Mwenge wa uhuru wa Zanzibar uko wapi?

Mwenge wa uhuru wa Zanzibar uko wapi?

battawi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2014
Posts
2,714
Reaction score
2,582
Kama swali linavyo jieleza,mwenge huu wa uhuru wa Tanganyika unavuuka bahari kila mwaka na kukimbizwa mikoa na wilaya zote za Unguja na Pemba huku ukiitwa mwenge wa uhuru.

Kwa ninachojuwa ,Historia ya mwenge huu ni alama ya uhuru wa Tanganyika 1961 uliowekwa juu ya mlima K/njaro ili kuangaza mipaka dhidi ya maadui wa uhuru na maaduiI wa amani na umoja..

Muungano wetu ulikuwa na mkataba maalum ulioanisha maeneo tuliyoungana na kuacha yote yasoyokuwemo kwenye makubaliano ya muungano kwa washirika wa muungano wenyewe bila ya kuathiri mkataba huu.

Ule mwenge uliingiaje kuwa wa muungano?

Pamoja na mambo ya muungano kuongezwa,mwenge haukuwemog
 
Hivi Mwenge wa Uhuru ulianza ku-exist lini? Kabla au baada ya Mapinduzi "matukufu" ya Zanzibar?
 
Mwenge wa Uhuru ulianza baada ya Uhuru wa Tanganyika na kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar auna uhusiano wowote na Zanzibar ila inaonekana umefanywa kuwa Mwenge wa Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kitu ambacho hakipo, kwasababu hakuna kitu kama Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Kaaazi kweli kweli nchi yetu hii. Yaani kama kitu cha msingi kama Mwenge wa Uhuru hakiko clear sijui kuna mauzauza mangapi nchi hii.
 
Kama swali linavyo jieleza,mwenge huu wa uhuru wa Tanganyika unavuuka bahari kila mwaka na kukimbizwa mikoa na wilaya zote za Unguja na Pemba huku ukiitwa mwenge wa uhuru.
Kwa ninachojuwa ,Historia ya mwenge huu ni alama ya uhuru wa Tanganyika 1961 uliowekwa juu ya mlima K/njaro ili kuangaza mipaka dhidi ya maadui wa uhuru na maaduiI wa amani na umoja..
Muungano wetu ulikuwa na mkataba maalum ulioanisha maeneo tuliyoungana na kuacha yote yasoyokuwemo kwenye makubaliano ya muungano kwa washirika wa muungano wenyewe bila ya kuathiri mkataba huu.
Ule mwenge uliingiaje kuwa wa muungano?
Pamoja na mambo ya muungano kuongezwa,mwenge haukuwemog

Mwenge ni ramli ya kizanaki ulikuwa unatumika kishirikina na machief ili kunyamazisha watawaliwa for smooth leadership. Sasa znz inatawaliwa na ccm hivyo ccm ka wafanyavyo bara ndio hivyo hivyo znz. Nyerere alipona mapinduzi nane kwa ramli hii. Someni historia ndugu zangu. Huu ni uchawi.
 
Mwenge ni ramli ya kizanaki ulikuwa
unatumika kishirikina na machief ili
kunyamazisha watawaliwa for smooth
leadership. Sasa znz inatawaliwa na
ccm hivyo ccm ka wafanyavyo bara
ndio hivyo hivyo znz. Nyerere alipona
mapinduzi nane kwa ramli hii. Someni
historia ndugu zangu. Huu ni uchawi.
 
Kama swali linavyo jieleza,mwenge huu wa uhuru wa Tanganyika unavuuka bahari kila mwaka na kukimbizwa mikoa na wilaya zote za Unguja na Pemba huku ukiitwa mwenge wa uhuru.
...

