vijana tuna hali mbaya kitaa
Wewe unayesubiri kuajiriwa na serikali endelea kusubiri kijiweni hivyo hivyo!
Nakuambia utaomba hadi sabuni ya kuogea kwa wazazi wako.
Pia inaonyesha kaelimu kako ulikokapata hakatakusaidia, kwasababu wewe ni mbinafsi. Unangoja vya kunyongwa.
 
Good reasoning Comrade.

Maswali fikirshi kama haya huwa hayapati majibu Mkuu. Tuna kasumba za ajabu sana (Nb; Nikiwa mmoja wao).

Falsafa za, Nenda shule-Soma kwa bidii-Faulu mitihani-Utapata kazi nzuri= Sufuri. Zinatuathiri mno kisaikolojia. Kiyosaki analizungumza kila uchwao katika tawasifu zake ila hatutokaa tumuelewe.

Specification zinatuachia maswali mengi mno yaso na majibu vichwani.

Lets change our graduates mindset.
Nina rafiki yangu mmoja ambaye alifungua genge la kuuza mboga mboga na mahitaji mengine madogo madogo ya nyumbani ambapo kipato alichokuwa akikipata alijiendeleza kielimu na sasa navyoandika tayari ni ana PhD na ni mkufunzi wa UDOM.
Hi kasumba ya watu kudhani kwamba kwa kuwa yeye ni msomi wa kiwango cha shahada hawezi kufanya kazi anayodhani ingefaa kufanywa na mtu asiye na kiwango kama chake kielimu imesababisha wengi kuishi maisha magumu sana na kuishia kulaumu serikali na circumstances kwa ujumla!
Nadhani tukibadili hii mentality tutafika mbali!
 
Mm nlijua labda ana pesa ndio anafanya hayo kumbe ni degree tu muache apambane na hali yake
 
Big up kwake na hiyo ndo maana halisi ya PR...

Kufanikiwa sio kuwa na degree Bali ni uthubutu na ujasiri uliochanganyikana na uvumilivu ndani yake katika kufukuzia ndoto yako
 
10c6e707c140687245fd68ad9a9c385e.jpg
a5516cde15aa084f1288b0a18acde19d.jpg
4c90dbb1ed7de792ab24fe143a73c4ef.jpg

Jamaa ana degree yake ya PR toka pale SAUT kaamua kujilipua kihivi
Hii ni kiashiria vijana tuna hali mbaya kitaa
ajira ime kuwa ngumu ,lakini kuna watu wana lalamika hawana mitaji uka angalia ana miliki simu ya laki 8 ana laptop ya laki 7 si uuze ufungue biashara ya kuku wa mayai
 
Back
Top Bottom