Mwenge stend leo ni vunja bomoa ondoa

LEGE

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2011
Posts
5,122
Reaction score
9,222
Leo ukifika MWENGE lazima ushangae kwani ni kweupeee hakuna msongamano wa watu wala daladala stendi ni nyeupe mpaka raha.
hakuna kukanyagana tena wala kupigana vikumbo.

Leo asubuhi na mapema polisi FFU na baadhi ya mgambo wameendesha operation ya bomoa bomoa meza na mabanda yote ya wamachinga yaliyopo ndani nje nayaliyo karibu na MWENGE STENDI.

kiukweli wamefanya KAZI nzuri sana hasa ni baada yakuzifuata mpaka meza zilizokuwepo zimehifadhiwa.

sababu wangeziacha jioni wanazibeba na kujakufungua biashara na kuwapa pesa watu wanaojiona kama MWENGE STENDI ni yakwao Mali yao wakiongozwa na babu kesi.

haina jinsi wakulaum mtalaum ila inabidi tukubali tu kuwa kitu kisipokuwa mahari pake ni uchafu.

kuna watu wanalipa mamilioni ya kodi ila hawa wangine kodi yao wanalipa kwa KESI yeye ndio tra WA mwenge

 

Mbona upo kishabiki sana wewe kidogo babu kesi wewe inaonyesha una chuki binafsi na kesi eeh!
 
Hakuna lolote. mbona Ubungo wamesharudi ? Wewe subiri pitia jioni ndo utajua.
 
Mleta mada umeandika kama we ndio uloendesha oparesheni
mi nadhani pale mwenge n center nzur kwa biashara na lengo la serekali ni kuongeza ajira nchni,chukuen ushauri wangu huu hapa,nnsf wapewe eneo hilo wajenge kituo na majengo meng ya biashara ya kisasa,ili mkusanye kodi nyie wenyewe baada ya huyo babu kesi,ilo linawezekana,lengo letu n kupiga hatua kimaendeleo
 
Pole zao walioumia,
wakati mwingine njaa inatufanya tufanye
vitu hata kama tunajua kuwa tunavunja sheria.
 
Tatizo la serikali yetu ni kufanya mambo kama zima moto. Watajidai endelevu baada ya wiki moja utaona kimya na watu watarudi kwenye maeneo hayo kwa nguvu. Hata kwenye mafuriko ni hivyo hivyo. Mpaka mvua inyeshe ndipo utasikia kauli za kuwataka wahame. Wakati wa kiangazi wanawaona kabisa wakijenga hawasemi kitu. Imekuwa ni serikali ya matukio. Walipaswa pia kufanya doria hata usiku kwani kuanzia saa 1 ndipo biashara huanza kusogezwa maeneo yasiyoruhusiwa.
 
Shikamooo Zembwela kwa karipio lako kali juu ya mwenge stendi sasa safii
 
Mwenge imetakata kabisa baada ya kipindi cha East Africa radio kinachoendeshwa na mwanahabari zembwela kukaripia kwa ukali sana uchafu na uwekaji mabanda pale mwenge stendi leo kumesafishwa kupo safi.

Ama kweli taaluma ya habari ikitumiwa vizuri huwa inaleta manufaa papo hapo.

Asante zembwela kwa kalipio lako.
 
Na mimi shikamoo Zembwela.., yaan nimepita hapo mwenge jana na leo kuna tofauti kubwa saaanaaa.., hakuna kibanda hata kimoja.., jiji litapendeza namna hii.., ila hili zoezi hili liwe endelevu..! SHIKAMOO ZEMBWELA!
 

nDO MAANA WAANDISHI WA HABARI UTAWASIKIA WAKISEMA WAO NI NGUZO YA NNE YA UONGOZI HAPA NCHINI. HAWAJAKOSEA KWA KWELI. NI KAMA VILE WANAZIKUMBUSHA HIZO NGUZO NYINGINE TATU. BIG UP ZEMBWELA
 
tukiwa na tabia ya kupongezana hivi kabla mtu ajafa me naona itakuwa jambo la maana sana sio mpaka mtu afe ndo usikie kweli alikuwa mtu wa watu asiyependa makuu kweli ameacha pengo
 
Bada ya sku 2 wanarudi ndio Ujinga wa hili linchi
 
Kwa Dar hiyo ni nguvu ya soda..Jioni pako full kama kawaida..

Waje waige Arusha..Kusafiii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…