Mkuu iko hivi:-

Mwenge wa Uhuru unaashiria nuru na mwanga. Uliwashwa kwa mara ya kwanza juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro mwaka 1961. Mwenge huu unamulika nchini na nje ya mipaka ili kuleta matumaini pale ambapo kuna kukata tamaa, upendo pale kwenye chuki na heshima pale penye dharau.Kila mwaka kuna mbio za mwenge zinazoanzia kwenye mikoa tofauti kuwakumbusha Watanzania jukumu lao la kulinda uhuru, umoja na amani ambavyo vimekuwepo na kudumu. (Tovuti Kuu ya Serikali: Mwenge wa Uhuru)

Usituambie Zanzibar haiyahitaji yote hayo. Jambo jema ni kwamba Mwenge wa Uhuru unamulika hadi "nje ya mipaka" na sio wa Tanganyika tu kama inavyodaiwa.
 
unafikiri zanzibar wanauhitaji uo mwenge, wanalazimishwa tu na michango ya mwenge zanzibar wanayokatwa wafanyakazi sio kwa ridhaa yao, ndio maana mwenge ukifika zanzibar wanaoshirikishwa ni watoto wa primary kwa sababu wenye akili zao hawana shida nao
 
Imeandikwa "ijuweni kweli nayo kweli itaweka huru"
Hivi ukiulizwa mwenge haswa umuhimu na malengo yake nini? Maana ya mwenge ni nini? Niliuliza mwalimu wangu nikiwa darasa la tano akakasirika maana hakuwa na jibu.

Sasa fahamuni tu ukweli kuwa chochote kisicho na nuru ni cha shetani. Sasa nuru ni uwazi wa maana ya kitu siyo mwanga wa kibatari. Mwenge haueleweki unamaana gani. Tafiti zimegundua ulitumika kishirikina na machief wa kizanaki ktk himaya zao ili kunyamazisha watawaliwa.
 
Mkuu iko hivi:-

Mwenge wa Uhuru unaashiria nuru na mwanga. Uliwashwa kwa mara ya kwanza juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro mwaka 1961. Mwenge huu unamulika nchini na nje ya mipaka ili kuleta matumaini pale ambapo kuna kukata tamaa, upendo pale kwenye chuki na heshima pale penye dharau.Kila mwaka kuna mbio za mwenge zinazoanzia kwenye mikoa tofauti kuwakumbusha Watanzania jukumu lao la kulinda uhuru, umoja na amani ambavyo vimekuwepo na kudumu. (Tovuti Kuu ya Serikali: Mwenge wa Uhuru)

Usituambie Zanzibar haiyahitaji yote hayo. Jambo jema ni kwamba Mwenge wa Uhuru unamulika hadi "nje ya mipaka" na sio wa Tanganyika tu kama inavyodaiwa.

Kwasababu huo mwanga na nuru unayozungumzia hata ukiwaka vipi unamulika mita mbili tu. Kwahiyo ni imagination kuwa unamulika hadi nje ya nchi. Chochote kinachofikirika huwa kipo kiroho na si asilia. Na chochote cha kiroho huwa ni cha Mungu au cha Shetani hakiwezi kuwa katika. Kama ni chema ni cha Mungu kibaya cha shetani.

Sasa wewe umesema mwenge unatoa matumaini pasipo na matumaini. Kwa wakristo Yesu mwenyewe anasema hivi "Mimi ndio.nuru na uzima". Kwahiyo kusema mwenge ni nuru ni kuwaletea wakristo Mungu mwingine.(Hapa waisikamu nao watanisaidia kufafanua upande wao ambao sijui). Anafafanua zaidi usimwaabudu Mungu mwingine ila mimi tuu. Sasa kwa maelezo yako hapo juu ni dhairi hatuwez wakriso tukatengeneza nuru nyingine nje ya Mungu tulie naye. Lakini pia Mungu kaonya juu ya kuabudu moto na kwakua mwenge ni moto ambao maana yake halisi kama jembe kaz yake linalima, bendera ni utambulisho haijaelezwa zaidi ya imagination. Yaani ka Kinjekitile Ngwale alivyokuja na maji kishirikina na kuwaaminisha asikari wake kuwa ukijipaka risasi haipenyi. Basi ni dhairi bila shaka kuwa mwenge ni wa shetani na ni ramli. Pia inathibitishwa na ukweli kuwa ulikuwa unatumika na
Machief wa Kizanaki kama njia ya kunyamazisha watawaliwa kwa imani hivi hivi.
 
