Carnivora
JF-Expert Member
- Jan 26, 2018
- 3,650
- 6,028
Nimesoma mahali kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe ametunukiwa nyumba na maaskofu wa kanisa lake. Hiki kitu kikatrigger (kuamsha) hisia zangu za siku nyingi kidogo ambazo nimewahi kuwaza juu ya eneo la Mwenge Dar es Salaam na maeneo ya jirani.
Kanisa la FGBF liko karibu kabisa na roundabout ya Mlimani City ni jirani na Mwenge pia. Kanisa hili lilianzishwa na Askofu Kakobe miaka karibia 30 iliyopita. Sijui lilianzia wapi, ila kwa sasa makao makuu yapo pale. Kakobe alitikisa sana enzi zake.......alikua maarufu mno na alijizolea waumini wengi sana. Kipindi hicho ukitaka uwe mlokole hasa basi ume unasali kwa Kakobe. Nakumbuka aliyewahi kuwa baba mkwe wangu mmoja ( my x's dad) alikataa kazi ya mashahara mnono TCC pale kisa ni kampuni ya sigara. Dah! Kakobe hata akifa leo kaacha legacy.
Sasa, kuna haya makanisa yaliyoibuka baadae ambayo yamekusanya watu wengi sana.....nayo yana asili ya Mwenge.
1. Efatha.....kanisa hili liko pale karibia na SUMA JKT
2. Amka uangaze....Mwamposa. Huyu bwana alianzia Mwenge pale ambapo kwa sasa kuna kituo cha mafuta cha Oryx, roundabout.
3. Kuna mtu anaitwa Kuhani Musa, yuko jirani tu pale na The Calabash Bar naye anawajaza sana kwa ibada na maombi yake.
Swali dogo la kujiuliza. Kuna nini eneo lile lina nini mpaka makanisa haya ya kiroho yanaanzishwa pale? Or it's just a co-incidence?
Kuna watu maalum wanalengwa? Kwamba wanapatikana kwa urahisi eneo lile? Kuna siri gani nyuma ya jambo hili?
Mshana Jr njoo unisaidie huku.