Mwenge University College of Education

Mwenge University College of Education

gbrother

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
408
Reaction score
51
Kwa wale mliopata post ya kuja kilichokuwa chuo kushiriki cha Mt Augustino tawi la moshi, (MWENGE)
NAKARIBISHA MASWALI YENU KUHUSU CHUO CHETU.

HONGERENI SANA KWA KUCHAGULIWA CHUONI HAPA, INGAWA KWA SASA TUMEPATA USAJIRI RASMI WA KUWA CHUO KAMILI, KUTOKA TAWI MAMA LA ST AUGUSTINE
 
Vipi kuhusu direct cost kwa first year?

Na mim mwenyewe ni mhitimu wa chuo hicho, kwa first year ukifika pale unalipa laki tatu na sitini ambayo itakuwezesha kusajiriwa alafu kama utapata hostel bei yake ni laki mbili na nusu, alafu jiandae na tope wakati wa mvua. Karibu mwenge
 
Hizo hosteli zinawatosha first year wote, nusu au robo?pia hiyo gharama ya hostel ni ya mwaka au semister?
 
Hizo hosteli zinawatosha first year wote, nusu au robo?pia hiyo gharama ya hostel ni ya mwaka au semister?

Hizo hosteli hazitoshi kwa first year wote ndo maana wanaopewa kipaumbele cha hosteli ni walemavu na wanachuo wanaotoka mikoa ya mbali kutoka kilimanjaro kwa mfano wanaotka kagera, kigoma, mwanza, ruvuma, lindi n.k, vyumba vya kupanga ni kuanzia elfu 35 hadi sitin kwa mwezi na hapo umeme mnachanga na maji unanunua ambapo ndoo moja ni sh. mia 3 hadi mia 4
 
hiyo laki 3 na 60 ya nn?

Hiyo laki tatu na 60 inaitwa administration fee ambayo ujumuisha pesa za usajili, kitambulisho, uongozi wa wanafunzi, na gharama nyingne nying nishazisahau na lazma uilipe ndo usajiliwe. Kwa wanaochukua koz za sayansi ulipiwa zote hadi hyo admistration fee hivyo urudishiwa pesa zao mwishon mwa semister ya pili ambapo board huwa tayari ilishawalipa ada za wanafunzi
 
Vyuo vingine bhana

Una maanisha nin mkuu au hupendi kuwepo na vyuo vikuu vya private ndo roho yako ifurahie zaidi, unataka watanzania wasipate degree ili muwe wachache wenye degree kutokana na kwamba vyuo vya serikali haviwezi kuchukua idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza form six. Acha roho mbaya bhana 😡
 
Hiki chuo cha wapi tena? Vyuo vya kata bhana.

Kipo Moshi, ni cha tangia 2005 ni miongini ya matawi ya mwanzo ya SAUT japokuwa huwa hakitangazi sana ndo maana hakijulikani ila kwa kanda ya kaskazin wanakijua kwa kuzalisha waalimu wazuri sana we ulizia mtu aliye kanda ya kaskazin atakwambia
 
Ok ahsante kwa taarifa.
 
Hiyo laki tatu na 60 inaitwa administration fee ambayo ujumuisha pesa za usajili, kitambulisho, uongozi wa wanafunzi, na gharama nyingne nying nishazisahau na lazma uilipe ndo usajiliwe. Kwa wanaochukua koz za sayansi ulipiwa zote hadi hyo admistration fee hivyo urudishiwa pesa zao mwishon mwa semister ya pili ambapo board huwa tayari ilishawalipa ada za wanafunzi
Thanks mkuu.
 
Baridaaa kabisa nimekusoma mkuu naelekea huko asante kwa dondoo!ila sijaluelewa hapo wakati wa tope?
 
Baridaaa kabisa nimekusoma mkuu naelekea huko asante kwa dondoo!ila sijaluelewa hapo wakati wa tope?

Mvua ikinyesha udongo wa kule ugeuka na kuwa tope na huwa na utelezi pamoja na kunata vilevile ugandamana na sole ya viatu na kukufanya utembee kwa shida uku miguu ikiwa mizito kama vile umefungiwa mawe ya kilo tano kwenye viatu
 
asante...vipi ukichelewa kuriport kama week moja na nusu hivi unaweza kupata hosteli? ni ndan ya sku ngap za kuriport unaweza kupata hostel kama watoka mbali?
 
asante...vipi ukichelewa kuriport kama week moja na nusu hivi unaweza kupata hosteli? ni ndan ya sku ngap za kuriport unaweza kupata hostel kama watoka mbali?

Unaweza kupata hostel ndio hata ukichelewa wiki tatu ni wewe tu kwa jinsi utakavyo ongea vizur na dean of students, akikupiga beat ukakubali mapema itakula kwako, ila nakushauri bora uwahi kufika na utafute magheto maana wanaokaaga hostel wakishazoea wanaonaga hostel inabana kwahyo utafuta vyumba vya kupanga ili kuwa huru zaidi lakin kama una elements za kilokole hostel itakufaa sana
 
Back
Top Bottom