Majibu ya maswali yako yanapatikana hapa: Tovuti Kuu ya Serikali: Mwenge wa Uhuru

Huko kote nilishapita siku nyingi. Ila zote ni nadharia not practical. Ni utopian yaani imagination ka ukienda kwa mganga anakupawambia tafuta kiungo cha albino uwetajiri. Sawa na kimbizeni mwenge mpate nuru. Jembe kazi yake kulima Bendera ni utambulisho sasa mwenge ni ni nini kwa vitendo siyo imani. Kunatofauti gani anaye ona matumaini kupitia mwenge na anayeona matumaini kupitia kiungo cha albino? Tukubaliane kuwa hata kama umekuwepo miaka hamsini tusikitike tu kuwa ni uchawi na ni ramli ka ramli zingine tu za kawaida.
 
Mwenge wa Uhuru ulianza baada ya Uhuru wa Tanganyika na kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar auna uhusiano wowote na Zanzibar ila inaonekana umefanywa kuwa Mwenge wa Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kitu ambacho hakipo, kwasababu hakuna kitu kama Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Everything is possible in Tanzania .................. provided that it achieves the objectives of the CCM's propaganda!!
 
Mwenge wa uhuru ni sanamu ya chama cha TANU ikiakisi uhuru wa Tanganyika. Ulibuniwa na Nyerere aliyekuwa na ndoto ya kutawala East Africa and eventually Africa nzima (akiwa na marafiki zake akina Kwame, etc). Kwa kuanzia kiujanja akaiteka Zanzibar. Jomo Kenyatta akamshitukia. Kuitawala kirahisi Zbr, akaamua kuunganisha vyama vya TANU na ASP, kuwa ccm.
Mwenge ni mali ya ccm na Zbr unakimbizwa kule kama ishara ya kutawaliwa na TANU.
 
Huu Mwenge una umuhimu gani ndugu yangu? au kuongeza maambukizi ya VVU.

[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD]The Uhuru Torch symbolizes freedom and light.(Uhuru wa kweli hivi sasa haupo , wote tunaona Gazeti la ----------- limefungiwa bila haki kwa vile tu limesema ukweli wa jinsi Dr Ulimboka alivyotekwa na kuteswa kule mabwepande) It was first lit on top of Mount Kilimanjaro in 1961.(Kweli Mwenge una uhusiano na Tanganyika bara tu na sio Zanzibar) Symbolically to shine the country and across the borders to bring hope where there is despair,( kila siku hivi sasa watu wanazidi kukosa matumaini na wanakata tamaa kwani maisha yanazidi kuwa magumu pamoja na kuimbiwa kila mara wimbo wa maisha mazuri) love where there is enemity (Watu hawapendani siku hizi kwani matabaka yamezidi , walionacho ndio kwanza hawataki tugawane keki ya Taifa) and respect where there is hatred. (Kuheshimiana hakupo tena mpaka Bungeni hivi sasa Mr Six anawaongoza wenzie kutoheshimu Maoni/Rasimu halali ya wanainchi) Yearly there is the Uhuru Torch race, starting from different regions throughout Tanzania, (Kila mwaka mwenge unaleta hasara kwa kukimbizwa, wazee vijijini wanachangishwa pesa/mifugo bila huruma ya kuangalia umaskini wao, Mwenge ukilala mahala fulani hebu nenda baada ya miezi mitatu kapime maambukizi ya ukimwi utajua hasara za Mwenge) to remind Tanzanians of their duty to jealously guard their cherished freedom, unity and peace. (Mwenge hauna tena mvuto wa kutuunganisha watanzania kama zamani na amani inayotajwa ni amani ambayo ipo kama picha ya Simba wa karatasi)[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
ZANZIBAR NYIE NDIO VIDUME VYA UHAKIKA HEBU MUULIZENI Mr Six MWENGE UPO KWENYE KATIBA NA SHERIA YA INCHI GANI
 
Back
Top Bottom