Mwenge social hall ni matapeli wa kutupwa

Mwenge social hall ni matapeli wa kutupwa

UKOSI

Member
Joined
Dec 18, 2012
Posts
35
Reaction score
5
Kuna ukumbi unaitwa mwenge social hall upo mwenge nyuma ya tra karibia na gorofa za jeshi,huu ukumbi una vituko vya ajabu,utapeli,uongo,utaratibu mbovu na huduma mbaya kuliko ubaya unaojua,ili mpambaji atoke nje ya ukumbi itamlazimu atoe laki tatu ikiwa ni kibali cha kuingiza mapambo kutoka nje na kukupa baadhi ya vifaa ambavyo hakwambii,kama haitoshi utaambiwa ulipie seat cover,viti vya wageni kwa sh500 kila kimoja pamoja na taa zinazozidi 20 kwa sh 5000 vitu hivi ni lazima uchuke hapohapo,pia utakutana na majibu yasiyo eleweka,matusi na dharau kutoka kwenye office yao ya booking,chakula wanapika hapo hapo lakini ni kibovu,kwa yeyote anayetaka kufany sherehe hapo awe makini,na kwa utaratibu wao hakuna haja ya kufanya shughuli kwenye ukumbi wao,kwani kumbi zipo nyingi dar,wahusika badilisheni utaratibu wenu na watoeni wanaokaa hapo booking,huyo anayeitwa dada GRACE na huyo mzee ambaye simjui
 
Bora umenishtua. Maana nina shughuli na huo ni moja ya kumbi nilizoelekezwa. Asante mkuu. Dar watu tunakondeana kwa mengi.
 
Wafanyabiashara bwana? sasa ukumbi ukianza kukosa wateja utasikia oohh tumelogwa. Nani akuloge wakati unafukuza wateja kwa mdomo wako mwenyewe?? badilikeni!!
 
Ha ha nasiku nyingi sana sijahudhuria Arus kwenye kumbi? nachukia sana purukushani za maandalizi ya Arusi sijui ukumbi, sijui mapambo, cover maua, kamati sijui ya nini shi...t, najua itafika wakati tutajifunza jambo.
 
poor customer care service,hicho ndo tunakishndwa sisi watz,na tutazidi kuwa maskini tusipobadilika,hapo reception angekuwepo mhindi mambo yangekuwa shwari kabsa,
 
na kwali hiii wataaaribu biashara inaonekana huyo meneja na kamati yake wanatamaa sana ya pesa na ukitaka kuwa mfanya biashara mzuri usiwe na tamaa na sababu hiyo wa2 weng hupoteza mipango
 
bosi wa huo ukumbi aaaangalie saaana anaweza akajikuta anafulia hiv hiv kwa 7babu ya uongozi wake wasiwe na tamaaa kiasi hichooooooo
 
mkuu si huwa wanaweka sanduku la maoni, si vizuri kuharibu biashara za watu kwenye mitandao kuna haja ya kuwashauri wajilekebishe mkuu!
 
mkuu si huwa wanaweka sanduku la maoni, si vizuri kuharibu biashara za watu kwenye mitandao kuna haja ya kuwashauri wajilekebishe mkuu!
Mkuu sehemu nyingi kuna masanduku kama hayo lakini ni geresha tu! Huwa hayafunguliwi, na kama yanafunguliwa malalamiko/ushauri hautiliwi maanani. Dawa ni kuwasuta humu humu!
 
Mbona kumbi nyingi utaratibu wao ndo huo nenda Deluxe nenda Mawela nenda Mwika hao wa Mwenge bei zao zipo chini kumbe
 
Kuna ukumbi unaitwa mwenge social hall upo mwenge nyuma ya tra karibia na gorofa za jeshi,huu ukumbi una vituko vya ajabu,utapeli,uongo,utaratibu mbovu na huduma mbaya kuliko ubaya unaojua,ili mpambaji atoke nje ya ukumbi itamlazimu atoe laki tatu ikiwa ni kibali cha kuingiza mapambo kutoka nje na kukupa baadhi ya vifaa ambavyo hakwambii,kama haitoshi utaambiwa ulipie seat cover,viti vya wageni kwa sh500 kila kimoja pamoja na taa zinazozidi 20 kwa sh 5000 vitu hivi ni lazima uchuke hapohapo,pia utakutana na majibu yasiyo eleweka,matusi na dharau kutoka kwenye office yao ya booking,chakula wanapika hapo hapo lakini ni kibovu,kwa yeyote anayetaka kufany sherehe hapo awe makini,na kwa utaratibu wao hakuna haja ya kufanya shughuli kwenye ukumbi wao,kwani kumbi zipo nyingi dar,wahusika badilisheni utaratibu wenu na watoeni wanaokaa hapo booking,huyo anayeitwa dada GRACE na huyo mzee ambaye simjui

naomba tafsiri ya neno utapeli!naona maelezo yako hayasadifu kichwa chako cha habari.
ningekuwa mimi ndie mmiliki wa huo ukumbi tungekutana na mahakamani unipe ushahidi wa hizi tuhuma na kuniharibia biashara.
wakati mwingine usidanganyike na hizi fake id's kuchafulia watu biashara,inaweza ikakugharimu sana mkuu.
nimesema kiroho safi.
 
mkuu si huwa wanaweka sanduku la maoni, si vizuri kuharibu biashara za watu kwenye mitandao kuna haja ya kuwashauri wajilekebishe mkuu!

Sanduku la maoni limewekwa na mfunguaji mkuu ndiye huyo huyo anayekujibu mbovu, kwa mtindo kama huu tutafika wapi??? Kifupi ni kwamba pale unapohitaji kitu utakiona thamani yake ukishapata thamani yake hutaiona kamwe. Ulevi wa madaraka ndiyo huo.
Ni sawa na mwanamke aliyeenda kwa mganga ili eti apewe dawa aweze kutakatisha nyota yake aweze kuolewa maana alikaa muda mrefu bila hata boyfriend, mganga wa kienyeji alimsoma vizuri sana yule mwanamke na kugundua kasoro zake akamtengenezea dawa, akamwambia dawa hii unatakiwa uitumie kwa kuoga kwa muda wa wiki tatu. Mara ukioga usikae ndani nenda kutembea tembea, yeyote utakaye kutana naye unatakiwa umuonyeshe tabasamu la hali ya juu, msalimie kuwa mchangamfu sana. Hakikisha unavaa vizuri na kamwe usinune. Ndani ya wiki moja na nusu alipata mchumba na harakati za kufunga pingu za maisha zikiaanza. Ndoa ikafungwa wakaendelea na maisha yao kama mume na mke.
Mwanamke akajua kisha pata akakunjua makucha yake ya awali. Hakika ndani ya miezi sita ndoa ilishageuka kuwa ndoano yenye chambo ya shubiri. Haikukalika.

Mfano huu kifupi ni kwamba hadi umepoteza hutaona umuhimu wake.
 
Nadhani tatizo hapo customer service tu lakini mambo mengine kumbi nyingi zipo hivyo ukitaka kumbi ambazo huduma kama mapambo utafuta mwenyewe mpambaji zipo chache sana nzuri nyingi kila huduma hapo hapo except Cake , Mc na Muziki.

Pia uzoefu wako unaonekana mdogo kwenye haya mambo.
 
Back
Top Bottom